Nenda kwa yaliyomo

Virginia Phiri

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Virginia Phiri (alizaliwa mwaka 1954) ni mwandishi wa Zimbabwe anayejihusisha na masuala ya usawa wa kijinsia (feminist writer).[1]

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Virginia Phiri alizaliwa mwaka 1954 katika jiji la Bulawayo, ambalo ni jiji la pili kwa ukubwa nchini Zimbabwe.

Akikulia katika familia ya wanasiasa waliokuwa wanahamasisha kupitia chama cha Zimbabwe African Peoples Union (ZAPU), Phiri alijihusisha kikamilifu na vita vya ukombozi vya Zimbabwe akiwa na umri wa miaka 17. Baadaye, mwaka 2000, akiwa pamoja na kikundi cha Zimbabwe Women Writers, alichangia katika mkusanyiko wa makala uliopewa jina la Women of Resilience – the voices of women ex-combatants.

Mwaka 1972, aliondoka nchini Zimbabwe kuelekea Botswana jirani, akiwa njiani kuelekea Zambia..[2]

  1. Zimbabwe Women Writers (2000). Women of resilience - the voices of women ex-combatants. South Africa: Southern African Research. ISBN 978-0797420021.
  2. "Virginia Phiri - Foreign Policy Research Institute". www.fpri.org (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-05-29.
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Virginia Phiri kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.