Vilabu vya ukahaba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Vilabu vya wahudumu wa jinsia ya kike ni hulka ya kawaida katika sekta ya burudani inayotendeka usiku nchini Ujapani na pia katika nchi za Asia ya mashariki na maeneo nje ya Asia yenye wakazi wengi kutoka Asia ya mashariki. Vilabu hivi vinawaajiri wafanyakazi ambao hasa ni wanawake na wanaohudumia wanaume wanaotafuta mahali pa kujiburudisha kwa vinywaji na mazungumzo. Hivi karibuni Vilabu vya wahudumu wa jinsia ya kiume vimeanzishwa, vinafanana na vilabu vya wahudumu wanawake ambapo kimsingi wafanyakazi walioajiriwa ni wanaume wanaohudumia wanawake. Vilabu hivi vinachukuliwa kama sehemu ya mizu shōbai au "water trade"(biashara ya maji) katika Ujapani.

Vilabu vya Wahudumu wa jinsia ya Kike[hariri | hariri chanzo]

Ujapani[hariri | hariri chanzo]

Picha la mabaa ya wahudumu katika Kabukichō, Tokyo

Nchini Ujapani, vilabu hivi huitwa kyabakura kyabakura (キャバクラ?) neno ambalo ni mchanganyiko wa maneno kyabare( "cabaret") kyabarē (キャバレー?, lit. "cabaret") na kurabu( "club")kurabu (クラブ?, lit. "club") Wahudumu hujulikana kama kyabajō (キャバ嬢?) "club girl" (wasichana wa kilabu) na huchaguliwa kutegemea urembo na utu yao. Kazi wanofanya kwa niaba ya wateja ni kama vile kuwawashia sigara, kuwapa vinywaji, kuchangia mazungumzo, na kuimba karaoke kwa jitihada ya kuwaburudisha wateja. Wanawake hawa wanaweza kulinganishwa na geisha wa miaka awali kwa kuwaburudisha makundi ya wafanyikazi wanaume ("salarymen") baada ya kazi. Vilabu hivi vinatenganishwa na vilabu viitwavyo "strip club" kwa ajili ya kutokuwa kwa kucheza ngoma au kuenda uchi. Mara nyingi mwanamke ambaye ana ujuzi katika kutengezeza vinywaji vya kila aina ("mixology") huajiriwa kama mtumishi wa vinywaji ("bartender"). Mwanamke huyu pia anaweza kuwa meneja au mamasan. Ingawa bei ya vinywaji inaelekea kuwa ghali zaidi kuliko katika baa nyingine na ada ya kuingia inalipizwa, vilabu vingi huwapa wateja nafasi ya kunywa kiasi wanachotaka -bila kikomo- cha baadhi ya vinywaji nomihōdai (飲み放題?) ("bottomless Refills") kama vile shōchū.

Wahudumu wanahitajiwa kunywa pamoja na wateja wao kila usiku, kwa ajili hii huenda wanapata matatizo kutokana na kunywa kiasi nyingi ya pombe. [1] Baa nyingi hufanya kazi kwa mfumo ambao wahudumu hupokea asilimia ya mauzo ya pombe. uriage (売り上げ?)

Wateja kwa ujumla husalimiwa mlangoni na hukalishwa mbali kutoka na wateja wengine. Katika baadhi ya matukio, mteja anaweza kuchagua atakaye mhudumia, lakini mara nyingi ni kilabu kinachochaglia mteja mhudumu. Aidha, mhudumu huondoka baada ya muda kiasi fulani au idadi ya vinywaji fulani, ili kumpa mteja nafasi ya kuona uso jingine. Wakati nyingi kuna mwanaume nje ya kilabu aliyeajiriwa kuwasapa wateja wengine, kazi hi pia inaweza kuangukia mhudumu wa kilabu (kawaida mhudumu huyu ni ajiri mpya).

Wahudumu hawa pia wanawajibu wa kushiriki katika "paid dates" dōhan (同伴?) ambako wanakutana na wateja wao nje ya kilabu na masaa ya kufanya kazi ya kawaida. Mfumo huu inawahimiza wateja kurudi wa kilabu fulani ("repeat patronage"). Wakati mwingine hutokea ngono katika mikutano haya. [2] Kiasi cha malipo ya wahudumu huweza kuondolewa ikiwa wankosa kujihusika katika mikutano ya nje au dōhan ya kutosha.

