Upandaji miti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya msitu wa kupandwa

Upandaji miti (Afforestation kwa lugha ya Kiingereza) ni upandaji wa mbegu au miti ili kutengeneza misitu katika eneo ambalo halijawahi kuwa na msitu hivi karibuni, au ambalo halijawahi kuwa na msitu kamwe. Reforestation kwa lugha hiyo ni upandaji miti au mbegu ili msitu urejeshwe baada ya kuondolewa katika eneo, kwa mfano wakati miti imekatwa kwa sababu za utengenezaji wa mbao.

Mataifa mengi yana uzoefu wa ukataji miti karne baada ya karne, na baadhi ya serikali na asasi zisizo za kiserikali hujihusisha moja kwa moja katika mipango ya upandaji miti ili kurejesha misitu na kusaidia kuhifadhi viumbehai tofauti.

Upandaji miti katika maeneo yenye udongo ulioharibiwa[hariri | hariri chanzo]

Katika baadhi ya maeneo, misitu huhitaji msaada kujiendelesha kwa sababu ya mambo ya mazingira. Kwa mfano, mara tu misitu inapoharibiwa katika mikuranga, maeneo hayo yaweza kukauka, kubaki kavu na kutokuwa karimu kwa upandaji upya wa miti. Sababu zingine ni pamoja na malisho ya mifugo yanayozidi maeneo ya malisho (overgrazing), hasa wanyama kama mbuzi na uvunaji uliyozidi wa rasilimali za misitu.

Haya yote pamoja yanaweza kusababisha jangwa na upotezaji wa udongo wa juu; bila udongo, misitu haiwezi kumea mpaka mchakato mrefu wa uumbaji wa udongo ukamilika - mmomonyoko wa udongo ukikosekana. Katika baadhi ya maeneo ya kitropiki, kuondolewa kwa misitu yaweza kusababisha duricrust au duripan ambayo husababisha kutoweza kwa udongo kunyonya maji na kutoweza kumea kwa mizizi. Katika maeneo mengi, upandaji miti ili kurejesha misitu haiwezekani kwa sababu watu wanatumia maeneo hayo. Katika maeneo mengine, kuvunjwa kwa duripans au duricrust ni muhimu, maji yafaa kumwagwa kwa makini mara kwa mara, na ulinzi maalum, kama vile zungusho au kuweka ugo, yaweza kuhitajika.

Maeneo ya Dunia[hariri | hariri chanzo]

Brazili[hariri | hariri chanzo]

Kwa sababu ya ukataji miti iliyozidi na inayoendelea katika msitu wa Amazon kwa miongo kadhaa iliyopita, juhudi ndogondogo za upandaji miti hazina umuhimu ikilinganishwa na ukubwa wa msitu wa mvua wa Amazon.

Uchina[hariri | hariri chanzo]

Uchina imekata miti ya misitu katika maeneo mengi ya kihistoria. Uchina ilifika kiwango ambacho utengenezaji wa mbao ulipungua kuliko viwango vya kihistoria.Hii ilitokana na uvunaji miti uliyopita kiasi cha umeaji. Ingawa imeweka malengo rasmi ya upandaji miti, malengo haya yaliwekwa kwa muda wa miaka 80 na hayakutimizwa kufikia mwaka wa 2008. Uchina inajaribu kurekebisha matatizo haya kwa miradi kama Green Wall of China, ambayo inalenga kupande upya misitu na kupunguza upanuzi wa jangwa la Gobi. Sheria iliyopitishwa mwaka wa 1981 inamhitaji kila raia mwenye umri zaidi ya miaka 11 kupanda mti mmoja angalau kwa mwaka. Kutokana na upandaji, Uchina sasa ina kiwango cha juu zaidi cha upandaji miti duniani kote. Mwaka wa 2008 Uchina ilikuwa imepanda miti katika eneo kubwa lenye mraba wa kilimita 47,000. Hata hivyo kwa wastani wa Uchina wa kupanda miti bado uko chini kuliko ule wastani wa kimataifa. Pendekezo kwa Uchina ni mfumo wa upandaji miti wa anga na upunguzaji wa mmomonyoko na pendekezo la mradi wa msitu wa Sahara pamoja na Seawater Greenhouse.

