Nenda kwa yaliyomo

Ugonjwa wa Poland

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ugonjwa wa Poland ni kasoro ya kuzaliwa[1] ambayo huathiri maendeleo ya misuli upande mmoja wa mwili, hasa katika kifua na mkono[2]. Hali hii hujitokeza zaidi kwa wanaume na mara nyingi huathiri upande wa kulia wa mwili. Katika baadhi ya visa, huambatana pia na utando wa vidole (sindaktili) katika mkono huohuo.[3]

Chanzo halisi cha ugonjwa huu haujulikani[3]. Hata hivyo kuna nadharia inayodai kuwa unachangiwa na kukatizwa kwa mtiririko wa damu wakati wa maendeleo ya kiinitete[4] katika wakati wa awali wa ujauzito.

Kwa kawaida, ugonjwa huo haurithiwi na bado hakuna jeni zilizothibitishwa kuhusika moja kwa moja. Utambuzi hufanyika kwa kuzingatia dalili za kimwili. Mara nyingi, watu walio na hali hii hubaki bila kutambuliwa, na baadhi yao huigundua tu wanapofikia umri wa kubalehe.[5][6]

Matibabu ya ugonjwa wa Poland hutegemea ukali wake, na yanaweza kujumuisha upasuaji wa kurekebisha kasoro zilizoonekana[7]. Hali hii huathiri takriban mtoto 1 kati ya 20,000 aliyezaliwa huku wanaume wakiathirika mara mbili zaidi ya wanawake[8]. Imepata jina lake kutoka kwa daktari wa upasuaji wa Kiingereza, Sir Alfred Poland ambaye aliieleza kwa mara ya kwanza akiwa mwanafunzi mwaka wa 1841.[9][10] Katika visa vingi, wagonjwa huonyesha pia kasoro nyingine za kifua kama vile kifua kilichozama ndani (pectus excavatum) au hali ya kupinda (pectus carinatum) kwa mfupa wa kifua kueleka nje pamoja na mbavu. Hivyo basi, tathmini ya kitaalamu inahitajika ili kubaini athari zake kwa mfumo wa upumuaji na moyo, na inapobidi, kufanyika upasuaji wa kurekebisha umbo la kifua.

Ishara na dalili

[hariri | hariri chanzo]

Ugonjwa huo hujitokeza kwa njia mbalimbali na dalili zake hutofautiana kulingana na mtu na kiwango cha athari, Kwa kawaida, huathiri upande mmoja (unilaterali). Dalili zinaweza kugawanywa katika makundi yafuatayo:[7][5]

1.Dalili za misuli na matiti.

Ukosefu au maendeleo duni ya pectoralis major, hasa kichwa cha sehemu inayoshikilia kwenye mfupa wa kifua (sternokostali).

Kwa wanawake: kutokuwepo kwa matiti au chuchu upande mmoja (amastia).

Kwa wanaume: kifua upande mmoja huonekana kimezama au kimepungua ukubwa.

2.Dalili za mkono na vidole.

  • Sindaktili: vidole vilivyoshikana kwa utando.
  • Right hand of patient with typical features of Poland Syndrome
    Mkono wa kulia wa mgonjwa aliye na simbrakidakti katika ugonjwa wa Poland
    Brakidaktili: vidole vifupi kupita kawaida.
  • Oligodaktili: upungufu wa idadi ya vidole.
  • Upungufu au kasoro katika mifupa ya mkono kama radius, ulna au humerus.
  • Mikono isiyo sawa kwa ukubwa au nguvu (asimetri ya viungo vya juu).

3. Dalili za ngozi na nywele.

  • Ukosefu wa nywele za kwapa upande ulioathirika.
  • Mikunjo ya ngozi isiyo ya kawaida, mfano kreasi ya simiani.

4. Dalili za mfumo wa mifupa na kifua.

  • Male presents with absent left pectoral muscle
    Mwanaume aliye na ugonjwa wa Poland akionyesha kutokuwepo kifua cha kushoto
    Kasoro ya mbavu, mara nyingine mbavu huwepo lakini hazijaungana vizuri na mfupa wa kifua.
  • Pectus excavatum au pectus carinatum.
  • Scapula (mfupa wa bega) inaweza kuwa na maumbile yasiyo ya kawaida.

5. Dalili nyingine (mara chache).

  • Moyo kuwa upande wa kulia wa kifua.
  • Kasoro za mfumo wa nyongo na ini.
  • Kichwa kidogo.
  • Kasoro za figo na mfumo wa mkojo (ureteric anomaly)[11].
  • Utoboaji wa kiwambo cha kupumulia (diaphramatic hernia).

