Utumwa barani Afrika

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Njia kuu za biashara ya watumwa katika Afrika ya kati
Kikundi cha watumwa cha Zanj huko Zanzibar (1889)

Utumwa barani Afrika ulipatikana kwa muda mrefu. Sawa na maeneo mengine ya Dunia ya kale, mifumo ya utumwa na kazi isiyo huru ilikuwa kawaida katika sehemu nyingi za Afrika. Utumwa huo ulikuwepo kabla ya kufika kwa wanfayabiashara wa watumwa Waarabu na Wazungu.

Wakati Afrika ilipoingizwa zaidi katika biashara ya kimaifa ya watumwa, mifumo hiyo ya utumwa wa kimapokeo ilianza kupeleka wafúngwa pia kwa masoko ya watumwa nje ya Afrika [1]. Biashara hiyo ya kimataifa ilitokea katika biashara ya watumwa kuvukia Sahara, biashara ya watumwa katika Bahari Hindi, na biashara ya watumwa ya Atlantiki (ambayo ilianza karne ya 16).

Utumwa wa kimapokeo katika Afrika ulipatikana kwa aina tofauti: Utumwa wa deni, utumwa wa mateka wa vita, utumwa wa kijeshi, utumwa wa ukahaba, na utumwa wa jinai; vyote vilifanywa katika sehemu anuwai za Afrika. [2] Utumwa kwa madhumuni ya nyumbani na kwa mahitaji ya watawala ulienea kote Afrika. Utumwa wa mashambani ulitokea pia, hasa kwenye pwani la Afrika ya Mashariki na katika sehemu za Afrika ya Magharibi. Umuhimu wa utumwa wa mashambani ya ndani uliongezeka wakati wa karne ya 19, kwa sababu ya kukomeshwa kwa biashara ya watumwa ya Atlantiki na katika Bahari Hindi. [3] Madola kadhaa ya Kiafrika yaliyotegemea biashara ya watumwa ya kimataifa yalirekebisha uchumi wao kuelekea biashara halali ambako bidhaa zilizalishwa na watumwa. [4]

Aina za utumwa[hariri | hariri chanzo]

Kulikuwa na aina tofauti za utumwa na kazi isiyo huru katika Afrika. Aina hizo ziliathiriwa na desturi za jamii za kienyeji lakini pia na taasisi ya utumwa wa Kirumi, mafundisho ya Wakristo kuhusu utumwa, taasisi ya utumwa wa Kiislam kupitia biashara ya watumwa ya Kiislamu, na hatimaye biashara ya watumwa ya Atlantiki. [5] [1]

Utumwa ulikuwa sehemu ya muundo wa uchumi wa jamii nyingi za Kiafrika kwa karne nyingi, ingawa viwango vilitofautiana. [6]. Ibn Batutta aliyetembelea Milki ya Mali katikati ya karne ya 14, alisimulia kwamba wakazi wa eneo hilo walishindana kwa idadi ya watumwa na watumishi wao, na yeye mwenyewe alipewa mtumwa kama "zawadi ya ukarimu."[7]

Katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, hali ya kisheria ya watumwa mara nyingi ilikuwa tata; watumwa walikuwa na haki mbalimbali na pia uhuru katika mambo kadhaa, na mabwana wao walibanwa katika uwezo wao kuwatendea na kuwauza. [8] Jamii nyingi ziliweka tofauti kati ya aina tofauti za watumwa: kwa mfano, kutofautisha kati ya wale waliozaliwa katika utumwa na wale ambao walitekwa katika vita. [9] Tofauti za utumwa barani Afrika zilihusiana na miundo ya ukoo. Katika jamii nyingi za Kiafrika, ambapo ardhi haingeweza kumilikiwa, idadi ya watumwa ilitumika kama njia ya kuonyesha ushawishi mtu alikuwa nao na kupanua uhusiano na koo nyingine. Hii ilifanya watumwa kuwa sehemu ya kudumu ya ukoo wa bwana, na watoto wa watumwa waliweza kuendelea kama sehemu ya ukoo wa Bwana.[10] [1] Watoto wa watumwa waliozaliwa katika familia waliweza kuhesabiwa kama watoto wa ukoo wa bwana na kupanda ngazi katika jamii, hata wakati mwingine hadi cheo cha chifu.[9]

Walakini, unyanyapaa mara nyingi ulibaki, na kulitokea pia na utengano mkali kati ya watoto wa watumwa katika ukoo na watoto wa sehemu huru ya familia.[11]

Utumwa wa kibiashara[hariri | hariri chanzo]

Utumwa wa kibiashara (ing chattel slavery) ni aina kali ya utumwa ambapo mtumwa hutendewa kama mali ya mmiliki. Kwa hiyo, mmiliki yuko huru kumuuza, kumnunua au kumtendea mtumwa kama vile atakavyokuwa na vitu vingine vilivyo mali yake, na watoto wa mtumwa mara nyingi hubaki kama mali ya bwana. [12] Kuna taarifa za aina hiyo ya utumwa mkali katika bonde la Mto Nile, sehemu kubwa ya Sahel na pia Afrika Kaskazini, lakini watafiti hawana uhakika kuhusu upatikanaji katika sehemu nyingine za bara kabla ya taarifa za kimaandishi ya wafanyabiashara Waarabu na Wazungu. [13]

Utumishi wa nyumba[hariri | hariri chanzo]

Kidesturi watumwa wengi walitumiwa katika nyumba za mabwana ambako walibaki na uhuru fulani. Watumwa wa nyumbani wangetazamwa kama sehemu ya ukoo wa bwana na kwa kawaida wasingeuzwa kwa wengine isipokuwa kwa sababu maalumu. [14] Watumwa hao waliweza kuwa na mapato yao waliweza kununua mali na ardhi , waliweza kuoa na mara nyingi waliweza kupitisha mali kwa watoto wao. [9] [15]

