Victor Obinna

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Victor Nsofor Obinna
Maelezo binafsi
Jina kamili Victor Nsofor Obinna
Tarehe ya kuzaliwa 25 Machi 1987
Mahala pa kuzaliwa    Jos, Nigeria
Nafasi anayochezea Mshambulizi
Maelezo ya klabu
Klabu ya sasa Malaga CFkatika mpango wa mkopo
Namba 18
Klabu za vijana
Plateau United, Kwara Uinited, Enyimba
Klabu za ukubwani
Miaka Klabu
Internazionale, Chievo
Timu ya taifa
Nigeria

* Magoli alioshinda

Victor Nsofor Obinna (amezaliwa Jos, Nigeria, 25 Machi 1987) ni mchezaji kandanda wa Nigeria ambaye anacheza kama mshambuliaji kwa timu ya Malaga CF, akicheza kwa mpango ya mkopo kutoka timu ya Internazionale.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Obinna katika lugha ya Kiigbo linamaanisha Moyo wa Baba. Yeye alichezea klabu ya Chievo katika ligi ya Italia ya Serie B, huku akicheza kwa kawaida katika klabu hiyo hadi waliposhushwa kutoka ligi yao katika mwaka wa 2007. Yeye alichezea ka mara ya kwanza katika mchezo ya kimataifa kwa timu ya Nigeria katika Shindano la Kombe la Afrika katika mwaka wa 2006,akafunga bao moja katika michuano mitatu.Nigeria walishindwa katika michezo ya nusu fainali.

Wasifu wa klabu[hariri | hariri chanzo]

Enyimba[hariri | hariri chanzo]

Obinna alichezea klabu za Nigeria: Plateau United na Kwara United , kabla ya kupiga saini mkataba na Mabingwa wa Afrika wakati huo,Enyimba katika mwaka wa 2005. Hata hivyo,hakucheza mechi yoyote ya Enyimba ya kushindana. Katika mwaka uo huo, alikwenda kufanya majaribio katika klabu za Kiitaliano ya Internazionale , Perugia na Juventus kabla ya kupiga saini mkataba na klabu ya Brazili ya Internacional lakini shida za kisheria zilifanya mpango huo ufeli. Yeye alirudi Enyimba ili kushiriki katika kampeni yao ya ligi ya Nigeria na ulinzi wa Kombe la Mabingwa la CAF.

Chievo Verona[hariri | hariri chanzo]

Obinna aliajiriwa na klabu ya Kiitaliano Chievo kwenye mkataba wa miaka mitatu mnamo Julai 2005. Katika msimu wake wa kwanza na Chievo, Obinna alifunga mabao sita katika michezo 26, pamoja na bao lake la kwanza katika ligi ya Serie A ya Parma katika ushindi wa 1-0, 11 Septemba 2005. Katika miezi ya kwanza ya msimu wa 2006, Obinna alikatazwa kucheza kwa kosa la kupiga saini mkataba na Internacional na Chievo katika mwaka wa 2005. Chievo walishushwa kutoka ligi hiyo mwishoni mwa msimu wa 2006-07, ikatia shaka kuhusu chenye kitamfanyikia Obinna; hata hivyo, klabu iliamua kuendelea kuwa na Obinna ndani ya kikosi ili kuwasaidia kupanda na kurudi ligi kuu ya Serie A.

Tarehe 4 Oktoba 2007, Obinna alihusika katika ajali ya gari akiwa njiani akirudi nyumbani kutoka mazoezi.Alikuwa anajaribu kulihepa gari ambalo liltaka kumpita kwa kona huku akihepa na majeraha madogomadogo na mshtuko.Gari lenyewe lilibingirika mara kadhaa na likaharibika kabisa. Katika ajali,alipoteza fahamu na akapelekwa hospitali. Ajali hilo lilitokea takriban mita 100 kutoka mahali ambapo mchezaji wa Chievo wa zamani Jason Mayele alikufa katika ajali(2002).