Visababishi

[hariri | hariri chanzo]

Chanzo halisi cha ugonjwa wa Poland hakijulikani. Hata hivyo, nadharia inayokubalika zaidi ni kwamba hali hii husababishwa na ukatizwaji wa mtiririko wa damu kwa kiinitete (embryo) katika kipindi cha maendeleo ya mapema ya ujauzito hasa takriban siku ya 46 baada ya utungwaji mimba.[12]

Pia, inaaminika kuwa ateri za subklaviani, ambazo hupitia chini ya mfupa wa kola (claviculum), hukoma kusambaza damu kwa tisha za kiinitete ambazo baadaye hutengeneza ukuta wa kifua na mkono. Kukosekana kwa usambazaji huu wa damu husababisha ukosefu wa maendeleo ya kawaida ya misuli ya kifua na viungo vya mkono upande mmoja wa mwili.

Tofauti katika eneo na ukubwa wa ukatizwaji wa damu zinaweza kueleza kwa nini dalili za ugonjwa huu hutofautiana kati ya mtu na mtu. Pia, tafiti zimependekeza kuwa kasoro katika muundo wa kiinitete unaoitwa “apical ectodermal ridge” ambao ni muhimu katika kuongoza ukuaji wa viungo vya mikono na miguu inaweza kueleza kwa nini baadhi ya wagonjwa pia hupata matatizo ya vidole na mikono[13]. Vilevile, kuna mashaka kuwa athari za azingira wakati wa ujauzito kama vile magonjwa ya mama hasa kisukari cha ujauzito huweza kuchangia hatari ya mtoto kupata ugonjwa wa Poland.[5]

Utambuzi

[hariri | hariri chanzo]

Ugonjwa huu kwa kawaida hutambuliwa wakati wa kuzaliwa, kwa kuzingatia sifa za kimwili zinazoonekana wazi. Katika baadhi ya visa ambapo hali ni kiwango cha chini, utambuzi unaweza kuchelewa hadi wakati wa kubalehe, ambapo tofauti katika ukuaji wa kifua au mikono huanza kuonekana kwa urahisi zaidi.[7][14]

CT scan inayoonyesha ukosefu wa Pectoralis
Mammogram showing absense of pectoralis major muscle on left side
Mammogram inayoonyesha kutokuwepo kwa miduli kuu ysa Pectorslid Majo upande wa kushotor na upande wa kulia ni sawa

Tathmini ya kinana ya kitaaluma inahitajika kutambua ugonjwa huu. Utambuzi unategemea uchunguzi wa kliniki pamoja na vipimo vya picha, ambavyo husaidia kuelewa kiwango na eneo lililoathirika. Uchunguzi wa kimwili hubaini kama kuna tofauti kwa ukubwa wa upande mmoja wa kifua, ukosefu au udhaifu wa misuli ya pectoralis major na kasoro za mikono au vidole ka vile sindaktili (vidole vilivyoshikana) au brakidaktili (vidole vifupi).

Vipimo vya picha kama X-Ray hutumika kuonyesha kasoro za mfupa wa kifua na mkono na MRI hutoa picha za kina zinazosaidia kuchunguza maendeleo ya misuli na hali ya viungo vilivyoathirika. Ingawa ugonjwa huu kwa kawaida hauhusiani moja kwa moja na urithi wa kijeni, ushauri wa kinasaba[15]unaweza kupendekezwa endapo kuna dalili nyingine za kasoro za kuzaliwa au hata historia ya matatizo ya kimaumbile katika familia. Hii husaidia kutathmini ikiwa kuna hatari ya kurudia kwa hali hii katika ujauzito wa baadaye[5].

Matibabu

[hariri | hariri chanzo]

Matibabu huhusisha mchanganyiko wa upasuaji na mbinu zingine kama dawa. Matibabu hulenga dalili maalum zinazoonekana kwa kila mgonjwa mmoja mmoja. Kwa kuwa athari zake hutofautiana kwa kiwango na eneo, matibabu mara nyingi huhitaji uratibu wa wataalamu mbalimbali wa afya.[16][5]

1. Urekebishaji kwa upasuaji.

Upasuaji wa plastiki mara nyingi hupendekezwa ili kujenga upya ukuta wa kifua na tishu za matiti hasa kwa wanawake, ili kuboresha mwonekano wa mwili na utendakazi wa eneo lililoathirika. Katika baadhi ya visa, upasuaji unaweza kufanywa pia kurekebisha kasoro za mifupa ya mikono au vidole[17].

2. Dawa bandia na vifaa mbadala.

Katika visa vya kasoro za vidole, vifaa vya bandia vinaweza kutumika ili kuboresha uhamaji.

3. Tiba ya kimwili.

Ili kusaidia kuimarisha nguvu, kuboresha harakati na kuzuia matatizo ya muda mrefu, tiba ya kimwili inaweza kuagizwa. Hii ni muhimu kuboresha maisha.

4.Msaada wa kisaikolojia 

Ushauri wa kisaikolojia inaweza kusaidia wagonjwa hasa vijana kukabiliana na changamoto za kisaikolojia kama vile hali ya kuonekana tofauti na kujithamini na vile kuishi na hali hiyo.

