Nenda kwa yaliyomo

Ugonjwa wa Charcot-Marie-Tooth

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ugonjwa wa charcot
Ukosefu wa tishu za misuli unaosababishwa na ugonjwa wa Charcot. Mgonjwa aliye na udhaifu wa neva husababisha hali iitwayo.

Ugonjwa wa Charcot-Marie-Tooth ni moja ya magonjwa ya kurithi. Mtu aliye na ugonjwa huu hukosa tishu za musuli na hisia ya kugusa sehemu mbalimbali za mwili wake. Hujulikana kama ugonjwa wa Charcot kutokana na jina la Jean-Martin Charcot, mwanasayansi wa neva wa Ufaransa ambaye kwa mara ya kwanza aliielezea kuhusu ugonjwa huu mwaka wa 1869.

Ugonjwa wa Charcot-Marie-Tooth ni katika kikundi cha magonjwa ya kurithi yanayosababishwa na mabadiliko ya kijeni yanayoathiri neva za pembeni, yaani neva zinazounganisha ubongo na uti wa mgongo na sehemu nyingine za mwili. Ugonjwa huo huanza kuathiri misuli ya miguu, kisha polepole huenea hadi viungo vingine. Wagonjwa hupoteza hisia kadhaa kamza za tetemeko, maumivu na joto.[1] Hata kama baadhi ya watu hupata dalili zisizoathiri maisha yao kwa kiasi kikubwa, wengine huathiriwa sana. Kwa mafano, baadhi ya wagonjwa hupatwa na matatizo ya kutokwa na jasho. Ingawa hakuna tiba kamili, kuna matibabu kama vile tiba ya viungo (fisiotherapi), upasuaji wa mifupa yanayoweza kudhibiti dalili na kuboresha maisha ya mgonjwa.[2]

Ugonjwa huu husababishwa na mabadiliko katika zaidi ya jeni[3] mia moja (100). Mabadiliko haya hasa huathiri nyuzi za neva (aksoni) zilizofunikwa ndani ya matabaka ya tishu yenye mafuta. Matabaka huitwa myelini.

Kazi ya myelini ni kupitisha ishra za umeme kwa haraka na usahihi. Myelini kinapoharibiwa neva haziwezi kupitisha ishara za umeme.[4] iIdadi ya visa vya magonjwa kinasemekana kuwa takribani watu 40 kati ya 100,000. Visa hivi hujitokezea sana sana wakati wa utoto au ujana. Ingawa ugonjwa huu upo barani Afrika bado kuna uhaba wa taaarifa. Utafiti mwingi umefanyika Afrika Kaskazini.[5]

Ishara na dalili

[hariri | hariri chanzo]

Dalili za ugonjwa huu huanza mara nyingi utotoni au wakati wa ujana, lakini kwa baadhi ya wagonjwa kisa kwanza cha ugonjwa huu huweza kujitokeza kwa utu uzima. Kiwango cah ukali na namna ugonjwa hujitokeza hutofautiana kati ya watu na hata ndani ya familia moja.

Dalili za kwanza ni kama ugumu kutembea, unaosababishwa na udhaifu wa misuli ya miguu na nyayo. Udhaifu wa neva husababisha hali iitwayo (footdrop).[6] Yaani mtu hupata ugumu kuinua nyayo na hujipata akitembea akiinua magoti juu zaid ya kawaida. Miongoni za dalili zingine za kawaida ni kuwa na upinde mkubwa wa nyayo (pes cavus) au vidole vya miguu kupinda kama nyundo (hammertoe). Hali hizi huongeza udhaifu na maumivu. Zaidi ya hayo, mgonjwa hupotea hisia ikiwemo kufa ganzi, kuwashwa au kuhisi joto sana kwenye miguu na mikono. Hali hii ni hatari kwani mgonjwa huweza kujeruhiwa bila kugunduliwa. Pia kupoteza hisia kwa mkono husabbaisha kufanya kazi ndogo kama kushika kalamu ngumu.[7]

Maumivu ni kawaida kwa wagonjwa na husababishwa na uchovu wa misuli na mabadilikoya mifupa. Maumivu haya yanaweza kudhibitiwa kwa kutumia dawa za kutuliza maumivu au kupewa magongo kusaidia wagonjwa kutemebea.

