Uchaguzi wa Rais wa Marekani, 1972

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Uchaguzi wa Rais wa Marekani, mwaka wa 1972 ulikuwa wa 47 katika historia ya Marekani. Ukafanywa Jumanne tarehe 7 Novemba. Upande wa "Republican Party", Rais Richard Nixon (pamoja na kaimu wake Spiro Agnew) alimshinda mgombea wa "Democratic Party" George McGovern (pamoja na kaimu wake Sargent Shriver).

Matokeo[hariri | hariri chanzo]

Nixon akapata kura 520, na McGovern 17 wakati mchaguzi mmoja kutoka Virginia alimpigia kura John Hospers badala ya Nixon. Ramani yaonyesha kura kwa kila jimbo.