Vijili wa Salzburg

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu ya Mt. Vijili katika kanisa kuu la Salzburg.

Vijili wa Salzburg (kwa Kilatini Vergilius, kwa Kigaelic Feirgil, 700 hivi - 27 Novemba 784) alikuwa mmonaki na mwanaastronomia kutoka Eire.

Mnamo mwaka 743 alihamia Ufaransa, ambapo alipokewa na mfalme Pipino Mfupi.

Baada ya kuishi miaka miwili huko Cressy, karibu na Compiègne, alikwenda Bavaria, kwa mwaliko wa mtemi Odiloni wa Bavaria, aliyemfanya askofu wa Salzburg (leo nchini Austria) mwaka 748.

Alijitahidi sana kueneza Ukristo kati ya wananchi wa Karinthia.

Alitangazwa mtakatifu na papa Gregori IX mwaka 1233.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake [1].

Mafundisho kuhusu umbo la Dunia[hariri | hariri chanzo]

Vijili alifundisha Dunia kuwa na umbo la tufe na uwezekano wa kuwepo kwa watu kwenye upande wa pili wa Dunia. Alishtakiwa mbele ya Papa wa Roma kuwa fundisho lake halikulingana na maandiko matakatifu. Hata hivyo aliweza kujitetea kwa kudokeza kuwa kama watu wako kwenye upande wa pili wa Dunia ni pia watoto wa Adamu walioathirika sawa na dhambi na ukombozi kama watu wote upande huu uliojulikana.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • M. Tangl, Die Briefe des heiligen Bonifatius und Lullus, Berlin, 1916
  • H. Lõwe, Ein literarischer Widersacher des bonifatius. Virgil von Salzburg und die Kosmographie des Aethicus Hister, in «Abhandlungen der geistes- und sozialwissenschaftlichen Klasse, Akademie der Wissenschaften und der Literatur», Mainz, 11, 1951
  • M. L. W. Laistner, Thought and Letters in Western Europe: A.D. 500 to 900, Ithaca, 1955 ISBN 0-8014-9037-5

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.