Hata hivyo, kuishi na ugonjwa huu is wa kutishia maisha kwa sababu ni ugonjwa unoendelea taratibu na pia kiwango cha ulemavu ni tofauti kwa kila mtu. Aina ya jeni iliyoathirika ina mchango mkubwa kwa jinsi dalili zinavyojitokeza. Baadhi ya watu huwa na maumivu ya neva (neuropathic pain) ambayo yanaweza bado kuwa kiwango tofauti. Aina ya CMT1 umejulikana kujaza mafuta kwenye misuli ya miguu badala ya ongezeko halisi. Hali hii huitwa (pseudohipertrofi)[8][9]

Ugonjwa huu husababishwa na kurithi neva za pembeni kutokana na mabadiliko ya vinasaba yaliyoharibu protini muhimu zinzazohakikisha muundo na kazi ya ganda la myelini. Protini hizi pamoja ni ; PMP22 (peripheral myelin protein 22), P0 (protein zero), connexin 32 na periaxin. Aidha, mabadiliko katika protini zinazosababisha usalama wa aksoni, kama Nf-L (neurofilament light chain), DNM2 (dynamin 2) na nyinginezo husababisha aina ya CMT inayoathiri aksoni. Aksoni bado huweza kuharibika kwa njia nyingine kutokana na mabadiliko yanayoathiri seli za Schwann (seli zinazozalisha myelini), hali inayozidisha ugonjwa. Hatimaye njia ya maendeleo ya ugonjwa (patogenesis) inahusisha uharibifu wa michakato ndani ya seli. ikiwemo kazi ya mitokondria, utengenezaji, uainishaji na usafirishaji wa protini.[10]

Aina za ugonjwa wa Charcot-Marie-Tooth

[hariri | hariri chanzo]

Ugonjwa huu huweza kusababishwa na mabadiliko katika vinasaba mbalimbali. Hadi sasa, jeni mengi yamhushishwa na kwa hivyo kuna aina tofauti za CMT, jambo linaloonyesha ugumu na utofauti wa msingi wa kijenetiki.[11]

Aina nyingi za CMT hurithiwa kwa njia ya dominanti autosomali.[12]Kwa sababu hii, CMT hugawanywa katika aina kuu kadhaa zikiwemo CMT1, CMT2, CMT4, CMTx, na aina zingine kulingana na jinsi ya kurithi na kama uharibifu upo kwa gamba la myelini au katika aksoni yenyewe.

  • CMT1 huhusisha upotevu wa myelini na mara nyingi husababishwa na jeni ya PMP22
  • CMT2 huathiri zaidi aksoni na sana sana husababishwa na mabadiliko katika jeni kama MFN2 au NEFL
  • Aina nyingine za X-linked yaani hirithiwa kupitia kromosomu X.[13] na zile zinzazorithiwa kwa jinisi ya resessivi autosomali kama CMT4 hufuatana na dalili kama kupoteza hisia kwa miguu mapema.

