Uwanja wa michezo wa Royal Bafokeng

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uwanja wa Royal Bafokeng , Phokeng

Uwanja wa michezo wa Royal Bafokeng ni uwanja wa michezo unaotumiwa na chama cha mpira wa miguu, Mchezo wa rugby pamoja na wanariadha na kinapatikana huko Phokeng karibu na mji wa Rustenburg,nchini Afrika Kusini. Ulijengwa na unasimamiwa na Royal Bafokeng Nation.[1] Unatumika kama uwanja wa nyumbani kwa ligi kuu ya soka na klabu inayojulikana kama Platinum Stars.Timu ya Leopards ya raga( rugby) iliandaa mechi kubwa zenye mahudhurio makubwa wakati wa Kombe la Currie kwenye uwanja huo, badala ya uwanja wao wa kawaida wa nyumbani, Olën Park.

Uwezo wa uwanja uliongezwa kutoka mashabiki 38,000 hadi 42,000 na kuweza kuandaa mechi tano za raundi ya kwanza na mechi moja ya raundi ya pili kwenye Kombe la Dunia la FIFA mwaka 2010.[2] Uboreshaji wa uwanja huo ulikamilishwa mnamo Machi 2009 na kuandaa mechi 4 za Kombe la Shirikisho la FIFA mwaka 2009.[3]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Uwanja wa michezo wa Royal Bafokeng kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  1. "Sports Palace | Royal Bafokeng Nation". Bafokeng.com. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-05-13. Iliwekwa mnamo 18 May 2010.  More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); Check date values in: |accessdate= (help)
  2. "Royal Bafokeng Stadium: 2010 Venue – Sportslens". soccerlens.com. 4 December 2009. Iliwekwa mnamo 19 April 2018.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  3. FIFA.com. "FIFA Confederations Cup Russia 2017 - Destination - FIFA". FIFA. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-04-19. Iliwekwa mnamo 19 April 2018.  Unknown parameter |= ignored (help); Unknown parameter |https://web.archive.org/web/20180419183405/https://www.fifa.com/confederationscup/destination/stadiums/stadium= ignored (help); More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); Check date values in: |accessdate= (help)