Victoria Inyama

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Victoria Inyama ni mwigizaji mkongwe wa Nigeria.

Maisha ya awali na Elimu[hariri | hariri chanzo]

Inyama alizaliwa katika jimbo la Enugu, ambapo ni Kusini Mashariki mwa Nigeria ambayo ilitawaliwa na wazungumzaji wa Igbo wa nchini Nigeria. Alipata shahada ya kwanza kutoka chuo kikuu cha shirikisho kilichoitwa Chuo Kikuu cha Lagos ndani ya Nigeria. Alizungumza na Channels TV kwenye mahojiano ambapo alisema kuwa bado yupo shule anasomea ushauri katika Lewisham Counselling school of London ili aweze kuwa msaada wa watu katika masuala ya kiakili.[1]

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Alianza kazi mnamo mwaka 1990. Katika mahojiano, alisema kuwa msanii mkongwe mwenzake, Alex Usifo ndiye aliyemuona na kumuingiza katika tasnia ya sinema ya Nigeria.[1] Inyama baada ya kuolewa na Godwin Okri, alihamia Uingereza[2] kitendo hiki kilikuwa na madhara katika kazi zake za uigizaji [3] kwa kuwa aliachana biashara za burudani na kujihusisha kwa umakini na familia yake.

Maisha Binafsi[hariri | hariri chanzo]

Inyama aliolewa na Godwin Okri na walipata watoto watatu.[4][5]

Afya[hariri | hariri chanzo]

Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Inyama alidhihirisha pambano lake dhidi ya saratani mnamo mwaka 2006.[6][7][8]

Filamu[hariri | hariri chanzo]

  • Silent Night
  • Danger Zone
  • Odum
  • Love from Above
  • Eze Nwanyi
  • Glamour Boys
  • Iyanga
  • Barraccuda

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 "Nollywood Actors Have A Lot To Learn -Victoria Inyama • Channels Television", Channels Television, 2017-09-15. (en-GB) 
  2. "I’ve no issues with homosexuals – Victoria Inyama, actress | The Sun News". sunnewsonline.com (kwa en-GB). Iliwekwa mnamo 2017-12-01. 
  3. "I don’t see myself relocating to Nigeria ---Victoria Inyama-Okri", Nigeriafilms.com. (en-gb) 
  4. G, Sunny. "WELCOME TO SUNNYGIST: Nollywood Star, Victoria Inyama Recent Looks After Three Kids.". WELCOME TO SUNNYGIST. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-12-02. Iliwekwa mnamo 2017-12-01.  More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
  5. "THE THINGS I DON’T LIKE ABOUT LONDON – Star actress, Victoria Inyama – Yes International! Magazine". theyesng.com. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-12-02. Iliwekwa mnamo 2017-12-01.  More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
  6. "Victoria Inyama's Emotional Story On Her Battle With Cancer | 36NG". www.36ng.ng (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2017-12-01. 
  7. Latestnigeriannews. "Victoria Inyama's Emotional Story On Her Battle With Cancer". Latest Nigerian News. Iliwekwa mnamo 2017-12-01. 
  8. "Actress Victoria Inyama Reveals Her Battle With Cancer - Breeze Reporters". www.breezereporters.com (kwa en-US). Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-01-27. Iliwekwa mnamo 2017-12-01.  More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Victoria Inyama kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.