Velocity (gazeti)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Velocity
Toleo la kwanza la Velocity 3 Desemba 2003.
Jina la gazeti Velocity
Aina ya gazeti *. Gazeti la kila wiki
*. Gazeti la bure
Lilianzishwa 3 Desemba 2003
Eneo la kuchapishwa *. Kentucky
*. Indiana Kusini
Nchi Marekani Marekani
Mmiliki Kampuni ya Gannett
Makao Makuu ya kampuni Louisville, Kentucky.
Tovuti Tovuti rasmi ya Velocity Weekly

Historia[hariri | hariri chanzo]

Velocity ni gazeti la bure la kuchapishwa kila wiki. Lilichapishwa kwa mara ya kwanza mnamo tarehe 3 Desemba 2003 na jarida la The Courier Journal ya Louisville, Kentucky.

Gazeti hili huchapishwa katika rangi zote na sio nyeusi na nyeupe tu. Linasambazwa katika maeneo 1,800 katika makata 13 ya Kentucky na Indiana Kusini

Velocity linaonekana na wengi kuwa jaribio la gazeti la Courier Journal na kampuni yake ya uzazi ya Gannett la kupata kipande cha soko liliodhibitiwa na gazeti la Louisville Eccentric Observer. Gazeti la Louisville Eccentric Observer ni gazeti badala linalochapishwa kila wiki huko Louisville.

Velocity hulenga watu wa umri wa miaka 25 hadi umri wa miaka 34 kama wasomaji wa gazeti lao. Gazeti hilo lina uangalifu mkali ili lisihusike katika siasa ingawa limechapisha makala kuhusu masuala kadhaa ya ubishi kama yale ya Vita ya Iraq na upigaji marufuku wa uvutaji sigara katika maeneo ya umma katika Louisville.

Makala ya kila wiki ni kama The Bar Hopper, baa ya mtaa inachunguzwa na maoni kutolewa kuihusu; Rock This Town, makala yanayozungumza kuhusu bendi au mwanamuziki wa mtaa huo; The Party Crasher, hadithi ya ki-picha ya matamasha yaliyofanyika huko; na All I'm Saying Is, makala yaliyoandikwa na msomaji. Gazeti hili linajumuisha sehemu ya filamu inayoitwa The Big Screen inayoangazia filamu zinazoonyeshwa kwenye sinema za mitaa. Maoni kuhusu filamu hizo huandikwa katika aya moja kwa njia inayochekesha.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]