Vincent shemasi
Jump to navigation
Jump to search
Vinsenti alikuwa shemasi wa Kanisa la Zaragoza, Hispania.
Mzaliwa wa Huesca, aliteswa vikali sana, akafa kwa ajili ya dini yake huko Valencia mwaka 304, wakati wa dhuluma ya Kaisari Dioklesian.
Heshima ya watu kwake kama mtakatifu ilienea haraka sana katika Kanisa lote.
Sikukuu yake huadhimishwa kila mwaka tarehe 22 Januari.
Tazama pia[hariri | hariri chanzo]
- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
![]() |
Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Vincent shemasi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |