Uweza Foundation
Uweza Foundation ni shirika lisilo la kiserikali ambalo linafanya kazi ya kukuza maendeleo ya binadamu katika mtaa wa mabanda wa Kibera jijini Nairobi, Kenya. Lilianzishwa mwaka wa 2008 na limesajiliwa nchini Marekani kama shirika la 501(c)3.[1]Linaongozwa na mwigizaji Rooney Mara[2]
Uweza limepewa jina kutokana na neno la Kiswahili ambalo linamaanisha fursa, uwezo na uwezeshaji.[3]
Historia
[hariri | hariri chanzo]Uweza Foundation ilianzishwa mwaka wa 2008.[4] Mwanzilishi wake alikuwa amehamia nchini na kuolewa na mwanamume wa huko baada ya kutembelea Kenya kwa ajili ya kujitolea katika makao ya watoto katika kituo cha watoto kilichoko katika mtaa wa mabanda wa Kibera.[4]
Mnamo Januari 2011, Uweza Foundation ilishirikiana na Faces of Kibera, shirika la hisani lililoanzishwa na Rooney Mara.[3]Faces of Kibera ililenga kutoa makazi, chakula, na huduma za matibabu kwa mayatima kwa kujenga kituo cha watoto yatima katika eneo hilo.[5] Shirika hilo lilipata msaada wa michango kutoka kwa timu za NFL chini ya uongozi wa Mara.[6]Mara alikuwa ameanza shirika hilo baada ya kutembelea eneo hilo kama mfanyikazi wa kujitolea mwaka wa 2006,ambapo aliguswa na hali ya mayatima,wengi waliokuwa wamepoteza wazazi kutokana na UKIMWI na magonjwa yanayohusiana na VVU.Alianzisha shirika lake kutokana na kuchoshwa na ongezeko la mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo alihisi kwamba yalikuwa yanatafuta faida za biashara tu: "The people who need help aren't really getting it.So I started my own " aliambia jarida la Interview mwaka wa 2009.[7]Uweza Foundation inaendelea kusimamiwa na Mara ambaye anahudumu kama rais wa bodi ya wakurugenzi wa shirika hilo.[2][5][8]
Mnamo 2022, Uweza Foundation ilishirikiana na ROAM Gallery na Xtina Parks kuonyesha kazi za wasanii wa Kibera katika Jumba la Museum of Contemporary Art huko Massachusetts.[9]
Maeneo ya kuzingatia
[hariri | hariri chanzo]Shirika hilo linafanya kazi kuwawezesha wakazi wa Kibera, hasa wanawake na vijana, kupitia programu za elimu zinazolenga kusaidia kukuza vipaji vya wasanii wachanga na kuwasaidia wasanii kujikimu kimaisha kupitia masoko ya kazi zao za sanaa.[4][10]Shirika hilo pia limejikita katika kuwawezesha wanawake na wasichana kwa kushughulikia changamoto zinazowakabili wasichana balehe katika eneo la Kibera.[11]Pia lina eneo maalum linalowawezesha wanafunzi ambao hawana umeme majumbani mwao kusoma nje ya shule na kufadhili timu ya soka ya vijana.[12][13]
Uweza Gallery
[hariri | hariri chanzo]Kama mojawapo ya shughuli zake,shirika hilo lilianzisha Uwezo Gallery katika eneo la Olympic Estate, Kibera mwaka wa 2012.[14]Jumba hilo la sanaa linaonyesha kazi za wasanii wa eneo hilo na pia linakuza vipaji vipya vinavyochipukia.Limewawezesha wasanii wachanga kufadhili elimu yao kupitia sanaa.[15]Awali,jumba hilo lilikuwa katika kontena la mizigo la zamani, lakini lilihamishwa mwezi Januari mwaka wa 2019.[14][16][17][18]
Janga kubwa la virusi vya korona
[hariri | hariri chanzo]Wakati wa janga la virusi vya korona, Uweza ilishirikiana na washirika kutoka sekta binafsi kuanzisha mpango wa kukuza usafi wa mazingira katika makazi yasiyo rasmi kama vile Kibera na kutoa barakoa za kisanii bila malipo kwa wakazi iliyoundwa na msanii wa eneo hilo.[19][20]Shirika hilo pia lilishirikiana na wasanii kutoka Uweza Gallery kuunda michoro ya ukutani yenye ujumbe wa kuelimisha jamii kuhusu tahadhari na uelewa wakati wa janga hilo.[21][22]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Financials". Uweza Foundation (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2025-10-16.