Utumishi wa deni[hariri | hariri chanzo]

Katika utumishi wa deni (ing. pawnship) mtu hutumiwa kama dhamana kwa deni. Mwiwa (mdeni), mtoto wake au mtu mwingine wa ukoo wake anapaswa kufanya kazi bila malipo kwa mwia. Utumishi wa aina hiyo ulikuwa umbo la dhamana liliopatikana mahali pengi katika Afrika Magharibi . [16] Ilikuwa kuhusu ahadi ya mtu kumtumikia mtu mwingine anayemtolea mkopo. [17] Utumishi wa deni uliweza kufanana na utumwa lakini mara nyingi ulikuwa tofauti na utumwa halisi; hasa kwa sababu mapatano kuhusu utumishi mara nyingi yalikuwa kwa muda fulani tu, au aina maalumu za kazi. Utumishi wa aina hiyo ulikuwa kawaida katika Afrika Magharibi kabla ya mawasiliano na Ulaya, pamoja na watu wa Akan, watu wa Ewe, watu wa Yoruba, na watu wa Edo , na umbo tofauti pia kati ya Waefik, Waigbo, Waijaw, na Wafon ). [18] [19] [20]

Utumwa wa kijeshi[hariri | hariri chanzo]

Watumwa wa dhabihu katika Forodha za kila mwaka za Dahomey - kutoka Historia ya Dahomy, Ufalme wa bara wa Afrika, 1793

Utumwa wa kijeshi ulikuwa pamoja na kujipatia wafungwa na kuwafundisha kazi ya uanajeshi. Hao waliendelea kuwa hali ya watumwa wa kijeshi hata baada ya kumaliza muda wao.[21] Vikosi vya askari watumwa viliendeshwa na kiongozi, ambaye angeweza kuwa mkuu wa serikali wa eneo fulani au kiongozi wa kujitegemea, aliyetumia askati wake kwa malipo au kwa masilahi yake yeye mwenyewe.

Utumwa wa kijeshi ulitokea hasa katika bonde la Mto Nile (nchini Sudan na Uganda), ambako vikosi vya wanajeshi watumwa viliendeshwa na mamlaka mbali mbali za Kiislamu[21], halafu kati ya viongozi wa kijeshi wa Afrika Magharibi. [22] Vikosi vya kijeshi huko Sudan viliundwa katika miaka ya 1800 kwa njia ya uvamizi wa kijeshi ambako wafungwa wengi walikamatwa.

Watumwa wa dhabihu[hariri | hariri chanzo]

Dhabihu ya wanadamu ilikuwa kawaida katika milki za Afrika Magharibi hadi wakati wa karne ya 19. [23] Katika jamii ambazo zilifanya dhabihu ya wanadamu, watumwa walikuwa idadi kubwa ya wahanga. [1]

Kwenye sikukuu ya kifalme ya kila mwaka katika milki ya Dahomey takriban wafungwa 500 waliuawa kama kafara. Dhabihu zilifanywa kote kwenye pwani ya Afrika Magharibi na maeneo ya bara. [24] Dhabihu zilikuwa za kawaida katika Milki ya Benin, katika Ghana, na katika madola madogo ya kujitegemea katika maeneo ya kusini mwa Nigeria ya leo. Katika Mkoa wa Ashanti, adhabu ya kifo ilitekelezwa kwa umbo la dhabihu ya wanadamu.[25]

Biashara ya watumwa wa ndani[hariri | hariri chanzo]

Mataifa na makabila mengi kama Milki ya Bono, Waashanti wa Ghana ya leo na Wayoruba wa Nigeria walihusika katika biashara ya watumwa. [26] Jamii kama Waimbangala wa Angola na Wanyamwezi wa Tanzania walishiriki katika vita dhidi ya jamii wa Waafrika jirani na kuwapeleka kama wafungwa hadi pwani walipouzwa kwa wafanyabiashara Wazungu na Waarabu. Wanahistoria John Thornton na Linda Heywood wa Chuo Kikuu cha Boston wamekadiria kuwa kati ya Waafrika waliotekwa na kisha kuuzwa kama watumwa kwenda Amerika katika biashara ya watumwa ya Atlantiki, karibu asilimia 90 walikamatwa na Waafrika wengine ambao waliwauzia wafanyabiashara kutoka Ulaya. Henry Louis Gates, Mwenyekiti wa Idara ya Mafunzo ya Kiafrika na Kimarekani-Kiafrika, amesema kuwa "bila ushirikiano wa kibiashara kati ya matabaka ya juu ya Kiafrika, wafanyabiashara wa Ulaya na mawakala wa kibiashara, [27] biashara ya watumwa kwenda "Ulimwengu Mpya" (Amerika) haingewezekana, angalau siyo kwa kiwango kilichotokea. " [28]

Hali ya utumwa kote Afrika[hariri | hariri chanzo]

Watumwa wa Malagasi ( Andevo ) wakiwa wamembeba Malkia Ranavalona I wa Madagaska

Afrika Kaskazini[hariri | hariri chanzo]

Wanubi Weusi wakisubiri kuuzwa katika soko la watumwa huko Misri ya zamani.

Utumwa kaskazini mwa Afrika ulianzia Misri ya Kale. Ufalme Mpya (1558–1080 KK) ulileta idadi kubwa ya watumwa kama wafungwa wa vita kwenye bonde la Mto Nile na kuwatumia kwa kazi za nyumbani na kazi za umma zilizosimamiwa.