Ulaya[hariri | hariri chanzo]

Ulaya imekata miti ya misitu katika maeneo mengi ya kihistoria. Umoja wa Ulaya (EU) imekuwa ikiwalipa wakulima kupanda miti tangu mwaka wa 1990, kutoa misaada ya kubadilisha makonde au mashamba ukipenda ziwe misitu tena na malipo kwa ajili ya usimamizi wa misitu. Kati ya miaka ya 1993 na 1997, sera za EU za upandaji miti ziliwezesha upandaji miti katika ardhi yenye mraba wa kilomita 5,000 ambayo misitu yake ilikuwa imekatwa. Mpango wa pili uliyofanyika kati ya miaka ya 2000 na 2006, ulisaidia upandaji miti zaidi katika ardhi yenye mraba wa kilomita 1000 (takwimu sahihi hazipatikani kwa sasa). Mpango wa tatu ulianza mwaka wa 2007.

Nchini Polandi, programu ya Kitaifa ya upandaji miti ilianzishwa na serikali baada ya Vita kuu ya pili ya Dunia, wakati jumla ya eneo la misitu ilipungua hadi asilimia 20, mpakani mwa nchi hiyo. Programu hiyo ilisaidia maeneo ya misitu ya Polandi kuongezeka miaka baada ya miaka, na tarehe 31 Desemba 2006, misitu ilifunika asilimia 29 ya nchi hiyo(tazama: misitu ya Polandi). Imepangwa kuwa kufikia mwaka wa 2050, misitu itajaza asilimia 33 ya Polandi.

Irani[hariri | hariri chanzo]

Iran inadhaniwa kama moja ya maeneo madogo ya misitu duniani kwani nchi hii ina asilimia saba pekee ya misitu. Thamana hii ilipungua kwa takriban hekta milioni sita ya mistu bikira, iliyojumuisha miti kama mwaloni, almond na pistacio. Kutokana na vichepechepe vya udongo, ni vigumu kupanda miti kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na maeneo mengine yenye udongo wenye rutuba zaidi na mawe chache na hali za mikurunga. Hivyo basi , upandaji miti zaidi hufanywa na spishi za miti zisizo za sehemu hiyo, ambazo hupelekea uharibifu wa mazingira kwa wanyama na mimea, na kusababisha hasara kwa kasi ya viumbe tofautitofauti vilivyo hai.

Angalia pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Andrea Cattaneo (2002) Jämvikt mellan Maendeleo ya Kilimo na ukataji miti katika Brazil Amazon, Int Sera ya Chakula Res Inst IFPRI, 146 kurasa ISBN 0896291308
  • Gerrit W. Heil, Bart Muys na Karin Hansen (2007) Environmental ATHARI Afforestation Kaskazini-Magharibi Ulaya, Springer, 320 kurasa ISBN 1402045670
  • Gerald A. McBeath na Tse-Kang Leng (2006) Utawala wa Biodiversity Conservation katika China na Taiwan, Edward Elgar Publishing, kurasa 242 ISBN 1843768100
  • Halldorsson G., Oddsdottir, ES na Sigurdsson BD (2008) AFFORNORD ATHARI Afforestation tarehe Ecosystems, Landscape na Maendeleo Vijijini, TemaNord 2008:562, 120 kurasa ISBN 978-92-893-1718-4
  • Halldorsson G., Oddsdottir, ES na Eggertsson O (2007) ATHARI Afforestation tarehe Ecosystems, Landscape na Maendeleo Vijijini. AFFORNORD kesi ya mkutano, Reykholt, Island, 18-22 Juni 2005, TemaNord 2007:508, 343pages ISBN 978-92-893-1443-5
  • John A. Stanturf na Palle Madsen (2004) Restauration of Boreal joto Forests, CRC Press, kurasa 569 ISBN 1566706351
  • EO Wilson (2002) The Future of Life, Vintage ISBN 0-679-76811-4