Upooza wa usingizini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Upooza wa usingizi ni hali ambayo huwapata baadhi ya watu wakati wa kuamka au kulala, ambapo fahamu za mtu zinakuwa zikifanya kazi lakini mtu huyo anakua amepooza kabisa. Hali hii inapompata, mtu anaweza kupatwa na maono ya ajabu, aidha kwa kusikia, kuhisi, au kuona vitu ambavyo havipo. Mara nyingi upooza wa usingizini huchukua dakika chache tu, zisizozidi tatu. Hali hiyo inaweza kutokea kwa wale walio na afya njema au walio na ugonjwa wa nakolepsia (kwa Kiingereza narcolepsy), au inaweza kutokea katika familia kutokana na mabadiliko maalum ya kijeni. Hali hiyo inaweza kuchochewa na kutopata usingizi wa kutosha ambao unashauriwa na wataalamu wa afya, msongo wa mawazo na ulevi.

Dalili[hariri | hariri chanzo]

Dalili kuu ya upooza wa usingizini ni kutoweza kusogea au kuzungumza wakati wa kuamka.

Kusikia sauti zisizo na uhalisia kama vile mivumo, kelele kama zile atoazo nyoka, kelele kama za king'ora huripotiwa na watu mbalimbali wanaokumbwa na upooza wa usingizini. Sauti zingine kama vile, minong'ono na mingurumo zinaweza kwa mtu mwenye upooza wa usingizini. Imegundulika pia kwamba mtu anaweza kuhisi shinikizo kwenye kifua chake na maumivu makali ya kichwa wakati wa anapata upooza kuwepowa usingizini. Dalili hizi kwa kawaida huambatana na hisia kali kama vile woga na hofu.

Upooza wa usingizini pia hujumuisha dalili kama, kushindwa kupumua vizuri, kuhisi uwepo wa viumbe vya ajabu katika chumba ulicholala, Watu wengine wanasimulia kuwa huwa wanapata hisia ya kuvutwa kwa nguvu kutoka kwenye kitanda na wengine hupata hisia ya kupaa angani.

Tamaduni[hariri | hariri chanzo]

Kwa hapa Tanzania, watu wengi husema, hali hii husababishwa na mambo ya kishirikina, kama pepo na mizimu. Hata hivyo, dalili kuu ya upooza wa usingizini (kupata maono ya ajabu) yanaonekana kuwepo ulimwenguni kote.

Kulingana na baadhi ya wanasayansi, maelezo ya kiutamaduni yanaweza kuwa sababu kuu katika kuchagiza upooza wa usingizini.

Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Upooza wa usingizini kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.