Kuachiliwa kwa watumwa wa Kikristo kwa kulipa fidia na watawa wa Katoliki huko Algiers mnamo 1661.
Kuchoma Kijiji Barani Afrika, na Kukamata Wakazi Wake (uk. 12, Februari 1859, XVI) [29]

Utumwa wa kibiashara ulikuwa halali na kawaida katika maeneo yote ya Afrika Kaskazini wakati wa utawala wa Dola la Roma (145 KK - mnamo 430 BK), na Waroma wa Mashariki kutoka 533 hadi 695). Biashara ya watumwa iliyowaleta kupitia jangwa hadi Afrika Kaskazini iliendelea. Ilikuwepo katika nyakati za Waroma wa Kale, na kuna hati tza kihistoria zinazoonyesha kuwa ilisimamiwa hapo kwa mikataba. [12] Jamhuri ya Roma ilipopanuka, ilifanya wafungwa kutoka vita zake kuwa watumwa. Kwa mfano, Orosius aliandika kwamba Roma ilifanya watumwa watu 27,000 kutoka Afrika Kaskazini mnamo 256 KK.

Mamluki walikuwa askari watumwa ambao walifanywa Waislamu kufundishwa uanajeshi. Waliwahudumia makhalifa wa Kiislamu na masultani Ayyubi wakati wa enzi ya kati . Mamluki wa kwanza walihudumia makhalifa wa Waabbasi katika karne ya 9 pale Baghdad. Kuanzia 1250 Misri ilitawaliwa na nasaba ya mamluki waliokuwa na asili ya watumwa wa kijeshi Waturuki. Watumwa kutoka Ulaya walikuwa kikosi maalum jeshini wakatawala Misri mara kadhaa baada ya kuasi dhidi ya mabwana wao. [30] Imekadiriwa kuwa takriban milioni 1 Wazungu walitekwa na maharamia kwenye Bahari Mediteranea na kuuzwa kama watumwa kwa Afrika Kaskazini na Milki ya Osmani kati ya karne ya 16 na 19. [31] [32]

Pembe ya Afrika[hariri | hariri chanzo]

Mwanamke 'mtumwa' huko Mogadishu (1882-1883)

Katika Pembe la Afrika, wafalme wa Kikristo wa Milki ya Ethiopia mara nyingi waliuza watumwa wa kipagani kutoka Waniloti kutoka mipaka yao ya magharibi kwa wafanyabiashara Waarabu.[33] [34] Sultani za Kisomali na Kiafar, kama vile Usultani wa Adal pia walifanya biashara ya watumwa wa Zanj ( Wabantu ) ambao walikamatwa kutoka bara. [35]

Watumwa nchini Ethiopia, karne ya 19.

Afrika ya Kati[hariri | hariri chanzo]

Soko la watumwa huko Khartoum, c. 1876
Mtumwa wa kike mzee, c. 1911/15, inayomilikiwa na Njapundunke, mama wa mfalme wa Bamum Ibrahim Njoya

Kuna historia ya kimdomo inayosimulia utumwa ulikuwepo katika Ufalme wa Kongo tangu wakati wa uundaji wake na Lukeni lua Nimi akimtumikisha Mwene Kabunga ambaye alimshinda kuanzisha ufalme wake. [36] Taarifa za kimaandishi ya Wareno zilitaja kuwepo kwa watumwa katika Ufalme wa Kongo, ambao walikuwa wafungwa wa vita kutoka Ufalme wa Ndongo .

Utumwa ulikuwa wa kawaida kando ya Mto Kongo. Katika nusu ya pili ya karne ya 18 maeneo hayo yalikuwa chanzo kikuu cha watumwa kwa Biashara ya Utumwa ya Atlantiki, wakati bei kubwa ya watumwa kwenye pwani ilifanya biashara ya watumwa ya masafa marefu kuwa na faida. Wakati biashara ya Atlantiki ilipokwisha, bei za watumwa zilipungua sana. Hii ilisababisha kukua kwa biashara ya watumwa wa ndani ambako wafanyabiashara wenyeji walininunua watumwa kwa shabaha ya kuunda vijiji vipya. [37] Tofauti ilifanywa kati ya aina mbili tofauti za watumwa katika mkoa huu; watumwa ambao walikuwa wameuzwa na kikundi cha jamaa zao, haswa kama matokeo ya tabia isiyofaa kama uzinzi, hawakuweza kujaribu kukimbia. Mbali na wale wanaofikiriwa kuwa hawapendezi kijamii, uuzaji wa watoto pia ulikuwa wa kawaida wakati wa njaa. [38] Watumwa ambao walikamatwa, hata hivyo, walikuwa na uwezekano wa kujaribu kutoroka na ilibidi wahamishwe mamia ya kilomita kutoka nyumbani kwao kama kinga dhidi ya hii. [39]

Afrika Magharibi[hariri | hariri chanzo]

Ramani ya Homann ya biashara ya watumwa ya ndani huko Afrika Magharibi, kutoka Senegal na Cape Blanc hadi Guinea, mito ya Cacongo na Barbela, na Ziwa la Ghana kwenye Mto Niger hadi Regio Auri (1743).

Aina anuwai za utumwa zilipatikana katika jamii tofauti za Afrika Magharibi kabla ya biashara na Ulaya. [40] Utumwa ulikuwepo, lakini haukuwa muhimu sana katika jamii nyingi ukilinganishwa na hali ya baadaye tangu kuanza kwa Biashara ya Watumwa wa Atlantiki. [41] [42]

Watumwa katika maeneo ya Sahel walikuwa sehemu ndogo ya watu wote, waliishi ndani ya kaya na walifanya kazi pamoja na watu huru wa kaya.

Wakati biashara ya watumwa kupitia Sahara ilipoanza kukua, milki kadhaa zilistawi kwa kushiriki katika biashara hiyo; pamoja na Dola ya Ghana, Milki ya Mali, Bono na Dola ya Songhai . [43] Walakini, jamii nyingine huko Afrika Magharibi zilipinga biashara ya watumwa kwa karne kadhaa[44] kama vile Wajola, Wakru na Wabaga [45], na Falme za Wamossi.

