Uhandisi wa Kikemia
Uhandisi wa kikemia ni uwanja wa uhandisi unaohusika na kubuni, kusanifu na kutekeleza michakato, ambapo mabadiliko ya kikemia au ya kimaumbile ya maunzi hubadilishwa kutoka hali ghafi hadi hali timilifu. Mhandisi wa kikemia hutumia ujuzi wa kemia, fizikia, hisabati, bayolojia na sayansi ya uzalishaji kubuni michakato na kuendesha viwanda[1][2].
Nadharia
[hariri | hariri chanzo]Operesheni za kitengo
[hariri | hariri chanzo]Katika kuchakata malighafi, vitendo vinavyofanywa kubadilisha maumbile ya maunzi katika mchakato huitwa operesheni za kitengo. Operesheni hizi zinajumuisha:
Michakato ya kitengo
[hariri | hariri chanzo]Kitendo ambacho kitabadilisha maumbile ya kikemikali ya maunzi yanapochakatwa huitwa mchakato wa kitengo. Vitendo hivi hufanyika katika atomu na vinaweza kusaidiwa na operesheni za kitengo[3]. Kwa mfano, katika mchakato wa kuzalisha sabuni, mmemenyuko wa hidrolisisi hufanyika katika halijoto 80 - 120 °C katika kinu kinachochukucha. Mchakato wa kitengo ni hidrolisisi, na operesheni za kitengo ni uhamisho wa joto (kutoka mvuke hadi mchanganyiko ulio ndani ya kinu) na kuchukucha.
Usanifishaji wa vinu
[hariri | hariri chanzo]Inahusisha kusanifisha muundo wa kinu, mhandisi akizingatia mwendojoto, mwendo kikemikali, umakanika wa giligili, uhamisho wa joto na uhamisho wa tungamo[4]. Parameta hizi huathiri jinsi mmemenyuko utafanyika, pamoja na kiwango na ubora wa mazao yatakayozalishwa kutoka mchakato wa kinu.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ McCabe, Warren L.; Smith, Julian Cleveland; Harriott, Peter (2005), "Chapter 1: Definitions and Principles", Unit operations of chemical engineering. Hauptbd., McGraw-Hill's chemical engineering series (tol. la 7. ed), McGraw-Hill Higher Education, ISBN 978-0-07-284823-6
{{citation}}:|access-date=requires|url=(help);|edition=has extra text (help) - ↑ Shreve, R. Norris; Brink, Joseph A. (1977). "Chapter 1: Objectives". Chemical process industries (tol. la 4th ed). New York: McGraw-Hill. ISBN 978-0-07-057145-7.
{{cite book}}:|edition=has extra text (help) - ↑ Shreve, R. Norris; Brink, Joseph A. (1977). "Chapter 2: UNIT PROCESSES AND UNIT Operations". Chemical process industries (tol. la 4th ed). New York: McGraw-Hill. ISBN 978-0-07-057145-7.
{{cite book}}:|edition=has extra text (help) - ↑ Levenspiel, Octave (1999), Chemical reaction engineering. Hauptbd. (tol. la 3. ed), Wiley, ku. 1–5, ISBN 978-0-471-25424-9
{{citation}}:|access-date=requires|url=(help);|edition=has extra text (help)