Uzalishaji wa mbwa

Uzalishaji wa mbwa (pia: mbwa wanaozalishwa) ni aina maalumu ya mbwa ambao hufugwa makusudi na binadamu kwa minajili ya kutekeleza majukumu fulani, kama vile kuchunga, kuwinda, na kulinda. Mbwa ni mamalia wenye mabadiliko makubwa zaidi duniani. Kumekuwa na uzalishaji mnemba wa mbwa aina hii zaidi 360 zinazotambulika kimataifa.[1] Aina hizi zina sifa maalum za kimofolojia, ikijumuisha ukubwa wa mwili, maumbo, sifa za kifeno[2] mkiani, na aina ya manyoya. Ingawa zina tofauti nyingi, zote bado ni spishi moja ya mbwa. Tabia zao za kimaumbile ni pamoja na ulinzi, uchungaji, uwindaji, na pia sifa za kirafiki, uthubutu, na uchokozi. Aina nyingi zilitokana na kundi dogo la wazazi waanzilishi katika kipindi cha miaka 200 iliyopita. Kutokana na uwezo wao wa kubadilika kwa mazingira tofauti na kufugwa kulingana na mahitaji ya binadamu, leo mbwa ni spishi inayopatikana kwa wingi zaidi ya wanyama wala nyama na wamesambaa ulimwenguni.
Mbwa hawa huzalisha uthabiti wa sifa za kimwili, mienendo, na tabia ambazo zilianzishwa kwa miongo ya uzalishaji kwa uchaguzi maalum. Kwa kila aina inayotambuliwa, klabu za mbwa na rejesta za aina kwa kawaida huchapisha kiwango cha aina ambacho kina maelezo yaliyoandikwa kwa mfano ulio bora wa aina hizo za mbwa.[3][4][5] Matumizi mengine ya neno aina linapohusiana na mbwa ni pamoja na aina safi ya mbwa, mchanganyiko, aina mchanganyiko na aina za asili.[6]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Parker, Heidi G.; Dreger, Dayna L.; Rimbault, Maud; Davis, Brian W.; Mullen, Alexandra B.; Carpintero-Ramirez, Gretchen; Ostrander, Elaine A. (2017). "Genomic Analyses Reveal the Influence of Geographic Origin, Migration, and Hybridization on Modern Dog Breed Development". Cell Reports. 19 (4): 697–708. doi:10.1016/j.celrep.2017.03.079. PMC 5492993. PMID 28445722.
- ↑ Katika biolojia, phenotype inamaanisha seti ya sifa zinazoonekana za kiumbe, ambazo hutokana na mwingiliano kati ya genotype (maumbile ya kijeni) na mazingira. Hii inaweza kujumuisha muonekano wa nje, tabia, na hata sifa za kisaikolojia. Kwa mfano, rangi ya macho, urefu, na tabia za kimaumbile za mbwa ni sehemu ya phenotype yake.
- ↑ "Dog Breeds - Types Of Dogs". American Kennel Club. 2017-11-12. Iliwekwa mnamo 2019-08-08.
- ↑ Irion, D (2003). "Analysis of Genetic Variation in 28 Dog Breed Populations With 100 Microsatellite Markers". Journal of Heredity. 94 (1): 81–7. doi:10.1093/jhered/esg004. PMID 12692167.
- ↑ "About Breed Standards". Home. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-07-23. Iliwekwa mnamo 2019-08-09.
- ↑ "Dog Breed Profiles". Dog Breed Profiles (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2020-02-29.