Nenda kwa yaliyomo

Uhuru wa Kenya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jamhuri ya Kenya

Makala hii imepangwa kwa mfululizo:
Siasa na serikali ya
Kenya



Nchi zingine · Atlasi

Uhuru wa Kenya ulipatikana tarehe 12 Desemba 1963 baada ya harakati za kijeshi na za kisiasa dhidi ya ukoloni wa Ufalme wa Muungano.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Katika mwisho wa karne ya 19, eneo la leo la Jamhuri ya Kenya liliingia chini ya ukoloni wa Waingereza, kwanza kupitia Kampuni ya Kifalme ya Afrika Mashariki ya Kiingereza na baadaye kama koloni rasmi.

Ujenzi wa Reli ya Uganda na kuanzishwa kwa kilimo cha walowezi vilibadilisha kwa kiasi kikubwa hali ya kijamii na ya kiuchumi, mara nyingi kwa hasara ya wenyeji.

Wakikuyu waliamua kuanzisha chama chao cha kwanza cha harakati za kisiasa ambacho kiliitwa Young Kikuyu Association. Kiongozi wake alikuwa Harry Thuku. Sababu nyingine ya kuanzishwa kwa chama hiki ni kwamba Waafrika hawakuwa na mwakilishi katika siasa. Chama hicho kilianzishwa mwaka 1921. Baadaye jina la chama lilibadilishwa likawa Kenya African Union (KAU), shirika la kitaifa lililodai kuingia katika nchi iliyomilikiwa na walowezi. Mwaka 1947, urais wa chama hiki ulitolewa kwa Jomo Kenyatta.

Upinzani dhidi ya utawala wa kikoloni uliongezeka kwa miongo kadhaa, na kufikia kilele chake katika harakati za kupigania uhuru kwa silaha zilizofanywa na kundi la Mau Mau katika miaka ya 1950. Kuanzia Oktoba 1952 mpaka Desemba 1959, Kenya ilikuwa katika hali ya hatari kufuatia mapigano ya Mau Mau dhidi ya Uingereza.

Baada ya juhudi hizo kushindikana na baada ya miaka mingine ya mapambano ya kisiasa zaidi, ambapo Waingereza walitaka kutenga wahalifu na wafuasi wao, uchaguzi wa kwanza wa moja kwa moja wa Waafrika katika bunge ulifanywa mwaka 1957. Licha ya Waingereza kuwa na matumaini ya kuwapa wapinzani Waafrika mamlaka "ya wastani" zaidi, ilikuwa Kenya African National Union (KANU) ya Jomo Kenyatta, wa kabila la Wakikuyu na mfungwa wa zamani, ambayo iliunda serikali muda mfupi kabla ya Kenya kupata uhuru.

Hatimaye Kenya ilipata uhuru kutoka kwa Uingereza tarehe 12 Desemba 1963, ambapo Jomo Kenyatta alikuwa waziri mkuu wa kwanza chini ya malkia Elizabeth II.

Mwaka mmoja baadaye, Kenya ikawa jamhuri na Jomo Kenyatta akawa Rais wa kwanza.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Uhuru wa Kenya kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.