Kila aina kati ya hizi hugawanywa zaidi katika aina ndogo kulingana na mahususi liliopatwa na mabadiliko na pia kulingana na hali ya mgonjwa. Uainishaji huu huelekeza utambuzi, utabiri wa maendeleo na hata tiba zinazolenga vinasaba (targeted therapy).[14]

Utambuzi

[hariri | hariri chanzo]

Utambuzi huhusisha mchanganyiko wa historia ya familia na vipimo vya aina tofauti vya uchunguzi. Vipimo ndivyo haya:

  • Uchunguzi wa mwendo wa msukumo wa neva (nerve conduction study)-kupima haraka ya umeme inayopita neva
  • Uchunguzi wa sampuli ya neva (biopsi ya neva)
  • Vipimo vya kijenetiki kuthibitisha ugonjwa wa CMT na kutofautisha aina gani na kuongoza maamuzi ya matibabu.[15]

Daktari pia hutafuta dalili za CMT kama; udhaifu wa misuli katika mikono, miguu, viganja na nyayo, kupungua kawa refleksi au uwezo wa kuhisi (sensory loss). Watu walio na aina ya CMT1 wanaweza kuwa na neva zilizovimba na huonekana kupitia kwenye ngozi (hypertrophic nerve). Hali hii huthibitishwa na unene wa ganda la myelini linaozunguka neva.[16] Hata hivyo, dalili hizi pekee hazitoshi kuthibitisha ugonjwa na huhitaji kuonekana na daktari wa neurojia (neurologist) kufanya uchunguzi wa kina.

Matibabu

[hariri | hariri chanzo]
Kifaa cha 'Ankle Foot Orthosis' kinachotumika kusaidia kifundo cha mguu na nyayo. Husaidia kuinua miguu na kurahihisha kutembea.
Kifaa cha 'Ankle Foot Orthosis' ambacho hutumiwa na wagonjwa walioathiriwa na ugonjwa wa Charcot-Marie Tooth.

Hakuna tiba ya moja kwa moja ya ugojwa huu lakini dalili zake zinaweza kudhibitiwa kuboresha maisha ya mgonjwa. Tiba ya kimwili kama programu ya mazoezi huweza kusaidia kudumisha nguvu ya misuli na kuboresha usawa na kusaidia kutembea. Vifaa vya kusaidia mifupa kama "ankle-foot orthosis" huweza rekebisha tatizo la husababisha hali iitwayo. Katika baadhi ya visa vya hali mbaya, upasuaji wa uingiliaji wa mifupa huweza imarisha viungo. Maumivu huweza kupunguzwa na dawa za maumivu ya neva (neuropathic pain) kama gabapentinoidi na "serotonin noreoeniphrine reuptake inhibitor".[7][17]

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Ugonjwa wa Charcot-Marie-Tooth uligunduliwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 1886 na wanasayansi watatu: Jean-Martin Charcot (1825–1893)[18] pamoja na msaidizi wake Pierre Marie,[19] na daktari wa Kiingereza Howard Henry Tooth (1856–1925)[20]. Katika chapisho lao la awali lililoitwa “Concerning a Special Form of Progressive Muscular Atrophy” (yaani, “Kuhusu Aina Maalum ya Kudhoofika kwa Misuli Kunakoendelea”), Charcot na Marie walieleza kuwa visa vinavyofanana na hivyo vilikuwa tayari vimeripotiwa katika maandiko ya kitabibu. [21]

Picha la wanasayansi
Jean-Martin Charcot

Uchunguzi wao ulieleza kuhusu ugonjwa wa neva wa kurithi, unaojulikana kwa kudhoofika kwa misuli taratibu na kupungua kwa hisia, hasa kwenye mikono na miguu. Ugunduzi huu muhimu uliuwezesha CMT kutambulika kama ugonjwa tofauti wa neva, ukitofautishwa na magonjwa mengine kama vile dystrofia ya misuli. Kadri miaka ilivyopita, maendeleo katika taaluma ya jenetiki ya neva yamewezesha kugunduliwa kwa mabadiliko mbalimbali ya kijeni yanayochangia ugonjwa huu, hivyo kuboresha uelewa wa chanzo chake na aina zake. [22]