- 1 2 Julie Ma (2013-05-31). "Rooney Mara and Mom, Hair Twins". The Cut (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-10-16.
- 1 2 "Rooney Mara on reinventing Lisbeth Salander for Hollywood". The Herald (kwa Kiingereza). 2011-12-17. Iliwekwa mnamo 2025-10-16.
- 1 2 3 Stefano Esposito (2023-01-06). "In Nairobi, Naperville native Jennifer Sapitro helps Kenyans fulfill their artistic dreams". Chicago Sun-Times (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2025-10-16.
- 1 2 "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-09-07. Iliwekwa mnamo 2025-10-16.
- ↑ "Steelers, Giants memorabilia auctioned to help Kenyan orphans". www.post-gazette.com. Iliwekwa mnamo 2025-10-16.
- ↑ Michael Martin (2009-04-24). "Rooney Mara". Interview Magazine (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2025-10-16.
- ↑ "Rooney Mara - Voguepedia". www.vogue.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-11-07. Iliwekwa mnamo 2025-10-16.
- ↑ The Berkshire Eagle (2022-05-26). "5 gallery shows to see in the Berkshires over Memorial Day weekend". The Berkshire Eagle (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-10-16.
- ↑ Joy Rutou. "Young artists turn passion into income". The Standard (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-10-16.
- ↑ "Kenya Election Results: Empowering Kenyan Girls is the Next Step For a Peaceful Kenya". Mic (kwa Kiingereza). 2013-04-10. Iliwekwa mnamo 2025-10-16.
- ↑ JUDIE KABERIA (2015-09-15). "Kibera pupils jam study centre as teachers' strike bites". Capital News (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2025-10-16.
- ↑ Standard Group PLC. "Uweza Soccer Academy are the winners of the thirteenth edition of the Annual Ramadhan Cup". The Standard (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-10-16.
- 1 2 "Finding a ten-year-old art gallery in Kibera". Business Daily (kwa Kiingereza). 2022-06-20. Iliwekwa mnamo 2025-10-16.
- ↑ Uzalendo News (2019-09-03), Uweza Art Gallery - Positive Community Impact by Kibera Youth - HUSTLE, iliwekwa mnamo 2025-10-16
- ↑ ""The Cure Is Us": Kibera artists take on the pandemic". www.gavi.org (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-10-16.
- ↑ "I am out to create a new image of Kibera, using paint and brush". Daily Nation (kwa Kiingereza). 2022-04-14. Iliwekwa mnamo 2025-10-16.
- ↑ "Instagram". www.instagram.com. Iliwekwa mnamo 2025-10-16.
- ↑ "Strive Masiyiwa, Dangote Group, Safaricom… Africa's private sector leads the fight against Covid". The Africa Report.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-10-16.
- ↑ Alicia Lee (2020-05-10). "In 2020, masks aren't just for protection – they're being used to make a statement". CNN (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-10-16.
- ↑ Agencies and compiled by Devadasan K. P, Picture Editor (2020-08-06). "Mural art: Coronavirus pandemic inspires global graffiti artists". Gulf News: Latest UAE news, Dubai news, Business, travel news, Dubai Gold rate, prayer time, cinema (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-10-16.
{{cite web}}:|author=has generic name (help) - ↑ Ama Nunoo (2020-03-30). "Artists in Kenya's Kibera slum are kicking out coronavirus with these eye-popping murals". Face2Face Africa (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-10-16.