Nenda kwa yaliyomo

Violet Barasa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Violet Awindi Barasa (Sikhendu, Kaunti ya Bungoma, 21 Juni 1975 - Webuye, 12 Februari 2007) alikuwa mchezaji wa voliboli wa Kenya. Jina lake la asili pia huandikwa Baraza.

Alikuwa nahodha wa muda mrefu wa timu ya wanawake ya kitaifa ya voliboli ya Kenya. Baraza alishiriki akiwa kwenye yimu ya Kenya katika michezo ya olimpiki ya 2000 na 2004 , mara tatu kwenye Kombe la Dunia la Voliboli na kwenye mapambano kadhaa ya bara Afrika. [1].

Alikuwa miongono mwa Wakenya wachache kucheza voliboli ya kulipwa katika nchi za ng'ambo, akichezea kilabu cha Al-Ahly nchini Misri, Vileo na Unic-Romania nchini Romania, Panellinios nchini Ugiriki na Chuo Kikuu cha Dicle nchini Uturuki.

Alifariki mnamo Februari 2007 katika Hospitali ya Wilaya ya Webuye na sababu za kifo chake hazikuwekwa wazi. Wakati wa kifo chake, alikuwa bado mchazaji wa kawaida na kilabu cha voliboli cha Kenya Commercial Bank ,ingawa alikuwa amechujwa kwenye kikosi cha kitaifa.

Alikuwa ameolewa na Kenneth G. Kimani, aliyezaliwa katika kata ndogo ya t Karatun, kata ya Ndarugu ,wilaya ya Kiambu , taarafa ya Gatundu katika Mkoa wa Kati. Alisomea shule ya msingi ya Ndarugu na kisha kijiunga na shule ya upili ya Muhoho, na kisha baadaye kujiunga na Chuo kikuu cha Jomo Kenyatta ,Juja.

Ken kama mkewe, alikuwa miongoni mwa Wakenya wachache kucheza voliboli ya kulipwa katika mataifa ya ng'mbo ,akichezea Panellinios nchini Ugiriki Chuo Kikuu cha Dicle nchini Uturuki.

Kenneth na Awindi hawakuwa na mtoto.

Ken sasa ndiye msimamamizi wa GTN (Gospel Television Network)

  1. The Standard, 14 Februari 2007: Former national team captain dies in hospital
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Violet Barasa kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.