Nenda kwa yaliyomo

Uzia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mfalme Uzia alivyochorwa na Guillaume Rouillé mwaka 1553.

Uzia (kwa Kiebrania: עֻזִּיָּהוּ, ‘Uzzīyyāhū, "Nguvu yangu ni YHWH";[1] kwa Kigiriki: Ὀζίας, kwa Kilatini: Ozias; anajulikana pia kama Azaria, עֲזַרְיָה, ‘Azaryā; Αζαρίας; Azarias[1][2]; alifariki 742 KK hivi) alitawala ufalme wa Yuda kwa miaka 52, kwanza pamoja na baba yake[3], Amazia, halafu peke yake, hatimaye pamoja na mwanae Yothamu.

Chini yake ufalme ulistawi sana.

Habari zake zinapatikana hasa katika Kitabu cha Pili cha Wafalme 15 na Kitabu cha Pili cha Mambo ya Nyakati 26, lakini anatajwa pia katika kitabu cha nabii Isaya na kile cha nabii Amosi.

Pia anatajwa na Injili ya Mathayo kati ya mababu wa Yesu Kristo.

  1. 1 2 "Ozias". Catholic Encyclopedia. 1917.
  2. Alexander Mackie Honeyman, "The Evidence For Regnal Names Among The Hebrews" in Journal of Biblical Literature, Vol. 67, No. 1, (Mar., 1948), pp.13-25.
  3. "Uzziah", Jewish Encyclopedia
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Uzia kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.