Nenda kwa yaliyomo

Uwanja wa michezo wa Mané Garrincha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uwanja wa Taifa Mané Garrincha
Mwonekano wa juu wa uwanja
Jina maarufuArena BRB Mané Garrincha
EneoBrasília, Brazil
Ufunguzi1974
Uwezo72,788
Aina ya nyasiNyasi asilia

Uwanja wa Taifa Mané Garrincha ni uwanja wa Taifa unaotumika katika shughuli mbali mbali za kitaifa, na michezo kama mpira wa miguu ulio katika jiji la Brasília, nchini Brazil.[1] Ulipewa jina la heshima kwa mchezaji maarufu wa Brazil, Mané Garrincha, ambaye alijulikana kwa ustadi wake mkubwa katika mchezo wa soka.

Uwanja huu umetumika kwa mashindano makubwa kama Kombe la Dunia la FIFA 2014 na Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Joto mnamo 2016.[2]

Uwanja huo una uwezo wa kuchukua zaidi ya watu 70,000 na ni miongoni mwa viwanja vikubwa zaidi nchini Brazil.

  1. "Estádio Nacional Mané Garrincha". Archived from the original on 1 July 2013. Retrieved 18 October 2025.
  2. "2014 FIFA World Cup Brazil™ – Estádio Nacional". FIFA.com. Retrieved 18 October 2025.
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Uwanja wa michezo wa Mané Garrincha kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.