Internazionale[hariri | hariri chanzo]

Obinna akisherehekea alipofunga bao akiwa timu ya Inter

Katika mwezi wa Agosti 2008, Obinna alihamia Internazionale na kutia saini mkataba wa miaka minne. [5] Klabu ya Uingereza ya Everton ilitaka kumwajiri katika mpango wa mkopo lakini hawakuweza kupata kibali cha kumpa kazi kutoka serikali. Bao la kwanza la Obinna akiwa Inter lilikuwa tarehe 19 Oktoba katika ushindi wao wa 4-0 dhidi ya Roma.

Malaga CF[hariri | hariri chanzo]

Tarehe 26 Agosti 2009, timu ya ligi ya Uhispania ya Malaga CF walimwajiri kwa mpango wa mkopo kutoka Internazionale kwa msimu mmoja. Yeye alifunga bao lake la kwanza kwa timu yake mpya katika mechi yao dhidi ya Xerez terehe 4 Oktoba,mechi iliisha 1-1.

Kazi ya Kimataifa[hariri | hariri chanzo]

Obinna aliitwa kwenye timu ya taifa ya Nigeria hapo katika Shindano la Kombe la Afrika akifunga bao moja kabla ya timu yao kutolewa katika mkondo wa nusu fainali.

Agosti 2008, alikuwa miongoni mwa wachezaji katika kikosi cha Nigeria cha Olimpiki ya 2008 iliyo Beijing. Obinna alifunga Nigeria bao la kwanza katika ushindi wao wa 2-1 dhidi ya Ujapani. Nigeria walicheza mechi dhidi ya Ivory Coast,huku Obinna akifunga mkwaju wa penalti na kupanga mchezo mzuri uliomfanya Peter Odemwingie afunge bao. Baadaye alikuwa nahodha katika timu yao iliposhinda Ubelgiji 4-1 katika mechi ya nusu fainali, walishindwa hapo baadaye katika fainali na Argentina.

Mabao ya kimataifa[hariri | hariri chanzo]

# Tarehe Pahali Wapinzani Mabao Tokeo Shindano
1 4 Februari 2006 Port Said, Misri Tunisia Tunisia 1-1 (6-5 pen.) Walishinda Shindano la Kombe la Afrika
2 11 Oktoba 2008 Abuja, Nigeria Sierra Leone Sierra Leone 4-1 Walishinda Mechi ya Kuhitimu Kucheza katika Shindano Kombe la Dunia
3 6 Juni 2009 Abuja, Nigeria Kenya Kenya 3-0 Walishinda Mechi ya Kuhitimu Kucheza katika Shindano Kombe la Dunia
4 6 Juni 2009 Abuja, Nigeria Kenya Kenya 3-0 Walishinda Mechi ya Kuhitimu Kucheza katika Shindano Kombe la Dunia
5 11 Oktoba 2009 Abuja, Nigeria Msumbiji Msumbiji 1-0 Walishinda Mechi ya Kuhitimu Kucheza katika Shindano Kombe la Dunia

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Maana ya jina "Obinna"
  2. "Victor Obinna"
  3. "Chievo wakataa kuwa Obinna ameondoka"
  4. ["Everton wajaribu kumwajiri Obinna"]. BBC Sport Online. 2008-08-28. http://news.bbc.co.uk/sport1/hi/football/africa/7586221.stm.
  5. McLeod, Scott (2008-09-01). "Obinna??". [www.evertonfc.com. http://evertonfc.com/news/archive/obinna-deal-falls-through.htmlArchived 26 Aprili 2012 at the Wayback Machine.. Obinna??]
  6. "Obinna pasó reconocimiento médico en el Complejo Sanitario Málaga C. F.". [www.malagacf.com. http://www.malagacf.com/noticias/obinna-paso-reconocimiento-medico-1491.html Archived 26 Septemba 2009 at the Wayback Machine. Obinna na Malaga.]
  7. [1] Archived 18 Agosti 2009 at the Wayback Machine.
  8. www.ussoccer.com. Niigeria Olimpiki. Archived 3 Desemba 2008 at the Wayback Machine.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]