Wakati biashara ya watumwa ya Atlantiki ilipoanza, mahitaji ya watumwa katika Afrika Magharibi yaliongezeka na milki mbalimbali zilijenga uchumi wao kwenye biashara hiyo. Milki zilizoongoza katika kukamata wafungwa na kuwauza zilikuwa pamoja na Ashanti na Dahomey.

Pia idadi ya watumwa wa nyumbani iliongezeka sana katika Afrika Magharibi. [46] Mwingereza Hugh Clapperton aliandika mnamo 1824 kwamba kwamba nusu ya watu wa Kano walikuwa watumwa. [47]

Mfanyabiashara wa watumwa wa Gorée, c. 1797

Katika eneo la Senegambia, kati ya 1300 na 1900, karibu theluthi moja ya idadi ya watu walikuwa watumwa. Katika milki ya kwanza ya Kiislamu ya Sahel ya magharibi, pamoja na Ghana (750-1076), Mali (1235-1645), Segou (1712-1861), na Songhai (1275-1591), karibu theluthi moja ya idadi ya watu walikuwa watumwa. Nchini Sierra Leone katika karne ya 19 karibu nusu ya wakazi wote walikuwa watumwa.

Kati ya Waashanti na Wayoruba theluthi moja ya watu wote walikuwa watumwa[48], vilevile theluji moja ya wakazi wa Kanem (1600-1800) [49]. Nusu ya watu wa ukhalifa wa Sokoto iliyoundwa na Wahausa kaskazini mwa Nigeria na Kamerun walikuwa watumwa katika karne ya 19.

Afrika ya Mashariki[hariri | hariri chanzo]

Mfanyabiashara wa watumwa wa Kizanzibari Tippu Tip alikuwa na watumwa 10,000

Katika biashara ya baharini kutoka eneo la Afrika ya Mashariki hadi Uajemi, Uchina, na India tangu milenia ya kwanza AD, watumwa walitajwa kama bidhaa lakini hawakuwa muhimu sanam bidha muhimu zilikuwa dhahabu na pembe za ndovu. Biashara ya watumwa ilikuwa ndogo na vyanzo vinataja kutekwa kwa wanawake na watoto kando ya visiwa vya Kilwa Kisiwani, Madagaska, na Pemba.

Imekadiriwa kwamba wafanyabiashara Waarabu walibeba takriban watumwa 1,000 kila mwaka katika karne kuanzia mwaka 800 hadi mnamo mwaka 1800.[50]

Tangu mwaka 1500 Wareno walifika katika Afrika ya Mashariki wakiwa na vituo kama Ilha de Mocambique na Mombasa kwa safari zao kwenda Goa na Uhindi; walianza kubeba pia idadi ndogo ya watumwa Waafrika kuelekea Uhindi. Katika karne ya 17 Waingereza walianza kununua watumwa kutoka Msumbiji na Madagaska kwa mahitaji yao katika Uhindi[51]. Baadaye ni hasa Wafaransa walioingia katika biashara ya watumwa katika Bahari Hindi, wakichukua watumwa kwa koloni zao kwenye Visiwa vya Maskarena (Morisi, Reunion) kutoka Afrika ya Magharibi, Uhindi na mabandari ya Afrika ya Mashariki kama Kilwa. Manmo 1776 sultani wa Kilwa alifanya mkataba na Wafaransa ambako aliahidi kuwapatia watumwa 1,000 kila mwaka[52].

Tangu miaka mnamo 1800, siasa ya Uingereza kuhusu utumwa ulibadilika. 1822 Waingereza walimshawishi Sultani wa Oman kukubali mkataba wa Moresby ambao uliweka vikwazo mbalimbali kwa usafirishaji wa watumwa kwenye bahari[53]. Ihali kuwepo kwa manowari za Uingereza zilizokamata mara kwa mara jahazi zilizobeba watumwa, wafanyabiashara Waarabu na Waswahili walianza kuanzisha mashamba kando ya pwani na kwenye visiwa ili watumie watumwa kwa kuzalisha bidhaa za biashara halali. Badiliko hilo na hasa kuanzishwa na upanuzi wa kilimo cha karafuu pale Unguja na Pemba lilisababisha kuongezeka kwa biashara ya watumwa, ila sasa hawakupelekwa katika nchi za mbali lakini walitumiwa kwenye mashamba ya pwani na kwenye visiwa vya Zanzibar. Mfanyabiashara mmoja mashuhuri na pia mjasiriamali wa karafuu alikuwa Tippu Tip. [54]

Mwandishi na mwanahistoria Timothy Insoll aliandika: "Takwimu zinarekodi kusafirishwa kwa watumwa 718,000 kutoka pwani ya Waswahili wakati wa karne ya 19, na kubakizwa kwa 769,000 kwenye pwani." [55] Kwa nyakati tofauti, kati ya asilimia 65 na 90 ya wakazi wa Unguja walikuwa utumwa. Kwenye pwani la Kenya, asilimia 90 ya wakazi walikuwa watumwa na nusu ya wakazi wa Madagaska walikuwa watumwa. [56]

Mabadiliko ya utumwa barani Afrika[hariri | hariri chanzo]

Mlango wa Hakuna Kurudi huko Ouidah . Kumbukumbu ya biashara ya watumwa kupitia bandari ya Ouidah.

Hali ya utumwa barani Afrika ilibadilishwa kupitia michakato minne mikubwa:

  • biashara ya utumwa kupitia Sahara,
  • biashara ya watumwa wa Bahari ya Hindi,
  • biashara ya watumwa ya Atlantiki,
  • harakati za kupinga utumwa katika karne ya 19 na 20.