Picha la wansayasi
Pierre Marie Charcot

Charcot pia alibaini kuwa maelezo ya awali kuhusu ugonjwa huu hayakuwa ya kina, kwani akaunti nyingi zilizokuwepo zilitaja tu kwamba Charcot-Marie-Tooth ni ugonjwa wa kurithi. Kwa msingi huo, aliona ni muhimu kutoa maelezo ya kina ili ugonjwa huu upewe uzito unaostahili katika taaluma ya tiba. [23]

Mnamo mwaka wa 2010, ugonjwa wa CMT ulikuwa miongoni mwa magonjwa ya kwanza ambayo chanzo chake halisi kilibainika kwa kutumia teknolojia ya usomaji wa jeni nzima ya binadamu (whole-genome sequencing). Wanasayansi wa Shirika la Charcot–Marie–Tooth Association (CMTA) waligundua uwepo wa mabadiliko mawili katika jeni ya SH3TC2, ambayo tayari ilikuwa inajulikana kuhusishwa na CMT. Ili kuelewa vyema namna ugonjwa huu unavyorithiwa, watafiti walilinganisha jenomu ya mgonjwa aliyeathirika na ile ya wazazi wake pamoja na ndugu zake saba—baadhi yao wakiwa na dalili za ugonjwa, wengine wakiwa hawana.

Uchunguzi huo ulibaini kuwa kila mzazi alikuwa na nakala moja ya kawaida na moja iliyobadilika ya jeni hiyo, na walikuwa na dalili hafifu au hawakuwa na dalili kabisa. Hata hivyo, watoto waliorithi nakala mbili zenye mabadiliko walionyesha dalili kamili za ugonjwa wa CMT.[24]

