Viktoriani, Frumenti na wenzao
Viktoriani, Frumenti na wenzao ni Wakristo waliofia imani ya Kanisa Katoliki huko Hadrumetum (leo Susa nchini Tunisia) tarehe 23 Machi 484 kwa agizo la mfalme wa Wavandali Huneriki aliyekuwa Mwario.
Alianza kudhulumu mapadri na watawa mwaka 480, ila kufikia mwaka 484 aliendelea na waumini wa kawaida.
Viktoriani alikuwa tajiri wa Hadrumetum aliyeteuliwa na Huneriki kuwa gavana. Alifanya kazi hiyo vizuri lakini alipodaiwa kukubali Uario, alikataa; hivyo aliteswa na hatimaye kuuawa.
Siku hiyohiyo waliuawa kikatili sana Wakatoliki wengine wanne: wafanyabiashara wawili wa Karthago wenye jina la Frumenti na ndugu wawili wa Aquae Regiae, Byzacena, waliouawa huko Tabaia.
Tangu kale wanaheshimiwa kama watakatifu wafiadini.
Sikukuu yao ya pamoja huadhimishwa tarehe ya kifodini chao[1].
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Saints of March 23: Sts. Victorian, Frumentius, and Companions Archived 13 Juni 2017 at the Wayback Machine.
- [1]
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |