Utumizi mzuri wa dawa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Utumizi mzuri wa dawa (pia: uzingativu) katika taaluma ya uuguzi, inaelezea kiwango ambacho mgonjwa huzingatia ushauri wa daktari. Kwa kawaida, humaanisha uzingativu katika matumizi ya dawa, lakini pia ina maana ya matumizi ya vifaa vya matibabu kama vile stockings compression, utunzi wa jeraha sugu, mazoezi ya binafsi, au kuhudhuria ushauri au kozi nyingine za matibabu.

Muuguzi na mgonjwa wote huathiri utumizi mzuri wa dawa, na uhusiano mwema baina ya daktari na mgonjwa huathiri pakubwa katika kuboresha utumizi bora wa dawa, ingawa gharama kubwa za dawa pia huchangia pakubwa.

Kutozingatia utumizi bora wa dawa ni kikwazo kikubwa katika utoaji wa huduma bora ya afya. Makadirio ya Shirika la Afya Duniani yanaonyesha kwamba ni karibu 50% ya wagonjwa wanaougua magonjwa sugu wanaoishi katika nchi zilizoendelea hufuata mapendekezo ya matibabu. Haswa, viwango vya chini vya kuzingatia matibabu ya pumu, kisukari na Shinikizo la damu huchangia kwa kiwango fulani gharama na mzigo wa kiuchumi wa hali hiyo. Makadirio ya viwango vya uzingativu yaweza kuwa juu katika maandiko ya utabibu, kwani kiwango cha uzingativu huwa juu katika uundaji wa majaribio ya kliniki lakini hushuka katika "ulimwengu wa halisi". [1]

Vikwazo vikuu katika uzingativu wa dawa ni kama vile mfumo wa matibabu wa kisasa ulio na utaratibu, ukosefu wa "elimu ya afya" na ukosefu wa ufahamu wa faida za matibabu, matukio ya adhari za kando za dawa zisizojadiliwa, gharama ya madawa ya kuagizwa na daktari , na mawasiliano duni au ukosefu wa uaminifu baina ya mgonjwa na muuguzi au muhuduma wake wa afya. Juhudi za kuboresha utumiaji mzuri wa dawa zimelengwa katika kurahisisha ufungashaji dawa, kutoa kumbusho za dawa bora, kuboresha elimu ya wagonjwa,na kuweka vikwazo kwenye idadi ya dawa zinazoagizwa kwa wakati mmoja.

Istilahi[hariri | hariri chanzo]

Jumla ya nusu ya watu ambao mfumo wa utaratibu wa matibabu wameagiziwa,hawauzingatii ipasavyo. [2] Hadi hivi karibuni, ilijulikana kama "kutozingatia", ambayo wakati mwingine ilimaniisha kutofuata maagizo ya matibabu na ilitokana na tabia za kihuni au kupuuza maelekezo kwa makusudi. Leo, wataalamu wa afya hutumia kwa kawaida zaidi "uzingatifu wa mfumo ulio na utaratibu" kuliko "utumizi bora wa dawa", kwa sababu maneno haya hukisiwa kuwasilisha haswa sababu ambazo huwafanya wagonjwa hauri wa daktari.[3] Hata hivyo, istilahi kamili bado suala la mjadala. [4] [5] Katika baadhi ya matukio, upatano hutumika hasa kwa mgonjwa kuzingatia mfumo ulio na utaratibu wa matibabu ambao umeundwa kwa ushirikiano wake na daktari, na kuutofautisha na uaminifu, ambao ni mfumo ambao ni daktari pekee anayetoa utaratibu wa tiba.[6] Licha ya mjadala unaoendelea, uaminifu ndio neno linalopendelewa na Shirika la Afya Duniani, Shirika la Wafamasia wa Marekani na Taasisi ya Utafiti na Mtandao wa Afya ya Marekani.[7]

Upatano pia unahusu mpango wa Ufalme wa Muungano NHS wa kuhusisha mgonjwa katika mchakato wa kutibiwa ili kuboresha ukubalifu. [8] Katika muktadha huu, mgonjwa anajulishwa hali yao na matibabu yaliyoko. Hushirikiana na timu ya matibabu katika uamuzi utakaochukuliwa na kuwajibika kwa kufuatilia na kuripoti kwa timu hiyo. Uzingativu wa matibabu ni huboreshwa kwa:

