Verckys Kiamuangana Mateta

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Verckys Kiamuangana Mateta (Kinshasa, Zaire, 19 Mei 1944 - 13 Oktoba 2022) alikuwa mwanamuziki (hasa mpiga saksafoni), mtunzi, kiongozi wa bendi, mtayarishaji wa rekodi, na kiongozi wa biashara ya muziki katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).[1]

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa kama Georges Kiamuangana. Alitoka katika familia tajiri; baba yake alikuwa mfanyabiashara huko Leopoldville (sasa ni Kinshasa). Alijifunza muziki kanisani. Kama mpiga saksafoni, alichukua jina la Verckys kulingana na mpiga saksafoni wa Kimarekani King Curtis, akisikia jina "Curtis" kama "Verckys."[1]

Alikuwa kwenye kikundi cha bendi ya soukous TPOS jazz,Iliyo ongozwa na François Luambo Makiadi, ambaye alitawala tasnia ya muziki wa Kong miaka ya 1950 hadi 1980.[2]

Mnamo 1969, Verckys Kiamuangana alihama TPOK Jazz na kuanzisha bendi yake, Orchester Vévé.

Verkys pia alisimamia bendi nyingine mbili, alizokuwa akizimiliki: Orchester Kiam na Orchester Lipua Lipua. Miongoni mwa wanamuziki waliowahi kuichezea Verkys miaka ya 1970 ni Nyboma Mwandido na Pepe Kalle. Katika miaka ya mapema ya 1980 Verckys aliacha uchezaji wa muziki, ili kufuata mambo mengine.[3]

Mnamo 2015, Sterns Music ilitolewa katika muundo wa MP3 sehemu kubwa ya lebo ya rekodi ya Verckys's Éditions Vévé (chapisho la blogu linalotangaza hili linajumuisha wasifu wa Verckys).

Marejeo[hariri | hariri chanzo]