Virginia Khunguni
Virginia Khunguni ni mwanaharakati wa haki za wanawake kutoka Malawi. Yeye ni mwanzilishi na mkurugenzi wa shirika la Girls Arise for Change Archived 2025-04-06 at the Wayback Machine, shirika linalolenga kuwawezesha wanawake ili kuhamasisha mabadiliko ya kijamii na kitamaduni. Shirika hilo limeongoza mipango ya kupambana na ajira ya watoto, ndoa za utotoni na unyanyasaji wa kingono. Khunguni ni mpokeaji wa tuzo ya Queen's Young Leader Award kwa kazi yake barani Afrika.[1][2][3][4]
Khunguni alihitimu shahada ya Mawasiliano ya Umma akijikita katika uandishi wa habari kutoka Chuo Kikuu cha Mahatma Gandhi.[5]
Maisha binafsi
[hariri | hariri chanzo]Khunguni alizaliwa Carolina Kaskazini, nchini Marekani. Yeye ni mtoto wa mwisho kati ya ndugu wawili wa kiume. Miaka michache baadaye, walihamia Blantyre, Malawi. Khunguni alipoteza wazazi wake na akalelewa na malezi ya babu na bibi zake.[5]
Akiwa anakua, Khunguni alitamani kuwa mtayarishaji wa muziki, aliota kuwa mwanamke wa kwanza mtayarishaji wa muziki nchini Malawi. Khunguni alienda mara kwa mara studio kujifunza uzalishaji wa muziki na uhandisi wa sauti. Mtayarishaji mmoja alimbaka,ambapo baada ya tukio hilo,babu na bibi zake walijibu kwa kumtishia kumfukuza nyumbani ikiwa angehusika tena katika matukio ya unyanyasaji wa kingono. Bibi yake pia alimwonya aache sekta ya muziki kwa kuwa inajulikana kutawaliwa na wanaume. Kutokana na unyanyapaa unaohusishwa na waathiriwa wa ubakaji, Khunguni alibaki kimya, aliacha muziki na akaamua kusoma Uandishi wa habari.[5]
Akiwa mwandishi wa habari, Khunguni alikutana na waathiriwa wengi wa kimya wa unyanyasaji wa kingono, akaamua kuanzisha kipindi cha redio cha "Girls Arise" ili kushughulikia suala hilo. Kipindi hicho kiliwajumuisha waathiriwa wa ukatili wa kijinsia, wataalamu wa haki za binadamu na afya walialikwa kutoa ushauri wao. Wanajamii pia walishiriki kujadili juhudi za kushughulikia tatizo hilo na kupunguza unyanyapaa unaohusiana nalo.[5][6]
Kipindi hicho cha redio kilipata mwitikio mkubwa kutoka kwa jamii, hata kulikuwa na taarifa kutoka kwa viongozi wanawake wa jamii. Khunguni aliamua kuwa kipindi cha redio pekee hakikutosha kumaliza ukatili wa kijinsia uliokithiri. Mwaka 2013, Khunguni alianzisha shirika la Girls Arise for Change Archived 2025-04-06 at the Wayback Machine.[7] Linalenga kupinga mitazamo na kumaliza mila zinazokwamisha kuboreshwa kwa hadhi ya wanawake nchini Malawi. Shirika linahamasisha haki za wanawake vijana katika afya na elimu. Khunguni aliwasiliana na viongozi wa jamii kutoka wilaya mbalimbali na kuanzisha muundo wa msaada wa kijamii ili kupanua mpango huo.[5][8][6][9]
Girls Arise for Change[7] imeokoa na kutoa msaada kwa wasichana waliokimbia ndoa za utotoni na wale waliolazimishwa kufanya ajira ya watoto au hata ukahaba. Shirika pia hutoa msaada wa kitabibu na kisaikolojia kwa waathiriwa wa ubakaji. Khunguni alishirikiana na mashirika ya afya kuanzisha kliniki tembezi katika maeneo ya mbali ili kuelimisha vijana na kutoa huduma za afya ya uzazi.[3][1][5][10]
Khunguni alijua kuwa umaskini ni sababu kubwa ya ndoa za utotoni na ajira ya watoto; alitambua kuwa wengi hawawezi kumudu elimu ya juu na hulazimika kukubali hali hizo. Hivyo,shirika hilo la Girls Arise for Change[7] hutoa mafunzo ya ufundi stadi kwa wasichana. Shirika limeshirikiana na watu kutoka Nigeria, Marekani na Kenya ili kuhakikisha bidhaa wanazotengeneza zinauzwa na waweze kujitegemea.[11][5] Wamewafundisha wasichana katika nishati mbadala, sanaa za upishi, videography na ubunifu wa mavazi; Girls Arise for Change imewasaidia zaidi ya wanawake vijana 3,500.[5][11][12]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- 1 2 "Virginia Khunguni | Queen's Young Leaders" (kwa Kiingereza). Queen Elizabeth Diamond Jubilee Trust. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 4 Agosti 2020. Iliwekwa mnamo 2 Novemba 2020.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Chiumia, Thom. "The Queen honours Malawi young talent: Virginia Khunguni". www.nyasatimes.com. Malawi Nyasatimes. Iliwekwa mnamo 2 Novemba 2020.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - 1 2 "Malawi's Virginia Khunguni to receive special award from The Queen". Nyasa Times. Iliwekwa mnamo 2 Novemba 2020.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Her Majesty the Queen to honour young Malawian woman with Queen's Young Leaders Award". www.maravipost.com. The Maravi Post. Iliwekwa mnamo 2 Novemba 2020.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - 1 2 3 4 5 6 7 8 Twea, Brenda. "Virginia Khunguni: Founder Of Girls Arise For Change | The Nation Online | Malawi Daily Newspaper". The Nation Online. Nation Publications Limited. Iliwekwa mnamo 2 Novemba 2020.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - 1 2 McCool, Alice. "Women protest against sexual violence in Malawi". Reuters. Iliwekwa mnamo 2 Novemba 2020.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - 1 2 3 "The Queen Honours Malawi Young Talent Virginia Khunguni". Girl's Arise For Change. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 6 Aprili 2025. Iliwekwa mnamo 9 Julai 2025.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Whelan, Alan. "Tackling violence against women in Malawi - Malawi". ReliefWeb (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2 Novemba 2020.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Gender Equality and Women's Empowerment | Malawi". USAID (kwa Kiingereza). 15 Novemba 2019. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Februari 24, 2013. Iliwekwa mnamo 2 Novemba 2020.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Findings on the Worst Forms of Child Labor - Malawi | U.S. Department of Labor". www.dol.gov. Iliwekwa mnamo 2 Novemba 2020.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - 1 2 "The Countess of Wessex meets Queen's Young Leaders in Malawi". The Royal Family (kwa Kiingereza). The Royal Household. 15 Machi 2017. Iliwekwa mnamo 2 Novemba 2020.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Brides, Girls Not. "Malawi - Child Marriage Around The World. Girls Not Brides". Girls Not Brides (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2 Novemba 2020.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)