Uwanja wa michezo wa Loftus Versfeld
Uwanja wa michezo wa Loftus Versfeld ni uwanja wa michezo wa shirika la rugby na chama cha mpira wa miguu, uwanja huu upo katika kitongoji cha Arcadia, Pretoria katika mkoa wa Gauteng nchini Afrika Kusini. Uwanja una uwezo wa kuchukua watu 51,762 na utumika mara kwa mara kwa mechi za mpira wa miguu.
Uwanja huo ni uwanja wa nyumbani wa Bulls rugby Bulls franchise inayoshiriki mashindano ya Super Rugby na umoja Blue Bulls Currie Cup ya Afrika Kusini . ulituika kuandaa pia Fainali ya mwaka 2009 Super 14 ambayo Bulls ilishinda 61-17 dhidi ya Waikato Chiefs, na Currie Cup ya mwaka 2009, ambayo Bulls walishinda 36-24 dhidi Duma Free State.
Pia, timu ya Taifa ya chama cha rugby ya Afrika Kusini imecheza mechi kadhaa za majaribio kwenye Uwanja wa Loftus Versfeld. Walicheza na New Zealand mnamo 1970, 1996, 1999, 2003 na 2006, na Australia mnamo 1967, 1997, 2001, 2005, 2010 na 2012, pia England mnamo 1994, 2000 na 2007, na Ireland mnamo 1998.
Mnamo Juni 2010, uwanja huo ulikuwa na michezo ya ufunguzi na mchezo mmoja wa raundi ya 16 ya Kombe la Dunia la FIFA mwaka 2010.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Uwanja huo ulipewa jina la Robert Loftus Owen Versfeld, kutokana na mwanzilishi wa michezo iliyoandaliwa huko Pretoria. Kwa miaka mingi uwanja huo umekua ukibadilishwa majina kwani wafadhili walikuja na kwenda, ingawa wenyeji kila wakati wamekuwa wakiuita uwanja huo kama Loftus Versfeld. Kuanzia 11 Juni 1998 hadi 4 Februari 2003 uwanja huo uliitwa rasmi Minolta Loftus baada ya Minolta kuwa mdhamini wa jina la uwanja. Udhamini ulichukuliwa na kampuni kubwa ya usalama Securicor, ambaye alitangaza jina Securicor Loftus mnamo 5 Februari 2003. Mnamo tarehe 1 Septemba 2005 mchakato wa kubadilisha jina ulikwenda kabisa wakati mtoa huduma wa rununu Vodacom, akichukua udhamini kutoka kwa Securicor, alibadilisha uwanja huo kuwa Loftus Versfeld.
marejeo
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu. Je, unajua kitu zaidi kuhusu Uwanja wa michezo wa Loftus Versfeld kama historia yake, uenezi au kanuni zake? Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |