Verdiana Masanja

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Verdiana Grace Masanja (alizaliwa 12 Oktoba 1954 mjini Bukoba nchini Tanzania), ni mwanahisabati aliyekuwa mwanamke wa kwanza Mtanzania kupata shahada ya uzamivu katika hisabati.

Tangu mwaka 2018 ni profesa wa hisabati kwenye Taasisi ya Kiafrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela huko Arusha, Tanzania.

Masanja alizaliwa mjini Bukoba katika familia ya Kashaga[1].

Elimu yake[hariri | hariri chanzo]

Alipata elimu yake ya sekondari Jangwani High School mjini Dar es Salaam, akaendelea kusoma hisabati na fizikia kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hadi alipopata shahada ya uzamili mnamo mwaka 1981.

Baada ya hapo, aliendelea na masomo katika Chuo Kikuu cha Ufundi Berlin, Ujerumani, ambapo alipokea shahada ya uzamivu mnamo mwaka wa 1986 na kuandika tasnifu juu ya A numerical study of a Reiner-Rivlin Fluid in an axi-symmetrical circular pipe.[2]

Baada ya kurudi Tanzania alikuwa profesa wa hisabati katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuongoza idara ya hisabati tangu mwaka 1994 hadi 2000.[3] Tangu mwaka 2006 alifundisha nchini Rwanda alipokuwa profesa wa Chuo Kikuu cha Rwanda akisimamia pia masomo ya juu, akaendalea kuwa mshauri kwenye Chuo Kikuu cha Kibungo[4].

Masanja alijishughulisha katika kuhakikisha anawawezesha katika elimu ya hisabati na sayansi wasichana na wanawake nchini Tanzania na katika Afrika kwa jumla.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. African Doctorates in Mathematics: A Catalogue, uk. 718, iliangaliwa kupitia google books tar. 1. Desemba 2018
  2. Verdiana Grace Masanja kwenye tovuti ya Mathematics Genealogy Project ya North Dakota State University, Marekani, iliangaliwa Desemba 2018
  3. L.H. Riddle, makala "Verdiana Grace Masanja" katika Biographies of Women Mathematicians, kwenye tovuti ya Agnes Scott College, Memphis, Marekani
  4. Ms Verdiana Grace Masanja, tovuti ya net4mobility.eu ya mradi wa Horizon 2020 ya Umoja wa Ulaya

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]