Kila moja ya michakato hii ilibadilisha aina, kiwango, na uchumi wa utumwa barani Afrika. [1]

Waafrika hasa katika magharibi walikuwa na habari kuhusu ukali wa utumwa pale A,erika ambako wengi walitumwa. Waafrika kadhaa wa matabaka wa juu walitembelea Ulaya kwa jahazi za watumwa kupitia Amerika. Mfano mmoja ni safari ya Antonio Manuel, balozi wa Kongo huko Vatikani, aliyesafiri kwenda Ulaya mnamo mwaka 1604, akipita kwanza huko Bahia, Brazil, ambapo aliwweza kumweka huru mtu wa nyumbani ambaye alikuwa amekamatwa na kuuzwa kimakosa. Walikuwepo wafalme wa Kiafrika waliotuma watoto wao katika jahazi hizohizo za watumwa kwenda kusoma huko Ulaya.[28] Ufalme wa Dahomey ulituma angalau mara tano ubalozi kwenda Brazil na Ureni katika miaka ya 1750 and 1818[57]

Biashara ya Kuvukia Sahara na ya Bahari ya Hindi[hariri | hariri chanzo]

Biashara ya watumwa katika Bahari ya Hindi inarudi mnamo 2500 KWK. [58] Wababeli wa kale, Wamisri, Wagiriki, Wahindi na Waajemi wote walifanya biashara ya watumwa kwa kiwango kidogo katika Bahari ya Hindi (na wakati mwingine Bahari ya Shamu ). [59] Biashara ya watumwa katika Bahari Nyekundu karibu wakati wa Alexander the Great inaelezewa na Agatharchides . Jiografia ya Strabo (iliyokamilishwa baada ya 23 BK) inawataja Wagiriki kutoka Misri wanaofanya biashara ya watumwa katika bandari ya Adulis na bandari zingine kwenye pwani ya Somalia. [60] Historia ya asili ya Pliny Mkubwa (iliyochapishwa mnamo 77 BK) pia inaelezea biashara ya watumwa ya Bahari ya Hindi. Katika karne ya 1 WK, Periplus ya Bahari ya Erythraean ilishauri juu ya fursa za biashara ya watumwa katika mkoa huo, haswa katika biashara ya "wasichana wazuri wa masuria." Kulingana na mwongozo huu, watumwa walisafirishwa kutoka Omana (labda karibu na Oman ya kisasa) na Kanê hadi pwani ya magharibi ya India. Biashara ya zamani ya watumwa ya Bahari ya Hindi iliwezeshwa kwa kujenga boti zenye uwezo wa kubeba idadi kubwa ya wanadamu katika Ghuba ya Uajemi kwa kutumia kuni zilizoingizwa kutoka India. Shughuli hizi za ujenzi wa meli zinarudi nyakati za Babeli na Achaemenid . [61]

Baada ya ushiriki wa Dola ya Byzantine na Dola ya Sassanian katika biashara ya watumwa katika karne ya 1, ikawa biashara kubwa. [59] Cosmas Indicopleustes aliandika katika Topografia yake ya Kikristo (550 BK) kwamba watumwa waliokamatwa Ethiopia wataingizwa nchini Misri ya Byzantine kupitia Bahari Nyekundu. [60] Alitaja pia kuagiza kwa matowashi na Byzantine kutoka Mesopotamia na India. Baada ya karne ya 1, usafirishaji wa Waafrika weusi ukawa "sababu ya kila wakati". [61] Chini ya Wasassani, biashara ya Bahari ya Hindi haikutumiwa kusafirisha watumwa tu, bali pia wasomi na wafanyabiashara.

Utumwa wa Waafrika kwa masoko ya mashariki ulianza kabla ya karne ya 7 lakini ilibaki katika viwango vya chini hadi 1750. [62] Kiasi cha biashara kilifikia karibu 1850 lakini kwa kiasi kikubwa kingemalizika mnamo 1900. Ushiriki wa Waislamu katika biashara ya watumwa ulianza katika karne ya nane na tisa BK, ikianza na harakati ndogo za watu kwa kiasi kikubwa kutoka eneo la Maziwa Makuu mashariki na Sahel . Sheria ya Kiislamu iliruhusu utumwa, lakini ilikataza utumwa unaowahusisha Waislamu wengine wa zamani; kama matokeo, lengo kuu la utumwa walikuwa watu ambao waliishi katika maeneo ya mipaka ya Uislamu barani Afrika. [12] Biashara ya watumwa kote Sahara na kuvuka Bahari ya Hindi pia ina historia ndefu inayoanza na udhibiti wa njia za baharini na wafanyabiashara wa Afro-Arab katika karne ya tisa. Inakadiriwa kuwa, wakati huo, watu elfu chache watumwa walikuwa wakichukuliwa kila mwaka kutoka Bahari ya Shamu na pwani ya Bahari ya Hindi. Ziliuzwa katika Mashariki ya Kati . [63] [64] Biashara hii iliongezeka kwani meli bora zilisababisha biashara zaidi na mahitaji makubwa ya wafanyikazi kwenye mashamba katika mkoa huo. [65] Hatimaye, makumi ya maelfu kwa mwaka walikuwa wakichukuliwa. [66] Kwenye Pwani ya Kiswahili, watumwa wa Afro-Arab waliteka watu wa Bantu kutoka ndani na kuwaleta kwenye littoral . [67] [68] Huko, watumwa polepole walijumuishwa katika maeneo ya vijijini, haswa katika visiwa vya Unguja na Pemba .

Wafanyabiashara wa watumwa wa Kiswahili na Waarabu na mateka wao kando ya Mto Ruvuma nchini Msumbiji, karne ya 19

Zanzibar wakati mmoja ilikuwa bandari kuu ya biashara ya utumwa ya Afrika Mashariki, na chini ya Waarabu wa Omani katika karne ya 19 idadi ya watumwa 50,000 walikuwa wakipitia jiji kila mwaka. [69]

Biashara ya watumwa Ulaya katika Bahari ya Hindi ilianza wakati Ureno ilianzisha Estado da Índia mwanzoni mwa karne ya 16. Kuanzia wakati huo hadi miaka ya 1830 hivi. Watumwa walisafirishwa kutoka Msumbiji kila mwaka na takwimu kama hizo zimekadiriwa kwa watumwa walioletwa kutoka Asia hadi Ufilipino wakati wa Muungano wa Iberia (1580-1640).