  1. "Ugonjwa wa Charcot-Marie-Tooth - Matatizo ya Ubongo, Uti wa Mgongo, na Mishipa". Toleo la Mtumiaji la Mwongozo wa MSD. Iliwekwa mnamo 2025-06-14.
  2. "Charcot-Marie-Tooth Disease | National Institute of Neurological Disorders and Stroke". www.ninds.nih.gov (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-06-14.
  3. "Vidokezo vya Haraka:Jeni na kromosomu". Toleo la Mtumiaji la Mwongozo wa MSD. Iliwekwa mnamo 2025-06-14.
  4. "Ugonjwa wa Charcot-Marie-Tooth - Matatizo ya Ubongo, Uti wa Mgongo, na Mishipa". Toleo la Mtumiaji la Mwongozo wa MSD. Iliwekwa mnamo 2025-06-14.
  5. Yalcouyé, A. et al. (2022) ‘Current profile of Charcot-Marie-Tooth disease in Africa: A systematic review’, Journal of the peripheral nervous system: JPNS, 27 (2), pp. 100–112. Available at: https://doi.org/10.1111/jns.12489.
  6. "Signs and Symptoms of Charcot-Marie-Tooth Disease (CMT) - Diseases". Muscular Dystrophy Association (kwa Kiingereza). 2015-12-17. Iliwekwa mnamo 2025-06-16.
  7. 7.0 7.1 Ugonjwa wa Charcot-Marie-Tooth: Dalili, Sababu, na Matibabu. Available at: https://www.medicoverhospitals.in/sw/diseases/charcotmarietooth-disease (accessed: 16 June 2025).
  8. Krampitz DE, Wolfe GI, Fleckenstein JL, Barohn RJ (Novemba 1998). "Charcot-Marie-Tooth disease type 1A presenting as calf hypertrophy and muscle cramps". Neurology. 51 (5): 1508–1509. doi:10.1212/WNL.51.5.1508. PMID 9818900
  9. Smith TW, Bhawan J, Keller RB, Degirolami U (July 1980). "Charcot-Marie-Tooth Disease Associated with Hypertrophic Neuropathy: A Neuropathologic Study of Two Cases". Journal of Neuropathology and Experimental Neurology. 39 (4): 420–440. doi:10.1097/00005072-198007000-00003. PMID 6260904.
  10. Niemann A, Berger P, Suter U (2006). "Pathomechanisms of mutant proteins in Charcot-Marie-Tooth disease". Neuromolecular Medicine. 8 (1–2): 217–242. doi:10.1385/nmm:8:1-2:217 (inactive 12 April 2025). hdl:20.500.11850/422903. ISSN 1535-1084. PMID 16775378.
  11. Hoyle JC, Isfort MC, Roggenbuck J, Arnold WD (2015). "The genetics of Charcot-Marie-Tooth disease: current trends and future implications for diagnosis and management". The Application of Clinical Genetics. 8: 235–243. doi:10.2147/TACG.S69969. PMC 4621202. PMID 26527893.
  12. "Ugonjwa wa Charcot-Marie-Tooth - Matatizo ya Ubongo, Uti wa Mgongo, na Mishipa". Toleo la Mtumiaji la Mwongozo wa MSD. Iliwekwa mnamo 2025-06-16.
  13. https://www.msdmanuals.com/sw/home/quick-facts-children-s-health-issues/
  14. Niemann A, Berger P, Suter U (2006). "Pathomechanisms of mutant proteins in Charcot-Marie-Tooth disease". Neuromolecular Medicine. 8 (1–2): 217–242. doi:10.1385/nmm:8:1-2:217 (inactive 12 April 2025). hdl:20.500.11850/422903. ISSN 1535-1084. PMID 16775378
  15. Ugonjwa wa Charcot-Marie-Tooth: Dalili, Sababu, na Matibabu. Available at: https://www.medicoverhospitals.in/sw/diseases/charcotmarietooth-disease (Accessed: 16 June 2025).
  16. "Charcot-Marie-Tooth Disease | National Institute of Neurological Disorders and Stroke". www.ninds.nih.gov (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-06-16.
  17. "Managing Neuropathic Pain". Charcot–Marie–Tooth Association (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2025-06-16.
  18. Kumar DR, Aslinia F, Yale SH, Mazza JJ (2011-03-01). "Jean-Martin Charcot: The Father of Neurology". Clinical Medicine & Research. 9 (1): 46–49. doi:10.3121/cmr.2009.883. ISSN 1539-4182. PMC 3064755. PMID 20739583
  19. Kumar DR, Aslinia F, Yale SH, Mazza JJ (2011-03-01). "Jean-Martin Charcot: The Father of Neurology". Clinical Medicine & Research. 9 (1): 46–49. doi:10.3121/cmr.2009.883. ISSN 1539-4182. PMC 3064755. PMID 20739583.
  20. Pearce JM (2000-01-01). "Howard Henry Tooth (1856–1925)". Journal of Neurology. 247 (1): 3–4. doi:10.1007/s004150050002. ISSN 1432-1459. PMID 10701890
  21. Brody IA, Wilkins RH (1967-11-01). "Charcot-Marie-Tooth Disease". Archives of Neurology. 17 (5): 552–553. doi:10.1001/archneur.1967.00470290106015. ISSN 0003-9942. PMID 4293350.
  22. Kazamel M, Boes CJ (2015-04-01). "Charcot Marie Tooth disease (CMT): historical perspectives and evolution". Journal of Neurology. 262 (4): 801–805. doi:10.1007/s00415-014-7490-9. ISSN 1432-1459. PMID 25201224.
  23. Brody IA, Wilkins RH (1967-11-01). "Charcot-Marie-Tooth Disease". Archives of Neurology. 17 (5): 552–553. doi:10.1001/archneur.1967.00470290106015. ISSN 0003-9942. PMID 4293350.
  24. Lupski JR, Reid JG, Gonzaga-Jauregui C, Deiros DR, Chen DC, Nazareth L, et al. (2010-04-01). "Whole-Genome Sequencing in a Patient with Charcot–Marie–Tooth Neuropathy". New England Journal of Medicine. 362 (13): 1181–1191. doi:10.1056/NEJMoa0908094. ISSN 0028-4793. PMC 4036802. PMID 20220177.