Matibabu mengine kwa kawaida ni ya kusaidia na kupunguza dalili.[5]

Visa vilivyoripotiwa katika Afrika

[hariri | hariri chanzo]

Uhakiki wa maandiko ya kisayansi unaonyesha kuwa ni visa viwili pekee vya ugonjwa wa Poland ambavyo vimeripotiwa kutoka Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara. Kisa cha kwanza kilichothibitishwa kilitokea Rwanda mwaka wa 2005 na kuhusisha mvulana mwenye umri wa miaka 12 aliyekuwa na viungo vya mwili, vidole, mbavu na moyo wake vilikuwa vya kawaida kupungua kwa umbo la kifua upande wa kushoto tangu utotoni. Uchunguzi wa kimwili ulionyesha kutokuwepo kwa misuli ya pectoralis major upande huo na kutokuwepo kwa mkunjo wa kwapa. Hata hivyo, misuli ya pectorlais minor na serratus anterior zilikuwepo na zilikuwa kawaida. Mtoto huyo alikuwa na ukuaji wa kawaida na uwezo wa kiakili wa kawaida pia. Hakukuwa na historia ya ugonjwa huu katika familia yake. Kisa hicho kinaonyesha jinsi ugonjwa wa Poland ulivyo nadra kuripotiwa katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.[18]

  1. Mwilaria, Reuben; Kobia, John; Musyimi, Dorcas (2024-10-24). "Mitindo ya Uwasilishaji wa Suala la Afya Katika Matini Teule za Fasihi ya Kiswahili ya Watoto". East African Journal of Swahili Studies. 7 (1): 492–503. doi:10.37284/jammk.7.1.2337. ISSN 2707-3475.
  2. Hoskins, Amber (2022-10-02). "Genetic and Rare Diseases Information Center (GARD)". Medical Reference Services Quarterly (kwa Kiingereza). 41 (4): 389–394. doi:10.1080/02763869.2022.2131143. ISSN 0276-3869.
  3. 1 2 "Genetics Home Reference". Reference Reviews (kwa Kiingereza). 18 (3). Abigail Leah Plumb: 38–39. 2004-04-01. doi:10.1108/09504120410528234. ISSN 0950-4125.{{cite journal}}: CS1 maint: others (link)
  4. 1 2 3 4 5 6 Ugonjwa wa Poland: Dalili, Utambuzi na Matibabu (no date). Available at: https://www.medicoverhospitals.in/sw/diseases/poland-syndrome/ (Accessed: 11 July 2025).
  5. "Kasoro za Misuli - Matatizo ya Afya ya Watoto". Toleo la Mtumiaji la Mwongozo wa MSD (in Swahili). Retrieved 2025-07-09.
  6. 1 2 3 "Poland syndrome". Genetic and Rare Diseases Information Center (GARD) – an NCATS Program. 2016. Retrieved 16 October 2018.
  7. Genetic and Rare Diseases Information Center (GARD) – an NCATS Program. 2016.
  8. "Poland Syndrome - Symptoms, Causes, Treatment | NORD". rarediseases.org (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2025-07-11.
  9. Weinzweig, Jeffrey (2010). Plastic Surgery Secrets Plus E-Book. Elsevier Health Sciences. p. 774. ISBN 978-0-323-08590-8.
  10. Ectopic Ureter: Dalili, Sababu na Matibabu (no date). Available at: https://www.medicoverhospitals.in/sw/diseases/ectopic-ureter/ (Accessed: 11 July 2025).
  11. Poullin P.; Toussirot E.; Schiano A.; Serratrice G. (1992). "[Complete and dissociated forms of Poland's syndrome (5 cases)]". Rev Rhum Mal Osteoartic. 59 (2): 114–20. PMID 1604222.
  12. "Poland syndrome: MedlinePlus Genetics". medlineplus.gov (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-07-11.
  13. Tafti, D. and Cecava, N.D. (2025) ‘Poland Syndrome’, in StatPearls. Treasure Island (FL): StatPearls Publishing. Available at: http://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK532259/ (Accessed: 11 July 2025).
  14. RoleCatcher.com (no date) Mwongozo wa Mahojiano: Ushauri Juu ya Magonjwa ya Jenetiki kabla ya Kuzaa. Available at: https://rolecatcher.com/sw/miongozo-ya-mahojiano/mwongozo-wa-ujuzi/ujuzi-mgumu/mawasiliano-ushirikiano-na-ubunifu/ushauri-na-ushauri/ushauri-juu-ya-magonjwa-ya-kinasaba-kabla-ya-kuzaa/ (Accessed: 11 July 2025).
  15. "Poland Syndrome - Symptoms, Causes, Treatment | NORD". rarediseases.org (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2025-07-11.
  16. "Cosmetic surgery – Poland Syndrome". Medical Solutions Barcelona (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2025-07-11.
  17. Gashegu, J., Byiringiro, J. C., Nyundo, M., Uwineza, A., & Mutesa, L. (2009). Poland’s Syndrome: A Case Report. East and Central African Journal of Surgery, 14(2), 112–114. Retrieved from http://www.bioline.org.br/