Kiasi cha utumwa[hariri | hariri chanzo]

Kiwango cha utumwa ndani ya Afrika na biashara ya watumwa kwenda maeneo mengine hakijulikani kikamilifu. Makadirio kuhusu biashara ya watumwa ya Atlantiki (iliyochunguliwa vizuri zaidi) yanacheza kati ya watu milioni 8 hadi milioni 20. [70] Hazinadata ya Biashara ya Utumwa ya Atlantiki inakadiria kuwa biashara ya watumwa ya Atlantiki ilichukua karibu watu milioni 12.8 kati ya 1450 na 1900. [1] [71] Biashara ya watumwa kuvukia Sahara na Bahari Nyekundu kutoka Pembe ya Afrika, na Afrika Mashariki, imekadiriwa kuwa watu milioni 6.2 kati ya mwaka 600 na 1600. Ingawa kiwango kilipungua kutoka Afrika Mashariki katika miaka ya 1700, kiliongezeka katika miaka ya 1800 na inakadiriwa kuwa milioni 1.65 kwa karne hiyo. [72]

Makadirio ya Patrick Manning ni kwamba karibu watumwa milioni 12 waliingia katika biashara ya Atlantiki kati ya karne ya 16 na 19, lakini karibu milioni 1.5 walikufa kwenye safari. Karibu watumwa milioni 10.5 walifika Amerika. Mbali na watumwa waliokufa baharini, Waafrika zaidi walifariki wakati wa vita za kukamata watumwa barani Afrika na matembezi ya kulazimishwa hadi pwani. Manning anakadiria kuwa milioni 4 walikufa ndani ya Afrika baada ya kukamatwa, na wengi zaidi walikufa wakiwa wadogo.

Mjadala kuhusu athari za kidemografia[hariri | hariri chanzo]

Picha ya kijana mtumwa Zanzibar . 'Adhabu ya bwana wa Kiarabu kwa kosa kidogo.' c. 1890.

Athari kwa uchumi wa Ulaya[hariri | hariri chanzo]

