Vikta Mwafrika

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mozaiki katika kanisa lake mjini Milano.

Vikta Mwafrika (kwa Kilatini: Victor Maurus) alikuwa askari Mkristo kutoka Mauretania (katika Algeria ya leo).

Mwaka 303 BK, akiwa Milano (nchini Italia), alibomoa altare kadhaa za dini za jadi za Dola la Roma.

Kwa sababu hiyo aliteswa mbele ya Kaizari Maximian na hatimaye kuuawa pamoja na Waberberi wenzake Nabore na Feliche tarehe 12 Julai huko Lodi Vecchio (Lombardia).

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na wengineo kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 8 Mei.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Christian cross.svg Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Vikta Mwafrika kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.