Ukaushaji wa chakula
Ukaushaji wa chakula ni mbinu ya kuhifadhi chakula ambapo chakula hukaushwa(kuondolewa unyevu/maji au kukauka kabisa). Ukaushaji wa chakula huzuia ukuaji wa bakteria, chachu na ukungu kwa kuondoa maji. Njia ya ukaushaji imekuwa ikitumika kwa wingi kwa madhumuni haya tangu nyakati za kale; matumizi ya mwanzo kabisa yanajulikana kuwa ni mwaka 12,000 K.K na wakazi wa maeneo ya Asia na Mashariki ya Kati ya leo[1]. Kwa kawaida, maji huondolewa kupitia uvukizaji kwa kutumia mbinu kama vile kukausha kwa hewa, kukausha kwa jua, kuvutwa kwa moshi au kukausha kwa upepo, ingawa siku hizi ukaushaji wa chakula unaweza kutumia mashine za umeme au kukaushwa kwa njia ya kugandishwa ambako kunaweza kuharakisha mchakato wa ukaukausha na kuhakikisha matokeo yenye uthabiti zaidi.[2]
Aina za vyakula
[hariri | hariri chanzo]Aina nyingi za vyakula zinaweza kuandaliwa kwa njia ya kukaushwa. Nyama imekuwa na nafasi kubwa ya kihistoria. Kwa karne nyingi, sehemu kubwa ya lishe ya Wazungu ilitegemea samaki wa kukaushwa aina ya cod—ujulikanao kama samaki wa chumvi (salt cod), bacalhau (uliotiwa chumvi), au stockfish (usiotiwa chumvi). Ulikuwa chanzo kikuu cha protini kwa watumwa waliokuwa kwenye mashamba ya miwa ya India Magharibi, na ulikuwa ni nguvu kubwa ya kiuchumi katika biashara ya pembetatu. Samaki waliokaushwa, hasa cod au haddock, wanaojulikana kama Harðfiskur, ni kitoweo nchini Iceland, ikiwa nyama ya paa wa kaskazini (reindeer) iliyokaushwa ni chakula cha kitamaduni cha watu wa Sámi. Nyama zilizokaushwa ni pamoja na prosciutto (Parma ham), bresaola, biltong na beef jerky.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Historical Origins of Food Preservation". Ilihifadhiwa 15 Oktoba 2011 kwenye Wayback Machine. Accessed June 2011.
- ↑ Rahman, M. Shafiur, mhr. (2007). Handbook of Food Preservation (kwa Kiingereza) (tol. la 2nd). Boca Raton: CRC Press. ISBN 9781420017373.