Karl Marx katika historia yake ya uchumi wa ubepari, Das Kapital, alidai kwamba "... kugeuza Afrika kuwa eneo kwa uwindaji wa kibiashara wa ngozi nyeusi [ambayo ni biashara ya utumwa], iliashiria alfajiri ya enzi ya uzalishaji wa kibepari. "Alisema kwamba biashara ya watumwa ilikuwa sehemu ya kile alichokiita" limbikizo asilia " la rasilmali ya Ulaya, limbikizo la utajiri ambalo kabla ya ubepari lililotangulia na kuunda misingi ya kifedha kwa kuanzisha viwanda vya Uingereza na ujio wa mfumo wa kibepari wa uzalishaji. [73]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 Lovejoy, Paul E. (2012). Transformations of Slavery: A History of Slavery in Africa. London: Cambridge University Press.  Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; name "Lovejoy-2012" defined multiple times with different content
  2. Foner, Eric (2012). Give Me Liberty: An American History. New York: W. W. Norton & Company. p. 18. 
  3. Fernyhough, Timothy (1988). "Slavery and the Slave Trade in Southern Ethiopia in the 19th Century". Slavery & Abolition 9 (3): 103–130. ISSN 0144-039X. doi:10.1080/01440398808574965. 
  4. David Eltis; Stanley L. Engerman; Seymour Drescher et al., eds. (2017). "Slavery in Africa, 1804-1936". New York: Cambridge University Press.  Missing or empty |title= (help);
  5. "Slavery, Slave Trade". doi:10.1163/1878-9781_ejiw_com_000524. 
  6. Painter, Nell Irvin; Berlin, Ira (2000). "Many Thousands Gone: The First Two Centuries of Slavery in North America". African American Review 34 (3): 515. ISSN 1062-4783. JSTOR 2901390. doi:10.2307/2901390. 
  7. Noel King (ed.), Ibn Battuta in Black Africa, Princeton 2005, p. 54.
  8. Fage, J.D. (1969). "Slavery and the Slave Trade in the Context of West African History". The Journal of African History 10 (3): 393–404. doi:10.1017/s0021853700036343. 
  9. 9.0 9.1 9.2 Rodney, Walter (1966). "African Slavery and Other Forms of Social Oppression on the Upper Guinea Coast in the Context of the Atlantic Slave-Trade". The Journal of African History 7 (3): 431–443. JSTOR 180112. doi:10.1017/s0021853700006514. 
  10. Gudmestad, Robert (2006-01-26). "Technology and the World the Slaves Made". History Compass 4 (2): 373–383. ISSN 1478-0542. doi:10.1111/j.1478-0542.2006.00313.x. 
  11. Snell, Daniel C. (2011). "Slavery in the Ancient Near East". In Keith Bradley and Paul Cartledge. The Cambridge World History of Slavery. New York: Cambridge University Press. pp. 4–21. 
  12. 12.0 12.1 12.2 Alexander, J. (2001). "Islam, Archaeology and Slavery in Africa". World Archaeology 33 (1): 44–60. JSTOR 827888. doi:10.1080/00438240126645.  Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; name "Alexander" defined multiple times with different content
  13. Gaspar, D. B. (1998). More than chattel: black women and slavery in the Americas. Bloomington: Indiana University Press. 
  14. Kett, Anna Vaughan (2017-04-20). "Without the Consumers of Slave Produce There Would Be No Slaves". University of Illinois Press 1. doi:10.5406/illinois/9780252038266.003.0005. 
  15. Domestic Slavery: What Is It?. Anti-Slavery International.
  16. Douglas, Mary (1964). "Matriliny and Pawnship in Central Africa". Africa 34 (4): 301–313. ISSN 0001-9720. JSTOR 1157471. doi:10.2307/1157471. 
  17. "Pledges. Delivery to Create a Future Pledge. Assignment of Debt to One Person and of Pledge to Another". Harvard Law Review 35 (3): 345. 1922. ISSN 0017-811X. JSTOR 1329636. doi:10.2307/1329636. 
  18. Regnier, Denis (2015). "Clean people, unclean people: the essentialisation of 'slaves' among the southern Betsileo of Madagascar". Social Anthropology 23 (2): 152–168. ISSN 0964-0282. doi:10.1111/1469-8676.12107. 
  19. Paul E. Lovejoy and David Richardson (2001). "The Business of Slaving: Pawnship in Western Africa, c. 1600–1810". The Journal of African History 42 (1): 67–89. doi:10.1017/S0021853700007787. 
  20. Paul E. Lovejoy; Toyin Falola, eds. (2003). Pawnship, Slavery, and Colonialism in Africa. Trenton, NJ: Africa World Press. 
  21. 21.0 21.1 Johnson, Douglas H. (1989). "The Structure of a Legacy: Military Slavery in Northeast Africa". Ethnohistory 36 (1): 72–88. JSTOR 482742. doi:10.2307/482742. 
  22. Wylie, Kenneth C. (1969). "Innovation and Change in Mende Chieftaincy 1880–1896". The Journal of African History 10 (2): 295–308. JSTOR 179516. doi:10.1017/s0021853700009531. 
  23. Drew University. Library. (1805–1917). [Quaker pamphlet collection]. OCLC 880321617. 
  24. "Figure 3. Schematic of experimental design.". doi:10.7554/elife.11695.005. 
  25. Clifford Williams (1988) However, The International Journal of African Historical Studies, Vol. 21, No. 3. (1988), pp. 433–441
  26. Peterson, Derek R.; Gavua, Kodzo; Rassool, Ciraj (2015-03-02). The Politics of Heritage in Africa (in English). Cambridge University Press. ISBN 978-1-107-09485-7. 
  27. "Harvard University, Department of African and African American Studies (AAAS)". doi:10.1163/_afco_asc_1693. 
  28. 28.0 28.1 Henry Louis Gates Jr.. "Ending the Slavery Blame-Game".  Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; name "Ending the Slavery Blame-Game" defined multiple times with different content
  29. "Burning of a Village in Africa, and Capture of its Inhabitants". Wesleyan Juvenile Offering XVI: 12. February 1859. Retrieved 10 November 2015. 
  30. The Mamluk (Slave) Dynasty (Timeline). Sunnahonline.com. Jalada kutoka ya awali juu ya 2011-07-16. Iliwekwa mnamo 2021-02-22.
  31. Robert C. Davis (December 2003). Christian Slaves, Muslim Masters: White Slavery in the Mediterranean, the Barbary Coast and Italy, 1500–1800. London: Palgrave Macmillan. p. 45. ISBN 978-0333719664. Retrieved 15 May 2015. 
  32. Jeff Grabmeier (8 March 2004). When Europeans Were Slaves: Research Suggest White Slavery Was Much More Common Than Previously Believed. researchnews.osu.edu. OSU News Research Archive. Jalada kutoka ya awali juu ya 25 July 2011. Iliwekwa mnamo 15 May 2015.
  33. From Isolation to Integration. World Bank. 2020-03-01. doi:10.1596/33513. 
  34. Pankhurst. Ethiopian Borderlands, p. 432.
  35. Willie F. Page, Facts on File, Inc. (2001). Encyclopedia of African History and Culture: African kingdoms (500 to 1500), Volume 2. Facts on File. p. 239. ISBN 978-0816044726. 
  36. Heywood, Linda M.; 2009 (2009). "Slavery and its transformations in the Kingdom of Kongo: 1491–1800". The Journal of African History 50: 1–22. doi:10.1017/S0021853709004228. 
