Visiwa Vipya vya Siberia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani

Visiwa Vipya vya Siberia (kwa Kirusi: Новосиби́рские Oстрова Novosibirskiye Ostrova) ni funguvisiwa la Bahari Aktiki katika kaskazini ya Urusi. Viko upande wa kaskazini wa pwani ya Siberia kati ya Bahari ya Laptev na Bahari ya Siberia Mashariki.

Ramani ya Visiwa Vipya vya Siberia (Philippe Vandermaelen "Ramani ya Urusi ya Asia", c. 1820). Ardhi ya Bunge ilikuwa haijagunduliwa, hivyo Kisiwa cha Faddeyevsky na Kisiwa cha Kotelny vilizingatiwa kando.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Mahali pa Visiwa vya New Siberian ndani ya Urusi.

Ni visiwa vikubwa 13 pamoja na idadi kubwa ya visiwa vidogo ambavyo kwa jumla vina eneo la nchi kavu ya Km² 29,000. Kikubwa zaidi ni kisiwa cha Kotelny chenye eneo la km2 11,700. Visiwa vyote hufununikwa na theluji na barafu. Hakuna wanadamu wanaoshi huko.

Mifupa ya viboko, vifaru na mamothi inapatikana, ikionyesha kwamba zamani tabianchi ilikuwa tofauti.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Kusoma zaidi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Urusi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Visiwa Vipya vya Siberia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.