Uwanja wa michezo wa Thohoyandou

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Uwanja wa michezo wa Thohoyandou ni uwanja wa michezo wenye matumizi mengi katika mji wa Thohoyandou katika maeneo ya Limpopo huko Africa Kusini. Mara nyingi umekuwa ukitumika kwa michezo ya mechi za mpira wa miguu (soka), na ni uwanja wa nyumbani wa timu ya mpira wa miguu ijulikanayo kwa jina la Chui weusi (Black Leopards). Uwanja huo una uwezo wa kuchukua idadi ya watu wapatao elfu ishirini (20,000). Uwanja huo pia unatumiwa na Timu ya zamani ya Limpopian iliyokuwa ikijulikana kama Tshakhuma Tsha Madzivhandila (TTM) kabla ya kuuzwa kwa Mfanyabiashara wa huko Gauteng ambapo alihamia mechi za uwanja wa nyumbani mpaka uwanja wa Peter Mokaba. Uwanja huo unapatikana nyuma ya maduka ya Thavhani na ni rahisi kupatikana. [1]

Haukutumika kwa takriban muda wa miaka minane (8) wakati timu ya Chui weusi(Black Leopards) ilianza kuutumia tena kama uwanja wao wa nyumbani. Musiiwa Eric Manyelenyele ndiye aliyekuw msimamizi wa uwanja huo

Kigezo:Rejea

  1. Data. Jalada kutoka ya awali juu ya 2014-07-14. Iliwekwa mnamo 2021-06-07.