Uwanja wa michezo wa Randi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Uwanja wa michezo wa Randi ni uwanja uliopo Rosettenville katika kitongoji cha Johannesburg huko Afrika Kusini. Uliwekwa kama uwanja wa mazoezi kwa timu zilizoshiriki kombe la dunia(FIFA) la mwaka 2010 baada ya kujengwa tena na kufunguliwa Agusti mwaka 2008. Licha ya udogo wake, inachukuliwa pia kama sehemu bora ya kuchezea nchini huko.[1]

Historia Yake[hariri | hariri chanzo]

Uwanja wa michezo wa Randi umetengenezwa kati ya mwaka 1949 na 1951 kwa jumla ya gharama za Euro 60,000 ukiwa na uwezo wa kuchukua watu elfu kumi na tano(15,000).[2] Kwa muda mrefu ukarabati uliendelea kufanyika , wa kwanza mi ule wa kati ya mwaka 1964 na 1965 ambapo vifaa viliongezwa na ule wa pili mnamo mwaka 1976 ambapo ulijumuisha uwekaji wa taa. Uwanja huo ulionekana kuhitaji maboresho zaidi na ikapitishwa kwamba utabomolewa mwaka 2006.[3]

Hapo mwanzo uwanja wa Randi ulikuwa na uwezo wa kuchukua idadi ya mashabiki 15,000 lakini mwaka 2009 katika maandalizi ya kombe la dunia mnamo mwaka 2010 maboresho yaliongezeka hadi kufikia uwezo wa kuchukua idadi ya washabiki elfu thelathini(30,000).

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Bafana face Angola at Rand Stadium", [[SuperSport (South African TV channel)|SuperSport]], 9 October 2015. 
  2. "Archived copy". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-06-26. Iliwekwa mnamo 2008-06-30.  Unknown parameter |url-status= ignored (help)
  3. "Archived copy". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-03-15. Iliwekwa mnamo 2010-03-29.  Unknown parameter |url-status= ignored (help)
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Uwanja wa michezo wa Randi kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.