Upasuaji wa plastiki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Upasuaji wa kale nchini India wa kurekebisha pua kwenye gazeti la Gentleman's Magazine, 1794

Upasuaji wa plastiki ni aina maalum ya upasuaji unaojumuisha utengenezaji mpya, urekebishaji au ubadilishaji wa mwili wa binadamu. Upasuaji huu unaweza kuwekwa katika makundu makuu mawili. Kundi la kwanza ni upasuaji wa kutengeneza upya ambapo ni pamoja na upasuaji wa mkono, upasuaji wa uso na matibabu ya majeraha yanayotokana na kuchomwa na moto au tindikali. Aina nyingine ni upasuaji wa urembo.[1] Wakati aina ya kwanza kazi yake kubwa ni kurekebisha sehemu ya mwili au kuongeza ufanisi wake, aina ya pili dhumuni lake ni kuimarisha uonekano wa sehemu ya mwili. Aina hii ya pili ni maarufu sana kwenye nchi zilizoendelea na hasa miongoni mwa watu maarufu kwenye fani mbalimbali kama muziki, filamu, n.k.[2] Hata hivyo, aina zote hizi hutumika duniani kote.


Inaaminika matumizi ya neno "upasuaji wa plastiki" kwenye lugha ya Kiingereza ni mwaka 1598.[3] The surgical definition of "plastic" first appeared in 1839, preceding the modern "engineering material made from petroleum" sense of plastic (coined by Leo Baekeland in 1909) by 70 years.[4]

Historia[hariri | hariri chanzo]

Upasuaji wa plastiki ili kurekebisha pua iliyovunjika inaaminika kuwa ndio upasuaji wa kwanza wa aina hii unaotajwa kwenye Edwin Smith Papyrus[5], maandiko ya Misri ya Kale, moja ya maandiko ya kale kabisa ya utabibu duniani kati ya mwaka 3000 hadi 2500 KK.[6]. Upasuaji wa plastiki ulikuwa ukifanywa huko India toka mwaka 800 KK.[7] Sushruta ndiye mtabibu aliyechangia kwa kiasi kikubwa kwenye nyanja hii karne ya 6 kk.[8]

Kazi za udaktari za Sushruta na Charak, zilizokuwa zimeandikwa kwa lugha ya Sanskriti, zilitafsiriwa kwa lugha ya Kiaranu wakati wa utawala wa Abbasid mwaka 750 BK.[9] Tasfiri ya Kiarabu ilifika hadi Ulaya.[9] Nchini Italia, familia ya Branca[10] ya Sicily na Gaspare Tagliacozzi (Bologna) walijifunza mbinu za Sushruta.[9]

sanamu ya Sushruta, Baba wa Upasuaji wa Plastiki huko Haridwar, India

.

Madakitari wa kiingereza walisafiri hadi India ili kuona upasuaji wa plastiki ukifanywa kwa mtindo wa utabibu wa India. [11]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Plastic surgery. Citelighter. Jalada kutoka ya awali juu ya 2016-04-01. Iliwekwa mnamo 15 January 2013.
  2. Celebrities and plastic surgery.
  3. plastic. Oxford University Press. Iliwekwa mnamo 12 February 2015.
  4. Plastic. Etymonline. Iliwekwa mnamo 2 March 2014.
  5. Shiffman, Melvin (2012-09-05). Cosmetic Surgery: Art and Techniques. Springer. p. 20. ISBN 978-3-642-21837-8. 
  6. Mazzola, Ricardo F.; Mazzola, Isabella C. (2012-09-05). Plastic Surgery: Principles. Elsevier Health Sciences. pp. 11–12. ISBN 978-1-4557-1052-2. 
  7. MSN Encarta (2008). Plastic Surgery Archived 22 Septemba 2008 at the Wayback Machine.
  8. Dwivedi, Girish & Dwivedi, Shridhar (2007). History of Medicine: Sushruta – the Clinician – Teacher par Excellence Archived 10 Oktoba 2008 at the Wayback Machine.. National Informatics Centre (Government of India).
  9. 9.0 9.1 9.2 Lock, Stephen etc. (200ĞďéĠĊ1). The Oxford Illustrated Companion to Medicine. USA: Oxford University Press. ISBN 0-19-262950-6. (page 607)
  10. Maniglia, Anthony J (1989). "How I do It". The Laryngoscope 99 (8): 865–870. PMID 2666806. doi:10.1288/00005537-198908000-00017. 
  11. Lock, Stephen etc. (2001). The Oxford Illustrated Companion to Medicine. USA: Oxford University Press. ISBN 0-19-262950-6. (page 651)