 • Kupendekeza matibabu ambayo ni bora katika muktadha ulioko
 • Kuchagua matibabu yaliyo na kiwango kidogo cha chini ya athari au matatizo machache kwa ajili ya matumizi ya muda mrefu
 • Kuagizia idadi ya chini ya dawa mbalimbali, kwa mfano, kuagizia dozi moja ya kiua vijasumu ambayo inatibu maambukizi mawili kwa wakati mmoja (ingawa kuhatarisha kuchangia ukuaji wa usugu wakiua vijasumu)
 • Kurahisisha mfumo ulio na utaratibu wa kipimo cha dawa kwa kuchagua dawa tofauti au kutumia kipimo cha dawa kinacho tolewa kwa uwendelevu na kuhitaji maandalizi na vipimo cha chini wakati wa siku [9]
 • Kujadili athari zinazowezekana, na kama kuna umuhimu wa kuendelea kutumia dawa hizo bila kujali athari
 • Ushauri juu ya kupunguza au kukabiliana na madhara, kwa mfano, kama kuchukua dawa ukiwa na njaa au kama umeshiba.
 • Kujenga uaminifu ili wagonjwa wasiwe na hofu,aibu au hasira kama hawawezi kuchukua dawa pekee, na kuruhusu daktari kujaribu njia mbadala ya muhula bora

Athari za jamii[hariri | hariri chanzo]

Makadirio ya utafiti wa Shirika la Afya Ulimwengu yaonyesha kuwa ni 50% tu ya wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa sugu katika nchi zilizoendelea hufuata mapendekezo ya matibabu. [2] Hii inaweza kuathiri afya ya mgonjwa, na kuathiri jamii pana wakati inasababisha matatizo kutokana na magonjwa sugu, kusababisha maambukizi sugu, au bila kutibiwa, ugonjwa wa akili. Viwango vya utumiaji mzuri wa dawa wakati wa kisomo cha kufuatiliwa kwa karibu huwa kwa kawaida juu zaidi ikilinganishwa na hali halisia duniani. Kwa mfano, taarifa ya utafiti mmoja uliripoti 97% kufuata katika kiwango cha mwanzo wa matibabu na statins lakini 50% ya wagonjwa walikuwa bado wanafanya inavyotakikana baada ya miezi sita. [1]

Masuala ya utumizi mzuri wa dawa[hariri | hariri chanzo]

Viwango vya kuagiza dawa kwa daktari[hariri | hariri chanzo]

Ingawa mhuduma wa afya akikumbana na mgonjwa huweza kusababisha mgonjwa kuondoka na dawa kwa ajili ya ugonjwa, si wagonjwa wote watachukuwa dawa hiyo katika duka la dawa. Nchini Marekani, ni 20-30% ya maagizo ya dawa kutoka kwa daktari ambayo hujazwa katika duka la dawa. [10] [11] Kuna sababu nyingi zinazowafanya wagonjwa kutojaza maagizo ikiwa nipamoja na gharama ya dawa , mashaka haja ya dawa, au upendeleo kwa-huduma hatua binafsi kuliko dawa nyingine. Gharama ndio kizuizi kikuu kwa kufuata maagizo ya madawa. Utafiti wa kitaifa wa Marekani uliofanyiwa watu wazima ya 1,010 mwaka wa 2001 uligundua kuwa 22% walichagua kutojaza maagizo kwa sababu ya bei, ambayo ni sawa na kiwango cha jumla 20-30% ya maagizo ambayo huwa hayajazwi. [12]

Kumaliza tiba[hariri | hariri chanzo]

Mara baada ya kuanza, wagonjwa mara si haba hawafuati mfumo wa matibabu kama ilivyoagizwa, na mara nyingi kumaliza kozi ya tiba. [13] [3] Gharama na uelewaji mbaya wa maelekezo kwa ajili ya matibabu (inajulikana kama elimu ya afya ) ni vikwazo vikuu katika ukamilisho wa matibabu. Kama ilivyotajwa awali, Shirika la Afya Duniani (WHO) lina makadirio ya kwamba ni 50% tu ya watu ambao hukamilisha tiba ya ya muda mrefu kwa ajili ya matibabu ya muda mrefu illnesses as they were prescribed, which puts patient health at risk.[2]

