Utamaduni wa Burkina Faso

Utamaduni wa Burkina Faso uliopo katika ukanda wa Afrika Magharibi unajulikana pia kama utamaduni wa Burkinabè.
Vipengele viwili muhimu vya utamaduni wa Burkina Faso (zamani ikiitwa Volta ya Juu) ni umahiri wao wa kucheza ngoma na vinyago vya asili. Kinyago hutumiwa kwa ajili ya shughuli za kitamaduni za kafara kwa miungu na roho za wanyama vijijini. Ngoma za asili hutumika kuonesha hamu ya wanavijiji kupata baraka kutoka kwa mizimu.
Fasihi
[hariri | hariri chanzo]Fasihi ya Burkina Faso inatokana na masimulizi ya jadi kwa njia ya mdomo, ambapo bado yana nafasi kubwa mno nchini humo.[1] Mnamo mwaka 1934, wakati wa ukoloni wa Ufaransa, Dim-Dolobsom Ouedraogo alichapisha Maximes, pensées et devinettes mossi, kitabu kilichokusanya historia ya simulizi ya watu wa Mossi.[1] Baada ya uhuru miaka ya 1960, waandishi kama Nazi Boni na Roger Nikiema waliendeleza fasihi iliyoathiriwa na simulizi za kale.[2] Miaka ya 1960 pia ilishuhudia ongezeko la waandishi wa tamthilia.[1] Tangu miaka ya 1970, idadi ya waandishi imeongezeka zaidi nchini humo.[3]
Mashairi ya majibizano yamekuwa yakipata umaarufu mkubwa kupitia kazi za Malika Ouattara.
Tamthilia
[hariri | hariri chanzo]Tamthilia nchini Burkina Faso huunganisha uigizaji wa jadi wa Burkinabè na athari za kikoloni pamoja na juhudi za baada ya uhuru katika kuelimisha watu wa vijijini, na hivyo kuunda tamthilia ya kitaifa yenye upekee wake.
Mapishi
[hariri | hariri chanzo]Mapishi ya Burkina Faso yanaendana sana na sehemu kubwa ya mapishi ya Afrika Magharibi, yakiegemea zaidi kwenye vyakula vya mtama, uwele, mchele, mahindi, karanga, viazi, maharage, mihogo na bamia.[4]
Sanaa
[hariri | hariri chanzo]
Mbali na urithi tajiri wa sanaa ya jadi miongoni mwa makabila mbalimbali, kuna jamii kubwa ya wasanii, hasa katika mji mkuu Ouagadougou. Sehemu kubwa ya kazi za mikono huzalishwa kwa ajili ya sekta ya utalii. Tigoung Nonma ni shirika lililoanzishwa na wasanii wenye ulemavu kwa ajili ya kupata kipato endelevu kwa kuuza kazi zao.[5]
Filamu
[hariri | hariri chanzo]Jukwaa la Popular Theatre mjini Ouagadougou ni kiini cha matukio ya kijamii na kitamaduni. Ouagadougou pia ni kituo kikuu cha filamu za Kiafrika, na huandaa tamasha la filamu la kila mwaka lijulikanalo kama FESPACO, linalovuta washiriki wa kimataifa. Pia, eneo la Laongo limegeuzwa kuwa uwanja wa sanaa ya miamba ambapo wasanii kutoka duniani hualikwa kuchonga sanamu moja kwa moja kwenye mawe ya graniti.[6] Mtayarishaji maarufu Idrissa Ouedraogo anatokea hapa.
Dini
[hariri | hariri chanzo]Serikali ya Burkina Faso ilikadiria katika sensa ya 1996 kuwa asilimia 60 ya watu ni Waislamu, wengi wao wakiwa Sunni, pamoja na wachache wa Shia na Sufi wa Tijaniyah au Salafi.[7] Pia kuna wafuasi wa Uislamu wa Ahmadiyya. Takriban asilimia 24 hufuata dini za jadi za Kiafrika, asilimia 17 ni Wakatoliki, na asilimia 3 ni Waprotestanti.[7]
Kufikia mwaka 2019 ilikadiriwa Waislamu kuwa 63.8%, Wakristo kuwa 26.3% (Wakatoliki 20.1 na Waprotestanti 6.2%), huku wafuasi wa dini za jadi wamepungua hadi kuwa 9% tu.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- 1 2 3 Salhi, Kamal (1999). Francophone Voices. Intellect Books. uk. 37. ISBN 1-902454-03-0.
- ↑ Allan, Tuzyline Jita (1997). Women's Studies Quarterly: Teaching African Literatures in a Global Literary. Feminist Press. uk. 86. ISBN 1-55861-169-X.
- ↑ Marchais, Julien (9 Desemba 2006). Burkina Faso (kwa Kifaransa). Petit Futé. ku. 91–92. ISBN 2-7469-1601-0.
{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Oxfam's Cool Planet - Food in Burkina Faso". Oxfam. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-05-17. Iliwekwa mnamo 2008-05-21.
- ↑ Our partners in Burkina Faso Archived 2014-04-07 at the Wayback Machine
- ↑ Burkina Faso (2006b). Sculptures de Laongo Burkina Faso Retrieved 04/12/ 2006 from
- 1 2 International Religious Freedom Report 2007: Burkina Faso
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Art and oracle: African art and rituals of divination, an exhibition catalog from The Metropolitan Museum of Art (fully available online as PDF), which contains material on art from Burkina Faso