Kuna kilabu ya wahudumu katika eneo ya Tokyo inayohudumia wasagaji. [3]

Kuwa mhudumu katika vilabu hivi ni ajira maarufu miongoni mwa wanawake vijana wa kigeni katika Ujapani. Kuna hitaji kubwa ya wafanyikazi katika sekta hii lakini ruhusa ya kufanya kazi ni ngumu kupata nchini Ujapani, wengi huchagua kufanya kazi kinyume cha sheria. Wakati mwingine vilabu huchukua nafasi hii kufaidika kutokana na hali wanawake hawa waliomo kutokana na kupata ajiri kinyume cha sheria. [4] Hatari katika sekta hii zilionyeshwa mwaka wa 1992, wakati Carita Ridgeway, mhudumu kutoka Australia, alipewa madwa ya kulevya na kuuawa baada ya "paid date", na mwaka wa 2000 wakati Lucie Blackman, mhudumu kutoka Uingereza, alitekwa nyara, kubakwa na kuuawa na mteja. Serikali iliahidi kukomesha biashara ya vilabu ambavyo viliajiri wahudumu wageni haramu, lakini operesheni ya kisiri mwaka wa 2006 iligundua kwamba vilabu kadhaa vilikuwa tayari kuajiri wanawake wageni kinyume cha sheria. [2] Mwaka 2007, serikali ilianza kuchukua hatua dhidi ya vilabu hivi, na kusababisha idadi kubwa ya vilabu hivi kufungwa, aidha wengi wa wahudumu wa asili za kigeni walikamatwa na kufukuzwa nchini zao asili. Sasa kufuata sheria kali, ni halali tu kwa wanawake wa kigeni kufanya kazi kama wahudumu ikiwa wao ni raia wa Kijapani au wana ruhusa kutokana na kuolewa kwa raia wa Kijapani.

Mabaa ya Makumbwe ("Snack Bars")[hariri | hariri chanzo]

Baa la Makumbwe, Ujapani (rejelea kutokuwa kwa vioo)

"Snack bar" (スナックバーsunakku ba), au "snack" kwa kifupi, ni aina ya baa ya wahudumu, baa hii inaandaa pombe na kuwaajiri wafanyakazi wanawake wanaolipwa kutumika na kuongea na wateja wanaume. Ingawa hawalipishi ada ya kuingia (na mara nyingi hawataji bei ya vyakula na vinywaji katika "menu"), kwa kawaida wana malipo holela (na ghali)au hulipisha kulingana na saa na "bottle charge". Wateja hununua chupa katika jina yao wenyewe na ni huadhimishwa kwa ziara zao zijazo. Mabaa haya hutengwa kikabila.

Kumbi nje ya Ujapani[hariri | hariri chanzo]

Baa hizi pia hupatikana katika nchi nyingine za Asia ya mashariki, Guam, na katika maeneo nchini Marekani kama vile California na Hawaii. Katika eneo ya Hawaii liitwalo Oahu nusu ya mabaa 300 yana leseni ya baa ya wahudumu. Katika nchi ya Guam na eneo la Hawaii mbaa haya yanaendeshwa na huajiri watu wa asili ya Kikorea.

Baadhi ya mabaa katika nchi ya Thailand hujijulisha kama kama baa ya wahudumu, ingawa mabaa hayo hufanana kimsingi na "go-go bars" ambako hakuna kucheza ngoma.

Vilabu vya wahudumu wa jinsia ya Kiume[hariri | hariri chanzo]

Picha la kilabu cha wahudumu wa jinsia ya kiume katika Kabukichō, Tokyo

Vilabu ja:ホストクラブ hivi vinafanana na vilabu vya wahudumu wajinsia ya kike, ijapokuwa kwamba wateja ni wanawake na wanaohudumia na wanaume. Baadhi ya vilabu hivi pia huwaajiri wanawake ambao wamebadili jinsia na wakawa wanaume. [5] Vilabu kwa kawaida hupatikana katika maeneo yenye idadi kubwa ya wakazi Ujapani, kuna vilabu vingi vya aina katika wilaya za Tokyo kama Kabukichō, na Osaka Umeda na Namba. Wateja wake wa kawaida ni mabibi ya wanaume tajiri na wanawake wanaofanya kazi kama wahudumu katika vilabu vwa wahudumu wa jinsia ya kike. [6]

Kilabu cha kwanza cha aina hiki kilifunguliwa katika eneo la Tokyo mwaka wa 1966. [7] Mwaka wa 1996, idadi ya vilabu hivi katika Tokyo ilikadiriwa kuwa 200, na usiku wa burudani bila ngono inaeweza kuwa na gharama ya $ 500 to $ 600. Profesa wa masomo ya wanawake alieleza kuwa kuwepo kwa vilabu vya aina hivi kulitokana na wanaume Kijapani kutosikiliza matatizo ya wanawake, na tamaa ya wanawake kumtunza mtu na kupendwa pia. [8]

