Valbenazini
| Jina la (IUPAC) | |
|---|---|
| (2R,3R,11bR)-3-Isobutyl-9,10-dimethoxy-1,3,4,6,7,11b-hexahydro-2H-pyrido[2,1-a]isoquinolin-2-yl L-valinate | |
| Data ya kikliniki | |
| Majina ya kibiashara | Ingrezza |
| AHFS/Drugs.com | Monograph |
| Kategoria ya ujauzito | ? |
| Hali ya kisheria | ℞-only (US) |
| Njia mbalimbali za matumizi | Kwa mdomo |
| Data ya utendakazi | |
| Kufunga kwa protini | >99% |
| Kimetaboliki | Uanzishaji huwa kwa hidrolisisi, kuzima huwa kwa CYP3A, CYP2D6 |
| Nusu uhai | Masaa 15–22 |
| Utoaji wa uchafu | 60% mkojo, 30% kinyesi |
| Vitambulisho | |
| Nambari ya ATC | ? |
| Visawe | NBI-98854 |
| Data ya kikemikali | |
| Fomyula | C24H38N2O4 |
| |
Valbenazini, inayouzwa chini ya jina la kibiashara Ingrezza, ni dawa inayotumika kutibu matatizo ya misuli yanayochelewa kutokea kutokana na matumizi ya dawa (tardive dyskinesia), ugonjwa wa mwendo wa muda mrefu unaosababishwa na dawa za kupunguza maumivu ya akili.[1] Dawa hii inamezwa kwa mdomo.[1] Matumizi yake ya muda mrefu yanahitajika.[1]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kinywa kikavu, usingizi, uhifadhi wa mkojo, kizunguzungu, na maumivu ya kichwa.[1] Madhara yake mengine ni pamoja na kurefuka kwa muda wa mapigo ya moyo (QT).[2] Matumizi yake hayapendekezwi kwa wale walio na matatizo makubwa ya figo.[1] Dawa hii ni kizuizi cha protini ya usafirishaji wa monoamini kwenye vifuko vya seli (VMAT2).[1]
Valbenazini iliidhinishwa kwa matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2017.[1] Kufikia mwaka wa 2018, iligharimu dola za Marekani 5,750 hadi 6,225 kwa mwezi.[2] Dawa hii inapatikana tu katika maduka fulani ya dawa.[3] Kwa sasa hakuna mipango ya kuiuza barani Ulaya kufikia mwaka wa 2018.[4]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- 1 2 3 4 5 6 7 "Valbenazine Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 24 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 4 Agosti 2021.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - 1 2 Uhlyar, S; Rey, JA (Juni 2018). "Valbenazine (Ingrezza): The First FDA-Approved Treatment for Tardive Dyskinesia". P & T : a peer-reviewed journal for formulary management. 43 (6): 328–331. PMID 29896031.
{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Ingrezza Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 21 Aprili 2019. Iliwekwa mnamo 5 Agosti 2021.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Valbenazine". SPS - Specialist Pharmacy Service. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 27 Agosti 2021. Iliwekwa mnamo 6 Agosti 2021.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)