  37. Thursby, Jerry; Thursby, Marie (2000). "Who is Selling the Ivory Tower? Sources of Growth in University Licensing". Cambridge, MA. doi:10.3386/w7718.  Unknown parameter |doi-access= ignored (help)
  38. Lawrence, Richard (1809). Observations on the causes which constitute unsoundness in horses : considered in regard to the sale and purchase of those animals / by Richard Lawrence, veterinary surgeon. London: printed by R. Jabet. doi:10.5962/bhl.title.21425. 
  39. Harms, Robert W. (1981). River of Wealth, River of Sorrow: The Central Zaire Basin in the Era of the Slave and Ivory Trade, 1500-1891. New Haven: Yale University Press. pp. 28–39. ISBN 978-0300026160. 
  40. Manning, Patrick (1983). "Contours of Slavery and Social Change in Africa". American Historical Review 88 (4): 835–857. JSTOR 1874022. doi:10.2307/1874022. 
  41. Nwokeji, U. G. (2011). The Cambridge World History of Slavery Volume 3. Cambridge University Press. pp. 86, 88. 
  42. Stillwell, Sean (2014). Slavery and Slaving in African History. Cambridge University Press. pp. 47, 179, 192, 211. 
  43. Meillassoux, Claude (1991). The Anthropology of Slavery: The Womb of Iron and Gold. Chicago: University of Chicago Press. 
  44. "– Slave Prices Data". The Atlantic Slave Trade from West Central Africa, 1780–1867: 176–177. 2017-06-26. ISBN 9781316771501. doi:10.1017/9781316771501.011. 
  45. Hillbom, Ellen. An Economic History of Development in sub-Saharan Africa. Palgrave. p. 70. 
  46. Manning, Patrick (1990). Slavery and African Life: Occidental, Oriental, and African Slave Trades. London: Cambridge. 
  47. Humphrey J. Fisher (2001). Slavery in the History of Muslim Black Africa. Hurst & Company. pp. 33–. ISBN 978-1-85065-524-4. Retrieved 31 May 2012. 
  48. Afolabi, Funmilayo Juliana; Aina, Olabisi Idowu (2014-02-01). "Gender Differentials in Subjective Well-Being Among Religious Elderly Yoruba People in Southwest Nigeria". Ageing International 39 (2): 180–193. ISSN 0163-5158. doi:10.1007/s12126-014-9197-8. 
  49. Rapalus, Peter (1994). "Optimum Human Population About One-third of Present Number". Environmental Conservation 21 (2): 176–177. ISSN 0376-8929. doi:10.1017/s0376892900024668.  Unknown parameter |doi-access= ignored (help)
  50. [https://www.scielo.br/pdf/tem/v23n2/1980-542X-tem-23-02-00294.pdf Richard B. Allen: Ending the history of silence: reconstructing European Slave trading in the Indian Ocean], Revista Tempo Vol. 23 n. 2, Artigo 6, Mai/Ago. 2017
  51. Allen, Ending .. uk 296 f.
  52. Kusimba, Chapurukha M. (2004). "The African Archaeological Review". Archaeology of Slavery in East Africa. 21 (2): 59–88. doi:10.1023/b:aarr.0000030785.72144.4a. JSTOR 25130793. S2CID 161103875.
  53. [http://self.gutenberg.org/articles/Moresby_Treaty Moresby Treaty], tovuti ya Self Gutenberg, iliangaliwa Februari 2021
  54. Kusimba, Chapurukha M. (2004). "The African Archaeological Review". Archaeology of Slavery in East Africa 21 (2): 59–88. JSTOR 25130793. doi:10.1023/b:aarr.0000030785.72144.4a. 
  55. Carlson, Roy L. (2017-06-06). Insoll, Timothy, ed. "Figurines and Figural Art of the Northwest Coast". Oxford Handbooks Online. doi:10.1093/oxfordhb/9780199675616.013.017. 
  56. Suzuki, Hideaki (2012). "Enslaved Population and Indian Owners Along the East African Coast: Exploring the Rigby Manumission List, 1860–1861". History in Africa 39: 209–239. ISSN 0361-5413. doi:10.1353/hia.2012.0014. 
  57. Ana Lucia Araujo: Dahomey, Portugal and Bahia: King Adandozan and the Atlantic Slave Trade, Slavery & Abolition, Vol. 33, No. 1, March 2012, pp. 1–19]
  58. Bernard K. Freamon. Possessed by the Right Hand: The Problem of Slavery in Islamic Law and Muslim Cultures. Brill. p. 78. The “globalized” Indian Ocean trade in fact has substantially earlier, even pre-Islamic, global roots. These roots extend back to at least 2500 BCE, suggesting that the so-called “globalization” of the Indian Ocean trading phenomena, including slave trading, was in reality a development that was built upon the activities of pre-Islamic Middle Eastern empires, which activities were in turn inherited, appropriated, and improved upon by the Muslim empires that followed them, and then, after that, they were again appropriated, exploited, and improved upon by Western European interveners. 
  59. 59.0 59.1 Bernard K. Freamon. Possessed by the Right Hand: The Problem of Slavery in Islamic Law and Muslim Cultures. Brill. pp. 79–80. 
  60. 60.0 60.1 Bernard K. Freamon. Possessed by the Right Hand: The Problem of Slavery in Islamic Law and Muslim Cultures. Brill. pp. 82–83. 
  61. 61.0 61.1 Bernard K. Freamon. Possessed by the Right Hand: The Problem of Slavery in Islamic Law and Muslim Cultures. Brill. pp. 81–82. 
  62. Patrick Manning (1990). Slavery and African Life: Occidental, Oriental, and African Slave Trades. Cambridge University Press. p. 12. 
  63. Sarant, Louise (2018-12-04). "Ancient North African tools show hominins were apt butchers". Nature Middle East. ISSN 2042-6046. doi:10.1038/nmiddleeast.2018.153. 
  64. Waite, Diana S., author. (September 2019). The architecture of downtown Troy : an illustrated history. ISBN 978-1-4384-7475-5. OCLC 1118691930. 
  65. "Middle East Oil Trade, 2012 and 2013". World Oil Trade 36 (1): 155–175. 2014. ISSN 0950-1029. doi:10.1002/wot.47. 
  66. John Donnelly Fage; William Tordoff (December 2001). A History of Africa (4 ed.). Budapest: Routledge. p. 258. ISBN 978-0415252485. 
  67. Lodhi, Abdulaziz (2000). Oriental Influences in Swahili: a study in language and culture contacts. Acta Universitatis Gothoburgensis. p. 17. ISBN 978-9173463775. 
  68. Edward R. Tannenbaum, Guilford Dudley (1973). A History of World Civilizations. Wiley. p. 615. ISBN 978-0471844808. 
  69. Swahili Coast. .nationalgeographic.com (17 October 2002). Jalada kutoka ya awali juu ya 2007-12-06. Iliwekwa mnamo 2021-02-22.
  70. Curtin, Philip D. (1972). The Atlantic Slave Trade: A Census. University of Wisconsin Press. ISBN 978-0-299-05403-8. Retrieved 29 March 2013. 
  71. Trans-Atlantic Slave Trade. Emory University. Jalada kutoka ya awali juu ya 25 March 2013. Iliwekwa mnamo 29 March 2013.
  72. "Boswellin". Reactions Weekly 1795 (1): 71. 2020. ISSN 0114-9954. doi:10.1007/s40278-020-76092-y. 
  73. Marx, K. "Chapter Thirty-One: Genesis of the Industrial Capitalist", Das Kapital: Volume 1, 1867.

Kujisomea[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]