Uwanja wa michezo wa Mokhtar El Tetsh
Uwanja wa michezo wa El-Tetsh(Kiarabu ستاد مختار التتش), mara nyingi hujulikana kama ni moja ya sehemu ya Al Ahly SC ambapo unawakilisha klabu huko Misri na kimataifa. Ingawa mchezo wa mpira wa miguu haukuwa moja ya malengo ya waanzilishi wa klabu cha Al Ahly lengo la kilabu lilikuwa kufungua milango yake kwa wanafunzi wa shule za juu kukutana na kufanya mazungumzo ya kisiasa, lakini wahitimu wa shule za upili wanachama wa kilabu wanapendana na chama cha mpira wa miguu , ambapo ilimchochea Ahly kujenga uwanja wa kwanza mnamo mwaka 1909 na walikuwa wakiuita Al-Hawsh, ambalo ni neno la kawaida kutoka kwa lahaja ya Misri linamaanisha ua kwa Kiarabu . Uwanja huo ulitengenezwa zaidi ya miaka kuwa Uwanja wa Mokhtar El-Tetsh. Hivi sasa uwanja unashikilia mazoezi ya timu na michezo ya kirafiki.
Historia
[hariri | hariri chanzo]- Mnamo mwaka 1917 Al Ahly aliamua kujenga uwanja wake wa timu.
- Mnamo mwaka 1927 Al Ahly ongeza stendi ya magharibi kwa gharama ya pauni 2500 ya Misri
- Uwanja huo ulipewa jina la nyota maarufu wa Wamisri | Wamisri Mahmoud Mokhtar El-Tetsh. Hivi sasa unatumika kama uwanja wa mazoezi wa Al-Ahly na pia kwa michezo ya kirafiki.
Uwanja huo ulibuniwa zaidi ya miaka ili kujulikana kama Uwanja wa Mokhtar El-Tetsh. Mnamo mwaka 1929, uwanja huo ulipewa jina la mkuu wa Misri wakati huu, Uwanja wa Prince Farouk. Kufikia mwak 1956, standi nyepesi ziliongezwa kwenye uwanja. Baadae uwanja huo uliitwa Mokhtar El Tetsh.[1]
Majina ya Uwanja
[hariri | hariri chanzo]- Mara ya kwanza Al Ahly kujenga uwanja huo jina lake liliitwa "Uwanja wa Al Ahly"
- Mnamo mwaka 1928 baada ya ufalme kudhaminiwa Al Ahly wakati wa King Foaud, Al Ahly alibadilisha jina la uwanja wake kuwa "'Uwanja wa Prince Farouk"
- Mnamo tarehe 21 Februari mwaka 1965 baada ya kifo cha Mahmoud Mokhtar El-Tetsh, Al Ahly iliamua kuitaja uwanja huo kwa jina la Mokhtar El-Tetch na bado ulianzishwa hadi sasa
- "" Hitimisho la Majina ""
Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 1959
[hariri | hariri chanzo]Uwanja huo ulikuwa mahali pekee kwa ajili ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 1959
Hatua za Kurekebisha Uwanja wa michezo wa Mokhtar El-Tetch
[hariri | hariri chanzo]- Mnamo mwaka 2009 Mwenyekiti wa Al Ahly Hassan Hamdy aliamua kusimasisha stendi ya magharibi baada ya kuibomoa na kuzinduliwa tena katika sura yake mpya mnamo mwaka 2010
- Mnamo mwaka 2016 Mwenyekiti wa Al Ahly Mahmoud Taher kwa kushirikiana na Kampuni ya Sela Sport, wanasimamisha tena stendi ya magharibi na kuongeza rangi ya timu kwenye stendi
Viungo vya njee
[hariri | hariri chanzo]- http://www.worldstadiums.com/stadium_pictures/middle_east/egypt/cairo_ahly.shtmlArchived 10 Februari 2012 at the Wayback Machine. Mokhtar El-Tetsh Stadium
- http://stadiumdb.com/stadiums/egy/mukhtar_al_tetsh_stadium Mokhtar El-Tetsh Stadium "Stadium DB"
marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "أول ملعب كرة". Al Ahly SC Website. 21 Septemba 2019. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-07-04. Iliwekwa mnamo 2 Julai 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu. Je, unajua kitu zaidi kuhusu Uwanja wa michezo wa Mokhtar El Tetsh kama historia yake, uenezi au kanuni zake? Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |