Nenda kwa yaliyomo

Tyrese Gibson

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tyrese Gibson

Amezaliwa Decemba 30, 1978
Los Angeles, California, Marekani
Majina mengine Black-Ty, Tyrese
Kazi yake Mwanamuziki na mwigizaji

Tyrese Darnell Gibson (alizaliwa Desemba 30, 1978)[1][2] ni mwimbaji wa R&B[3] na mwigizaji kutoka Los Angeles, California, Marekani. Alisaini mkataba na RCA Records mwaka 1998, na akaachia wimbo wake wa kwanza, Nobody Else,” mnamo Agosti mwaka huo. Wimbo huo uliingia kwenye nafasi za juu 40 za chati ya Billboard Hot 100 na ukatangulia albamu yake ya kwanza iliyopewa jina lake mwenyewe (1998), ambayo ilipata cheti cha platinamu kutoka Recording Industry Association of America (RIAA) na ikazaa wimbo wake wa pili uliokuwa kwenye nafasi za juu 40, Sweet Lady.”

Albamu yake ya pili na ya tatu, 2000 Watts (2001) na I Wanna Go There (2002), zote zilipata ithibati ya dhahabu kutoka RIAA. Albamu ya pili kati ya hizo iliongozwa na wimbo “How You Gonna Act Like That”, ambao ulifika nafasi ya saba kwenye chati ya Billboard Hot 100 na bado unabaki kuwa wimbo wake uliopata nafasi ya juu zaidi kwenye chati. Albamu yake ya nne, Alter Ego (2006), ilijaribu muziki wa kurapu(kufokafoka) chini ya jina la kisanii Black Ty, huku albamu yake ya tano, Open Invitation (2011), ikipata uteuzi wa Tuzo ya Grammy kwa Albamu Bora ya R&B katika Tuzo za Grammy za 55. Albamu ya sita ya Gibson, Black Rose (2015), ilianza ikiwa juu kabisa kwenye chati ya Billboard 200.

Gibson ameweza kuuza zaidi ya nakala milioni 4 za nyimbo na albamu nchini Marekani, na amewahi kuteuliwa mara sita kwa Tuzo za Grammy.[4]

Gibson alipata nafasi yake ya kwanza kama mwigizaji mkuu katika filamu ya ukuaji wa maisha ya mitaani Baby Boy (2001) iliyoongozwa na John Singleton, na alipata umaarufu mkubwa kwa kuigiza kama Roman Pearce katika filamu saba za mfululizo wa Fast & Furious (2003–sasa) pamoja na Robert Epps katika filamu tatu za kwanza za mfululizo wa filamu ya Transformers (2007–2011). Gibson alikutana tena na Singleton katika filamu ya kusisimua Four Brothers (2005). Pia alionekana katika filamu ya vichekesho Ride Along 2 (2016) na filamu ya shujaa wa kubuni Morbius (2022).

Maisha ya Awali

[hariri | hariri chanzo]

Gibson alizaliwa na kulelewa huko Watts, Los Angeles, California.[5] Mama yake, Priscilla Murray Gibson (jina la kuzaliwa Durham), alimlea yeye pamoja na ndugu zake watatu wakubwa pekee yake baada ya baba yao, Tyrone Gibson kuondoka.[6] Alipokuwa akikua huko Watts katika Mtaa wa 113 mwishoni mwa miaka ya 1980, Gibson alikumbana na mazingira ya magenge ya kihalifu, huku baadhi ya marafiki zake wa utotoni wakijiunga na genge la Crips. Kwenye tawasifu wake, Tyrese alisema kuwa ni jambazi mmoja mkubwa aliyejulikana kwa jina la “Dirtbike Fred” aliyemhimiza achague njia tofauti maishani. Baadaye alihitimu masomo yake katika Shule ya Sekondari ya Locke mwaka 1996.

Kazi ya Muziki

[hariri | hariri chanzo]

Kazi ya muziki ya Gibson ilianza alipofanya majaribio ya kuonekana katika tangazo la Coca-Cola kwa ushauri wa mwalimu wake wa muziki wa shule ya sekondari. Kuonekana kwake katika tangazo la Coca-Cola [7]mwaka 1994, akiimba kauli “Always Coca-Cola”, kulimpatia umaarufu mkubwa zaidi. Pia kulimfungulia milango ya kuonekana katika matangazo mengine, ikiwemo ya Guess na Tommy Hilfiger.

Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani wa Marekani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tyrese Gibson kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  1. https://californiabirthindex.org/birth/tyrese_darnell_gibson_born_1978_13629289
  2. https://web.archive.org/web/20151003005943/http://www.tvguide.com/celebrities/tyrese-gibson/bio/177762/
  3. https://www.allmusic.com/artist/tyrese-mn0000807361
  4. https://www.billboard.com/pro/tgts-three-kings-debuts-at-no-1-on-top-rbhip-hop-albums-chart/
  5. https://www.billboard.com/music/music-news/backbeat-tyrese-plays-new-album-open-invitation-at-virgins-nyc-offices-1169662/
  6. https://www.npr.org/2003/09/04/1419618/r-b-sensation-tyrese
  7. https://web.archive.org/web/20070202120139/http://www.ballerstatus.net/beyond/read/id/04270158/