Aina mbalimbali ya mbinu zimependekezwa ili kusaidia wagonjwa kukamilisha ya matibabu kama walivyoagizwa. Mbinu hizi ni pamoja na miundo zinazosaidia kurahisisha kukumbuka mfumo wa matibabu na kipimo na pia maandiko mbalimbali kwa ajili ya kuongeza uelewano na subira ya maelekezo. Kwa mfano, dawa wakati mwingine hupakiwa na mifumo ya kukumbusha siku na / au muda wa wiki wa kuchukua dawa. Kwa lengo la kusaidia uzingativu wa dawa na wagonjwa, shirika lisilo na kibiashara ( Healthcare Compliance Packaging Council of Europe/HCPC-Europe ) [2] Archived 19 Oktoba 2008 at the Wayback Machine.[58] ilianzishwa kati ya wanasekta wa dawa, sekta ya upakiaji na wawakilishi, wa mashirika ya wagonjwa wa Ulaya. Maudhui ya HCPC-Ulaya ni kusaidia na kuelimisha sekta ya afya katika uboreshaji wa ufuataji wa matumizi ya dawa na wagojwa kupitia upakiaji mzuri. Aina mbalimbali ya upakiaji zimeendelezwa na ushirikiano huu ili kusaidia katika kufuata maagizo ya dawa.

Kushindwa kukamilisha mfumo wa matibabu kama ilivyo agizwa ina athari mbaya ya afya duniani kote. [2] Mifano ya kiwango na matokeo ya kutozingatia mfumo wa matibabu kwa magonjwa kadha ni kama ifuatavyo:

 • Kutozingatia matumizi kwa Ugonjwa wa kisukari (98% katika Marekani) ni sababu kuu ya matatizo kuhusiana na ugonjwa wa kisukari yakiwa ni pamoja na uharibifu wa neva na kuharibika kwa figo.
 • Kutozingatia kwa Shinikizo la damu (93% nchini Marekani, 70% katika Uingereza) ni sababu kubwa ya mmambukizi ya ghafla ya moyo na kiharusi.
 • Kutozingatia kwa ugonjwa wa Pumu ni (28-70% duniani kote) huongeza hatari ya mashambulizi makali ya pumu yanayohitaji kulazwa hospaitalini.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. 1.0 1.1 "Patient Compliance with statins". Bandolier. 2004. http://medicine.ox.ac.uk/bandolier/booth/cardiac/patcomp.html. Retrieved 2010-09-20.
 2. 2.0 2.1 2.2 2.3 World Health Organization (2003). Adherence to Long-Term Therapies: Evidence for Action (PDF), Geneva: World Health Organisation. ISBN 92-4-154599-2. 
 3. 3.0 3.1 Ngoh LN (2009). "Health literacy: a barrier to pharmacist-patient communication and medication adherence". J Am Pharm Assoc (2003) 49 (5): e132–46; quiz e147–9. doi:10.1331/JAPhA.2009.07075 . PMID 19748861 .
 4. Osterberg L, Blaschke T (2005). "Adherence to Medication". N Engl J Med 353 (5): 487–97. doi:10.1056/NEJMra050100 . PMID 16079372 .
 5. Aronson JK (2007). "Compliance, concordance, adherence". Br J Clin Pharmacol 63 (4): 383–4. doi:10.1111/j.1365-2125.2007.02893.x . PMC 2203247 . PMID 17378797 .
 6. US NIH Office of Behavior and Social Sciences Research (2008). Framework for adherence research and translation: a blueprint for the next ten years. Jalada kutoka ya awali juu ya 2010-05-28. Iliwekwa mnamo 2010-09-20.
 7. Office of Behavior and Social Sciences Research. Adherence Research Network. U.S. National Institutes of Health. Jalada kutoka ya awali juu ya 2010-05-02. Iliwekwa mnamo 12 Mei 2010.
 8. Marinker and Shaw (15 Februari 2003). "Not to be taken as directed - Putting concordance for taking medicines into practice". BMJ 326 (7385): 348–9. doi:10.1136/bmj.326.7385.348 .
 9. "Dosing and compliance?". Bandolier 117: Figure 1. Novemba 2003. http://www.medicine.ox.ac.uk/bandolier/band117/b117-8.html. Retrieved 2010-09-20.
 10. Fischer MA, Stedman MR, Lii J, et al. (Aprili 2010). "Primary medication non-adherence: analysis of 195,930 electronic prescriptions". J Gen Intern Med 25 (4): 284–90. doi:10.1007/s11606-010-1253-9 . PMC 2842539 . PMID 20131023 .
 11. Norton M. (Reuters Health) Many patients may not fill their prescriptions (2010), [1] Accessed 12 Mei 2010
 12. "Out-of-pocket costs may be a substantial barrier to prescription drug compliance", Harris Interactive. Retrieved on 12 Mei 2010. Archived from the original on 2010-01-03. 
 13. Enhancing Patient Adherence: Proceedings of the Pinnacle Roundtable Discussion. APA Highlights Newsletter (Oktoba 2004). Jalada kutoka ya awali juu ya 2011-06-15. Iliwekwa mnamo 2021-12-29.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]