Nenda kwa yaliyomo

Siasa za Kenya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Ufisadi nchini Kenya)
Uchaguzi wa 2022 thibitisho la ukabila nchini kenya

Kenya ni nchi ya demokrasia ya urais ambapo utawala wake unafuata mfumo wa mgawanyo wa madaraka kati ya serikali kuu na serikali za kaunti kulingana na Katiba ya 2010. Ingawa taifa limepiga hatua katika demokrasia, bado linakumbwa na changamoto kama migogoro ya uchaguzi, vurugu za baada ya uchaguzi, ufisadi, na ukabila wa kisiasa. [1]

Siasa za Kenya kwa kiasi kikubwa zinaendeshwa na ushindani wa kikabila kati ya jamii za Mlima Kenya (hasa Wakikuyu na Wathagichu) dhidi ya Waluo, huku makundi mengine kama Wakalenjin, Waluhya, na Wakamba yakicheza nafasi muhimu kulingana na miungano ya kisiasa. Historia ya Kenya imejawa na mapambano kati ya watawala wa jadi wa Mlima Kenya na wapinzani wakuu wa kisiasa kutoka Nyanza, hali inayochochea migawanyiko ya kisiasa na mvutano wa mara kwa mara katika uchaguzi.

Mjadala wa kumng’oa madarakani Naibu Rais Rigathi Gachagua ulianza kuibuka kufikia mwaka wa 2024, ukichochewa na migawanyiko ya ndani ya muungano wa Kenya Kwanza, mvutano wa mamlaka ndani ya Mlima Kenya, na tofauti kati yake na Rais William Ruto. Baadhi ya viongozi wa kisiasa walidokeza uwezekano wa bunge kuanzisha mchakato wa kumwondoa Gachagua kupitia kura ya kutokuwa na imani naye, ingawa suala hilo lilizua hisia mseto ndani ya chama tawala.

Vyama na Miungano

[hariri | hariri chanzo]

Kenya ina historia ya vyama vya kisiasa vinavyobadilika mara kwa mara, ambapo vyama huungana, kugawanyika, au kubadilishwa kabla ya uchaguzi. Mfumo wa vyama vingi vya siasa ulirejeshwa mwaka 1992, baada ya kipindi cha utawala wa chama kimoja cha KANU (1969-1991). Tangu wakati huo, siasa za Kenya zimekuwa zikizunguka kati ya muungano wa vyama vya tawala na vyama vya upinzani, mara nyingi yakiongozwa na viongozi wenye ushawishi wa kikabila.

Vyama na Miungano Mikubwa (Kufikia Uchaguzi wa 2022)

[hariri | hariri chanzo]

1. Kenya Kwanza Alliance (KKA) – Inayoongozwa na Rais William Ruto, muungano huu unajumuisha vyama vya:

  • United Democratic Alliance (UDA) – Chama kikubwa cha muungano huu.
  • Amani National Congress (ANC)
  • Forum for the Restoration of Democracy–Kenya (FORD-Kenya)
  • 2. Azimio la Umoja–One Kenya Coalition – Inayoongozwa na Raila Odinga, muungano huu unajumuisha:
  • Orange Democratic Movement (ODM)
  • Jubilee Party – Chama kilichokuwa madarakani chini ya Uhuru Kenyatta.
  • Wiper Democratic Movement

Vyama vya kisiasa vya Kenya mara nyingi huzingatia ushawishi wa kikabila badala ya sera za maendeleo, na wanasiasa wengi hubadili miungano yao kulingana na maslahi ya kisiasa badala ya misingi ya kiitikadi.

Ukabila ni kipengele kikubwa katika siasa za Kenya, ambapo kura nyingi huamuliwa kwa misingi ya ushirikiano wa kikabila badala ya itikadi za kisiasa. Migawanyiko mikubwa ya kisiasa nchini Kenya mara nyingi huzingatia uhasama wa kihistoria kati ya GEMA(Wakikuyu, Waembu, Wameru) kutoka Mlima Kenya dhidi ya (Waluo, Luhya, Kalenjin) kutoka Nyanza.[2]

Historia ya Ukabila wa Kisiasa

[hariri | hariri chanzo]