Wahudumu wa jinsia ya Kiume[hariri | hariri chanzo]

Huwaandalia wateja vinywaji na mara nyingi hushirika katika mazungumzo ya kipenzi ("flirt") na wateja wao, zaidi kuliko wahudumu wenzao wanawake. Mazungumzo haya kwa ujumla huwa ya kuchesha, yenye lengo ya kuburudisha; wahudumu hawa huwa ni machale ambao mara nyingine huweza kutenga hadithi kwa ustadi au huenda wanauwezo katika kiini macho. Baadhi ya vilabu hutenga sehemu ya kilabu ambako wahudumu wanaweza kuwaburudisha wateja kwa kucheza ngoma, kuimba, kufanya kiini macho au kutoa vichekesho.

Umri ua wahudumu kwa kawaida huwa kati ya 18 hadi 25. Huchukua jina la kujibandika ("stage name") (源氏名), kwa kawaida jina hili huazimiwa kutoka mhusika katika manga, filamu, au mtu muhimu kihistoria. Mara nyingi hata huelezea tabia zao. Wahudumu aidha hawawezi kupata kazi nyingine, au huvutwa kwa matarajio ya mapato makubwa kutokana na tume. [7]

Vilabu vya wahudumu wanawake katika Tokyo vinaajiri wanaume wanaosimama nje ya kilabu na kuwasapa wateja wapya mara nyingi katika vilabu vinavyohudumia wanawake ni wahudumu wenyewe ambao hutafuta wateja (tendo hili linajulikana kama "catch" (キャッチ), lakini haya ni kawaida tu katika wahudumu wenye umri na ujuzi mdogo. Kwa kawaida wahudumu huvaa suti nyeusi, shati, mapambo ya fedha , pia huwa na ngozi hadharani [3] na nywele iliyobadilishwa rangi yake ya asili. Hivi karibuni, vilabu ambapo wahudumu huvaa nguo yao ya kawaida vimeongezeka, lakini bado mavazi desturi ni suti. Katika vilabu hivi, yaweza kuwa (私服デー-shifukudē) au "own clothes day" ambako wahudumu wanaweza kuvaa nguo zao za kawaida.

Malipo kwa kawaida ni kwa tume ya mauzo ya kinywaji, au uriage (売上), na mara nyingi wahudumu hunywa zaidi ya kiasi wanachoweza kunywa, aidha hujaribu kuficha ulevi wao. Kwa sababu ya ujira mdogo mno, karibu mtu yeyote anaweza kuwa mhudumu bila kujali sura au uwezo yake ya kuburudisha (kutegemea baa) Hata hivyo, wahudumu ambao hawawezi kuongeza mauzo yao kwa kawaida wanaacha kazi haraka sana, kwa sababu ya ujira ndogo. Kwa kawaida mazingira katika mabaa haya ni ya ushindani mno, kutokana na kuwa wakati mwingine makumi ya maelfu ya dola yanatolewa kwa wahudumu ambao wanaweza kufikia mauzo ya juu.

Vinywaji[hariri | hariri chanzo]

Wengi ambao huziara vilabu hivi ni wanawake wahudumu ambao humaliza kazi saa 1:00 au 2:00, kwa ajili hii wanasababisha mabaa haya, mara nyingi, kufanya biashara usiku kucha, na wahudumu katika mabaa hayo hufanya kazi hadi kuchoshwa mno. Polisi wamejaribu kukomesha mfumo huu wa vilabu kufanya kazi usiku kucha. Hii ni kwa sababu wateja ambao hawakuweza kulipa madeni yao walianza kujihusisha katika ukahaba knyume ya sheria ili kulipa madeni yao. Siku hizi vilabu hivi hufunguliwa saa 4:00 na hufunga kati ya usiku wa manane na saa 2:00. Hata baada ya amri ya polisi, baadhi ya vilabu bado huwa wazi usiku wote, au, vimeongeza mikutano baina ya wahudumu na wateja nje ya vilabu zoezi lijulikanalo kama "new stategy". Bei ya vinywaji huanzia ¥ 1000 (Dola 10) lakini inaweza kufikia kote 3 million yen (Dola za Marekani 25,000) kwa chupa ya champagne.

