Nenda kwa yaliyomo

Uwekezaji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Baa ya Uwasilishaji Bora, kiwango cha biashara katika masoko makubwa ya dhahabu ya kimataifa.
Ukubwa wa kipande cha dhahabu cha gramu 100 - kilichofungwa ndani ya jaribio la uthibitisho wa uhalisi - ikilinganishwa na kadi ya kuchezea karata.

Uwekezaji humaanisha "kuweka rasilimali katika kitu kinachotarajiwa kupata thamani baada ya muda". [1] Ikiwa uwekezaji unahusisha pesa, basi unaweza kufafanuliwa kama "kutenga pesa katika kitega uchumi fulani ili uweze kuvuna pesa zaidi baadaye".

Madhumuni ya uwekezaji ni kutoa faida kwenye mali iliyowekezwa. Faida inaweza kujumuisha ongezeko la mtaji (faida) au hasara endapo uwekezaji utauzwa. Inaweza pia kujumuisha mapato ya mara kwa mara kama vile gawio, riba, au mapato yatokanayo na kukodisha rasilimali. Faida pia inaweza kuongezeka au kupungua kutokana na mabadiliko katika viwango vya ubadilishaji wa fedha za kigeni.

Wawekezaji hutarajia faida kubwa kutoka kwa uwekezaji wenye hatari zaidi . Wakati uwekezaji wenye hatari ndogo unapofanywa, faida pia kwa ujumla huwa ndogo. Vile vile, hatari kubwa huja na nafasi ya hasara kubwa. Wawekezaji, hasa wanaoanza, mara nyingi wanashauriwa kutowekeza fedha zote sehemu moja. Kutoweka mayai yote katika kapu moja inasaidia sana kupunguza hatari ya hasara kubwa.

Aina za uwekezaji wa kifedha

[hariri | hariri chanzo]

Katika uchumi wa kisasa, uwekezaji unajumuisha:

  • Hisa - Umiliki wa biashara, katika makampuni yanayouzwa hadharani mtu yeyote anaweza kununua
  • Dhamana - wananchi kuikopesha serikali yao, hufanyika katika masoko ya mnada wa umma.
  • Pesa taslimu - kushikilia sarafu fulani, ili kuja kuibadilisha baadae itakapo itakapo panda thamani. (kiwango cha ubadilishaji wa sarafu)
  • Mali isiyohamishika, Majengo ambayo yanaweza kukodishwa ili kutoa mapato yanayoendelea au kuuzwa tena ikiwa thamani itaongezeka.
  • Dhahabu, platinamu na fedha, ni maarufu sana miongoni mwa vito vya thamani katika uwekezaji. Kwa ujumla wawekezaji hununua dhahabu kwa ajili ya kuwekeza. Soko la dhahabu linakabiliwa na mabadiliko ya bei mara kwa mara kama ilivyo kwa masoko mengine.
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Uwekezaji kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  1. True Tamplin. "Investments". Finance Strategists (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2025-05-01.