Kabla ya Ukoloni jamii au kabila za kenya ziliishi bila migogoro mikubwa, Wakikuyu , Waembu na Wameru walikuwa Wakulima katika mlima kenya. Wamasai na Samburu walikuwa wafugaji, Waluhya, Waluo na Wakisii walikuwa wavuvi na Waswahili walikuwa wafanya biashara. Utawala wa Kikoloni (1895-1963) ulileta migawanyiko katika kabila kupitia mkakati wa "gawa na tawala" . Baada ya Uhuru (1963), Rais Jomo Kenyatta aliendeleza sera za ukabila na kupendelea jamii za Mlima kenya

Wakikuyu wamekuwa na ushawishi mkubwa katika siasa za Kenya, wakiwa na marais watatu kati ya watano wa kwanza wa nchi hii:

  • Jomo Kenyatta (1963–1978)
  • Mwai Kibaki (2002–2013)
  • Uhuru Kenyatta (2013–2022)

Upinzani wa Waluo: Waluo, wakiongozwa na wanasiasa kama Jaramogi Oginga Odinga na Raila Odinga, mara nyingi wamekuwa mstari wa mbele kupinga kile wanachokiita "ukiritimba wa kisiasa wa Wakikuyu".

Ushawishi wa Kalenjin: Wakati wa utawala wa Daniel arap Moi (1978-2002), jamii ya Kalenjin ilikuwa na ushawishi mkubwa katika serikali, lakini hali hii ilibadilika baada ya Moi kuondoka madarakani.

Athari za Ukabila Katika Siasa

[hariri | hariri chanzo]
  • Kugawanyika kwa kura: Jamii tofauti hupigia kura wagombea wao wa kikabila, badala ya kuzingatia sera za maendeleo.
  • Vurugu za kisiasa: Mfano mkubwa ni vurugu za baada ya uchaguzi wa 2007-2008, ambapo watu zaidi ya 1,100 waliuawa na maelfu kufurushwa makwao kutokana na mgogoro wa uchaguzi kati ya Kibaki (Mwakilishi wa Mlima Kenya) na Raila Odinga (Mwakilishi wa Waluo).

Ubadhirifu wa mali ya umma: Viongozi wa kikabila huajiri watu wa jamii zao katika serikali, wakihakikisha kuwa maeneo yao yanapewa upendeleo wa kimaendeleo.

Uchaguzi

[hariri | hariri chanzo]

Kenya hufanya uchaguzi mkuu kila baada ya miaka mitano, lakini uchaguzi huu mara nyingi umekuwa na dosari nyingi, ikiwa ni pamoja na madai ya wizi wa kura, ghasia, na mizozo ya kisheria.

Migogoro Maarufu ya Uchaguzi

[hariri | hariri chanzo]
  • Uchaguzi wa 2007:

Ghasia za uchaguzi wa Kenya wa 2007 zilianza baada ya Mwai Kibaki kutangazwa mshindi huku kukiwa na madai ya udanganyifu, zikisababisha mapigano ya kikabila yaliyoua zaidi ya watu 1,000 na kuwafurusha 600,000. Jamii pinzani zilishambuliana, polisi walitumia nguvu, na biashara ziliharibiwa. Makubaliano ya kugawana madaraka yaliyosimamiwa na Kofi Annan yalimaliza mgogoro huo lakini yakafichua mgawanyiko mkubwa wa kikabila na kisiasa.

  • Uchaguzi wa 2017: Mahakama ya Juu ya Kenya ilibatilisha ushindi wa Uhuru Kenyatta kutokana na ukiukwaji wa sheria za uchaguzi, na uchaguzi wa marudio ulisusiwa na upinzani.
  • Uchaguzi wa 2022: William Ruto alitangazwa mshindi dhidi ya Raila Odinga kwa kura chache, hali iliyozua maandamano kutoka kwa wafuasi wa upinzani.

Rushwa imekuwa tatizo sugu katika siasa za Kenya, ambapo viongozi wengi wa serikali wamehusika katika kashfa za ufisadi. Miongoni mwa kashfa kubwa za kisiasa ni pamoja na:

  • Goldenberg Scandal (1990s) – Iliigharimu Kenya zaidi ya $600 milioni.
  • Anglo Leasing Scandal (2000s) – Ilihusisha mikataba ya uongo ya serikali.
  • Huduma ya Vijana kwa Taifa (NYS) Scandal (2015, 2018) – Fedha za maendeleo ya vijana ziliporwa na viongozi wa serikali.
  1. Britannica. "Politics of Kenya" (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-02-23.
  2. "Ukabila nchini Kenya" (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-02-23.