Baada ya kununua chupa la champagne kwa kawaida kuna zoezi liitwalo 'champagne call' (シャンパンコール). Wahudumu wote ya kilabu hukusanyika kwa meza ya mteja aliyeamrisha chupa cha champagne na hutoa burudani kwa wimbo, majadiliano nk. Mteja hunywa champagne moja kwa moja kutoka kwenye chupa, akifuatiliwa na mhudumu aliyemchagua, na kisha wahudumu wengine walizokusanywa. Tauli yenye maji hutiliwa chini ya kidevu cha wateja na wahudumu wakati wao wa kunywa ili kuzuia mwagiko mwingi wa champagne. Zoezi hili hutofautiana kutoka kilabu kwa kilabu, na ni huaminiwa kuwa na asili katika kilabu kiitwacho Ryugujo katika eneo la Kabukicho chenye meneja jinale Yoritomo.

Kawaida pia ni mnara wa champagne "champagne tower" (シャンパンタワー) unaoweza kufanyika kusherehekea matukio maalum. Bilauri za champagne hupangwa katika piramidi, na champagne hutiwa kwenye bilauri ya juu na hutiririka kwa bilari zote zingine. Mnara wa champagne hutumia angalau vyupa 6, lakini kwa mnara wa matabaka 7,vyupa 20 zinaweza kutumika. Kutegemea na aina ya champagne iliyotumika, gharama ya mnara inaweza kuwa kati ya 1,000,000 ~ ¥ 2,000,000.

Tabia[hariri | hariri chanzo]

Katika ziara ya kwanza kwa kilabu, mteja hupewa 'menu' ya wahudumu, (男メニュー) na hupata nafasi ya kumchagua mhudumu angependa kukutana naye kwanza. Mteja atakutana na baadhi kubwa ya wahudumu katika kilabu usiku huo na atapewa kadi zenye majina ya wahudumu hao. Baada ya mteja kuamua mhudumu atakaye, anaweza kumfanya mhudumu huyo kuwa mhudumu wake wa kudumu (指名), na mfanyakazi huyo atapokea asilimia fulani ya mauzo yanayotokana na mteja huyo. Mteja anaweza kumchagua mhudumu huyo kwa kununua chupa kiitwacho "keep bottle" (chupa cha pombe kitakachookolewa wakati ujao),kusema kua amevutiwa na mhudumu huyo, au kumkaribisha mhudumu akae karibu naye. Vilabu vingi hufanya kazi kwa mfumo ambako mhudumu aliyechaguliwa kwanza ndiye anayedumu "permanent nomination" (永久指名) na mteja hawezi kubadili mhudumu huyo, ijapokuwa chini ya mazingira maalum ambayo yanapaswa kujadiliwa na kilabu.

Wakati mwingine wahudumu na wateja huenda mkahawani au kwa karaoke(mahali ambako wanaweza kuimba) baada ya biashara; hii inarejelewa kama "after"(baada) na si tabia nzuri. Kukaa muda mrefu katika kilabu huhesabiwa kama njia 'sahihi' ya kumtunza mhudumu wako. Hata hivyo ni kuna uwezekano wa kuenda safari ya siku moja au kusafiri na mhudumu, lakini mhudumu lazima awe yule aliyechaguliwa awali. Kukutana au kuwasiliana na mteja ambaye si mteja wako mwenyewe ni kinyume cha 'sheria' ya wahudumu na mhudumu akigunduliwa akiyatenda makosa haya huenda hulipizwa faini au hupoteza ajira.

Vinywaji vinaweza kununuliwa 'on tab' (掛け売り) ikiwa mteja hana fedha za kutosha yaani mteja huwa na deni kwa kilabu. Nakala ya kitambulisho yao itachukuliwa, vilevile nambari ya simu yao na anuani, pamoja na ahadi ya kulipa wakati watakapopata mshahara au mwisho wa mwezi. Ikiwa mteja halipi mwenyeji atahukumiwa kwa niaba yake. Kuenda kulipa deni hujulikana kama 'kaishu' (回收).

Ni tabia mbaya kuondoka na kumwacha mteja peke yake, na tno hili lina jina "only" (オンリー) inayomaanisha 'tu'. Wakati mwingine tukio hili haliwezikusaidiwa (kwa mfano katika mchanganyiko baada ya "champagne call") na msamaha huombwa kwa mteja. A mteja ambaye hunywa na hutenda mabaya, anasema matusi , na huleta tatizo wakati wa malipo, au huleta matatizo kwa wahudumu na wateja wengine anajulikana kama "painful customer" (痛客). Wao huweza kuwa marufuku kutoka kilabu.

