Nenda kwa yaliyomo

Umarsioni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Umarsioni ulikuwa aina ya Ukristo[1] iliyoenea sana katika karne za kwanza za Kanisa[2] ikifundisha uwepo wa miungu wawili, mmoja mwema na wa kweli (yule wa Injili), mwingine mbaya (yule Muumba wa Agano la Kale)[1][2][3]. Jina lilitokana na lile la mwanzilishi wake, Marsioni, mtoto wa askofu wa Sinope, Ponto, leo nchini Uturuki. Alipohamia Roma katikati ya karne ya 2, alifundisha na kuandika hayo[4], akikataa vitabu vyote vya Biblia isipokuwa Injili ya Luka aliyoifupisha na barua 10 za Mtume Paulo[5][6][7]. Maandishi yake yamepotea, lakini yanajulikana kupitia yale ya Tertuliani na Mababu wa Kanisa waliompinga mapema[8].

  1. 1 2 Ehrman, Bart D. (2005) [2003]. "At Polar Ends of the Spectrum: Early Christian Ebionites and Marcionites". Lost Christianities: The Battles for Scripture and the Faiths We Never Knew. Oxford: Oxford University Press. ku. 95–112. doi:10.1017/s0009640700110273. ISBN 978-0-19-518249-1. LCCN 2003053097. S2CID 152458823.
  2. 1 2 Dunn, James D. G. (2016). ""The Apostle of the Heretics": Paul, Valentinus, and Marcion". Katika Porter, Stanley E.; Yoon, David (whr.). Paul and Gnosis. Pauline Studies. Juz. la 9. Leiden and Boston: Brill Publishers. ku. 105–118. doi:10.1163/9789004316690_008. ISBN 978-90-04-31668-3. LCCN 2016009435. S2CID 171394481.
  3. BeDuhn, Jason (2015). "The New Marcion" (PDF). Forum. 3 (Fall 2015): 165. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2019-05-25. Iliwekwa mnamo 2023-12-23.
  4. History of the Christian Church, Volume II: Ante-Nicene Christianity. A.D. 100–325. Marcion and his School by PHILIP SCHAFF
  5. Ehrman, Bart D. (2005). Misquoting Jesus: The Story Behind Who Changed the Bible and Why. New York: HarperOne. uk. 33. ISBN 978-0-06-085951-0.
  6. "Eusebius' Church History". Ccel.org. 2005-06-01. Iliwekwa mnamo 2013-01-25.
  7. Ehrman, Bart D. Misquoting Jesus. ku. 33–34.
  8. Ehrman, Bart D. Misquoting Jesus. uk. 163.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Umarsioni kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.