Nenda kwa yaliyomo

Victoria (mwimbaji wa Ucheki)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Victoria Vera Blyth (alizaliwa kama Ficková, na anajulikana kitaaluma kama Victoria au Victoria Velvet; 13 Novemba 198411 Juni 2024) alikuwa mwimbaji na mfanyabiashara wa Ucheki-Afrika Kusini.[1]

Alikuwa mmoja wa waimbaji mashuhuri zaidi wa R&B katika Jamhuri ya Ucheki. Alijulikana sana kwa wimbo wa Hotel California uliopatikana kwenye albamu yake ya kwanza This Is Me! iliyotolewa mwaka 2006.[2] Pia alijizolea umaarufu kupitia ushirikiano wake na waimbaji kama Dara Rolins na Kristína. Alifanikiwa kutoa albamu mbili za studio wakati wa maisha yake ya muziki.

Mnamo Juni 2024, Victoria aliuawa na mume wake nchini Uturuki, akiwa na umri wa miaka 39.[3][4]

Victoria alizaliwa tarehe 13 Novemba 1983 Cape Town, Afrika Kusini. Baba yake alikuwa raia wa Jamhuri ya Ucheki, na mama yake alikuwa Mnamibia. Yeye na familia yake walirejea katika Jamhuri ya Ucheki mwaka 1998 walipohamia mjini Prague.[5]

Licha ya kuwa Ucheki, lugha yake ya asili ilikuwa Kiingereza kwa kuwa alikulia Afrika Kusini akizungumza Kiingereza na Kiholanzi pekee. Alianza kujifunza Kicheki mara tu baada ya kuanza masomo katika shule inayotumia lugha hiyo kufundishia. [6]

Albamu za studio

[hariri | hariri chanzo]
  • This Is Me! (2006)
  1. "Zpěvačku Victorii, která proslula coverem "Hotel California", zastřelil manžel" (kwa Kicheki).
  2. "Zpěvačku Victorii, která proslula coverem "Hotel California", zastřelil manžel" (kwa Kicheki).
  3. "Zpěvačku Victorii, která proslula coverem "Hotel California", zastřelil manžel" (kwa Kicheki).
  4. lara (2024-06-14). "Zavražděná zpěvačka Victoria (†40): Manželovi podřídila život. Putovala po světě, přála si domov…". Blesk.cz (kwa Kicheki). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2025-01-09. Iliwekwa mnamo 2025-01-09.
  5. "Českom otriasa násilná smrť speváčky Victorie Velvet: Po hádke ju mal v Turecku zavraždiť jej manžel" (in Slovak). 14 June 2024.
  6. "Královna? Zatím jen nadějná princezna" (ya Ucheki). Archived from the original on 2025-01-09. Retrieved 2025-01-09.
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Victoria (mwimbaji wa Ucheki) kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.