Kupokea busu katika elevator (chombo cha kuwasafirisha watu kutoka ghrorofa moja hadi jingine katika jumba) hujulikana kama 'ere chu' (エレチュー).

Mkakati wa Biashara[hariri | hariri chanzo]

Kawaida, wahudumu hujaribu kuwafanya wateja wahisi wanapendwa bila kujamiiana nao, kwa ajili ya kitendo hicho kuchukua muda na nishati. [7]Wakati mwingine, kwa mfano kama mteja amelipa kiasi kikubwa cha fedha na / au kama mhudumu wake anampenda, mhudumu anaweza kufanya ngono na mteja. [3] Kama mhudumu hukutana na mteja fulani mara kwa mara, wana nafasi kubwa ya kufanya ngono kuliko mhudumu huyo na mteja mwingine ambao hawajakutana sana awali. Mhudumu anayefanya ngono na mteja wake huitwa, kwa mfano 'colourful love business' (色恋営业), 'colourful love' (色恋), 'colourful guy' (色彼), 'pillow business' (枕営业) au 'pillow' (枕).

Kuna njia nyingine ya 'biashara', kwa mfano 'biashara pepe' (メール営業) ambapo mhudumu huwatumia wateja wake barua pepe mara kwa mara ili kuhakikisha marejeo yao. Vilevile huweza kuwapigia wateja simu, lakini zoezi hili limepoteza umaarufu kwa ajili ya barua pepe. Wahudumu kwa kawaida hubeba simu ya biashara (営业电话) na simu ya kibinafsi.

Maandishi na filamu[hariri | hariri chanzo]

Chuku (Fiction)[hariri | hariri chanzo]

Kuna magazeti kadhaa kwa mfano, Men's Knuckle, ambayo huhudumia wahudumu, na mara nyingine pia waajiri na mashabiki wao.

Kuna vipindi vya runinga, riwaya, michezo, manga(na anime) ambayo yanahusisha vilabu/mabaa ya wahudumu. Km. Club 9 , Bloodhound na Ouran Koukou Host Club ) Hizi zinalenga watazamaji kwa ujumla, na huonyesha jinsi vile vilabu vimekuja kuwa sehemu ya kawaida, kwa kiasi fulani, nchini Ujapani. Riwaya jinaleTokyo (2000), iliyoandikwa na mwingereza Mo Hayder, ilikuwa na mhusika mkuu akiwa mhudumu. Rosa Kato muigizaji aliyekuwa mhusika mkuu katika kipindi kilichotozwa na TV Asahi jinalo "Jotei" ambako yeye aliigiza kama mwnafunzi maskini ambaye alilazimishwa kuwa mhudumu baada ya mamake kufa kutokana na ugonjwa wa saratani

Yasiyo Chuku ("Non-fiction)[hariri | hariri chanzo]

Shohei Imamura(1970) ni kipindi History of Postwar Japan as Told by a Bar Hostess (にっぽん戦後史 マダムおんぼろの生活 Nippon Sengoshi: Madamu Onboro no Seikatsu?) kinachoelezea habari ya mhudumu / kahaba katika eneo la Yokosuka, Kanagawa.

Shinjuku Boys kipindi cha mwaka wa 1995 kutoka Kim Longinotto kilielezea habari ya kilabu cha wahudumu katika eneo la Shinjuku ambako waajiri walikuwa wanawake waliovaa kama wanaume.

Tokyo Girls (2000) ni kipindi ambako raia wanne wanawake wa Canada walionyesha uzoefu wao kama wahudumu.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. As Lucie Blackman murder verdict approaches, foreign hostesses remain vulnerable, Japan Today, 13 Aprili 2007
  2. 2.0 2.1 Nightclub hostess world still seen as one where profit trumps visas, safety, Japan Times, 3 Julai 2007
  3. 3.0 3.1 3.2 Tokyo plays host to sexual shift, Guardian, 18 Septemba 2005
  4. Japanese flesh traders targeting Western women, Asian Sex Gazette, 13 Januari 2005
  5. Japanorama, BBC Three, Season 3 Episode 2, first aired 26 Machi 2007
  6. Japan, The International Encyclopedia of Sexuality, 1997-2001
  7. 7.0 7.1 7.2 [19] ^ Akiko Takeyama, Commodified Romance in a Tokyo Host Club
  8. [18] ^ Clubs Where, for a Price, Japanese Men Are Nice to Women The New York Times, 8 Septemba 1996

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]