Veronika Giuliani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Veronika Giuliani alivyochorwa akiwa na alama zake maalumu.

Veronika Giuliani alizaliwa Mercatello sul Metauro (Marche, Italia tarehe 27 Desemba 1660 akafariki Città di Castello (Umbria, Italia) tarehe 9 Julai 1727.

Alikuwa mmonaki wa urekebisho wa Wakapuchini wa Utawa wa Mt. Klara.

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu bikira.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Orsola Giuliani anasimulia alivyoanza kujaliwa karama za pekee akiwa na umri wa miaka 3 tu.

Alijiunga na Waklara Wakapuchini wa monasteri ya Città di Castello mwaka 1667 ambapo akawa abesi tangu mwaka 1716 hadi kifo chake.

Kwa namna ya pekee aliambatana na Yesu msulubiwa kadiri ya karama ya Fransisko wa Asizi.

Maandishi[hariri | hariri chanzo]

Kwa agizo la padri aliyemuongoza kiroho, aliandika kirefu (kurasa 22,000 kwa mikono bila ya sahihisho lolote) kumbukumbu za maisha yake yote, ambazo zilitolewa baada ya kifo chake kwa jina Il Tesoro Nascosto (ni magombo 36).

Kutokana na shajara hiyo, Veronika Giuliani anahesabiwa kati ya Wakristo wanasala waliojaliwa mang'amuzi ya juu zaidi.

Heshima baada ya kufa[hariri | hariri chanzo]

Ingawa aliheshimiwa mara baada ya kufa, kesi ya kumtangaza mtakatifu ilicheleweshwa na uchunguzi wa maandishi yake marefu.

Papa Pius VII alimtangaza mwenye heri mnamo Juni 1804, halafu Papa Gregori XVI alimtangaza mtakatifu tarehe 26 Mei 1839.

Kanisa Katoliki linakubali ukweli wa madonda matakatifu aliyokuwanayo tangu tarehe 5 Aprili 1697 hadi kifo chake.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]