Vincent Long Van Nguyen
Mandhari
Vincent Nguyễn Văn Long O.F.M. Conv. (alizaliwa 3 Desemba 1961) ni kiongozi wa Kanisa Katoliki mwenye asili ya Vietnam nchini Australia.
Tarehe 5 Mei 2016, Papa Fransisko alimteua kuwa Askofu wa nne wa Parramatta, Australia. Amekuwa askofu tangu mwaka 2011 baada ya kuhudumu kwa miaka kadhaa katika uongozi wa Wafransisko, kwanza nchini Australia na baadaye Roma. Yeye ndiye wa kwanza aliyezaliwa Asia kuwa askofu nchini Australia na askofu wa kwanza mwenye asili ya Vietnam kuongoza jimbo nje ya Vietnam.[1]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Murphy, Damien (6 Mei 2016). "Pope Francis appoints Vincent Long Van Nguyen new Catholic bishop for Parramatta". The Sydney Morning Herald. Iliwekwa mnamo 13 Desemba 2017.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
| Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |