Nenda kwa yaliyomo

Tyler Perry

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tyler Perry
Perry being interviewed for Boo! A Madea Halloween in 2016
AmezaliwaEmmitt Perry Jr.
Septemba 13 1969 (1969-09-13) (umri 55)
Kazi yakeMwigizaji, mtayarishaji wa filamu, mwongozaji, mwandishi, mwandishi wa tamthilia, mjasiriamali
Miaka ya kazi1992–hadi sasa
MwenzaGelila Bekele (2009–2020)
Watoto1

Tyler Perry (alizaliwa na jina la Emmitt Perry Jr.; 13 Septemba, 1969)[1] ni mwigizaji, mtayarishaji wa filamu, na mwandishi wa tamthilia kutoka Marekani. Tyle ndiye mtunzi na mchezaji wa nafasi ya Mabel "Madea" Simmons, mwanamke mzee mwenye msimamo mkali, na pia hucheza kama kaka yake Madea, Joe Simmons, na mpwa wake, Brian Simmons.[2][3][4] Filamu za Perry zinatofautiana kwa mitindo—kutoka mbinu za kawaida za utengenezaji wa filamu hadi kurekodi maonyesho ya moja kwa moja ya jukwaani, nyingi kati ya hizo zilibadilishwa kuwa filamu kamili. Madea alionekana kwa mara ya kwanza katika tamthilia ya Perry, I Can Do Bad All by Myself (1999), iliyochezwa Chicago.

Perry aliandika na kutayarisha tamthilia nyingi za jukwaani, zilizofanikiwa sana miaka ya 1990 na 2000. Umaarufu wake mkubwa ulianza mwaka 2005 kupitia filamu Diary of a Mad Black Woman, aliyoiandika na kuitayarisha kama toleo la jukwaani lililobadilishwa kuwa filamu. Pia alitengeneza mfululizo wa vipindi vya televisheni, maarufu zaidi ikiwa ni Tyler Perry's House of Payne, iliyodumu kwa misimu minane kwenye TBS kutoka 2006 hadi 2012, na kisha kurejeshwa tena mwaka 2020. Mwaka 2011, Forbes ilimtaja kama mtu anayelipwa zaidi katika burudani, akiwa amepata dola milioni 130 kati ya Mei 2010 hadi Mei 2011.[5]

Mwaka 2012, Perry alisaini mkataba wa kipekee wa muda mrefu na Oprah Winfrey kupitia Oprah Winfrey Network (OWN). Mkataba huo ulihusisha vipindi vya maigizo kama The Haves and the Have Nots.[6] Mwaka 2019, alitayarisha mfululizo wa kisiasa The Oval kwa ajili ya BET.

Mbali na kazi zake binafsi, Perry ameigiza katika filamu nyingi za Hollywood kama Star Trek (2009), Alex Cross (2012), Gone Girl (2014), Teenage Mutant Ninja Turtles: Out of the Shadows (2016), Vice (2018), Those Who Wish Me Dead (2021), na Don't Look Up (2021). Perry pia amefanya kazi ya uingizaji wa sauti katika filamu za katuni kama The Star (2017) na Paw Patrol: The Movie (2021).

Filamu na vipindi vya Perry kwa pamoja vimeingiza zaidi ya dola milioni 660, na utajiri wake unakadiriwa kuwa dola bilioni 1,[7] jambo linalomfanya kuwa miongoni mwa watu matajiri zaidi kwenye tasnia ya burudani. Licha ya mafanikio ya kibiashara, kazi zake zimekosolewa na wakosoaji na wataalamu wanaoamini kuwa filamu zake zinachochea taswira mbaya au ya kudhalilisha dhidi ya Waafrika-Waamerika, na hata ukosoaji wa kazi zake kwa ujumla umekuwa hasi.[8][9][10] Mwaka 2020, Perry aliorodheshwa katika Time miongoni mwa watu 100 wenye ushawishi mkubwa duniani[11] na alitunukiwa Tuzo ya Gavana kutoka Academy of Television Arts & Sciences. Pia, alipewa Jean Hersholt Humanitarian Award na Academy Awards mwaka 2021, na mwaka uliofuata, akaingizwa katika Black Music & Entertainment Walk of Fame.[12]

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Tyler Perry alizaliwa kwa jina la Emmitt Perry Jr. huko New Orleans, Louisiana, kwa wazazi Willie Maxine Perry (jina lake kabla ya ndoa ni Campbell) na Emmitt Perry Sr., ambaye alikuwa seremala.[13] Ana ndugu watatu.[14] Perry ameuelezea utoto wake kama "jahanamu ya duniani".[15] Tofauti na baba yake mwenye ukatili, mama yake alimpeleka kanisani kila wiki, ambapo alipata faraja na utulivu fulani.[15] Akiwa na umri wa miaka 16, alibadilisha rasmi jina lake la kwanza kutoka Emmitt kwenda Tyler ili kujitenga na baba yake.[1]

Miaka mingi baadaye, baada ya kutazama filamu Precious, Perry aliguswa hadi kufichua kwa mara ya kwanza kuwa alibakwa na mama wa rafiki yake akiwa na umri wa miaka 10.[16] Pia alinyanyaswa kingono na wanaume watatu kabla ya hapo na baadaye aligundua kuwa baba yake mwenyewe alimnyanyasa rafiki yake.[17] Uchunguzi wa vinasaba uliofanywa na Perry ulionyesha kuwa Emmitt Sr. hakuwa baba yake wa kumzaa.[18]

Ingawa Perry hakumaliza shule ya sekondari, alipata cheti cha General Educational Development (GED).[19] Akiwa katika miaka yake ya ishirini, wakati akiangalia kipindi cha The Oprah Winfrey Show, alimsikia mtu mmoja akielezea namna uandishi unavyoweza kuwa tiba ya kiakili kwa kumsaidia mwandishi kushughulikia matatizo yake binafsi. Kauli hiyo ilimvutia Perry na kumhamasisha kujitosa katika uandishi. Hivi karibuni alianza kuandika barua mfululizo kwa nafsi yake, ambazo baadaye zikawa msingi wa tamthilia ya muziki I Know I've Been Changed.[20]

Jukwaani

[hariri | hariri chanzo]

Karibu mwaka wa 1990, Perry alihamia Atlanta, ambako miaka miwili baadaye tamthilia yake ya kwanza I Know I've Been Changed ilioneshwa katika ukumbi wa umma, ikiwa imefadhiliwa na akiba ya maisha ya Perry mwenye umri wa miaka 22, kiasi cha dola za Marekani 12,000 (20168).[21] Tamthilia hiyo ilijumuisha maudhui ya Kikristo kama msamaha, heshima, na kujithamini, huku ikigusia masuala kama ukatili kwa watoto na familia zisizofanya kazi vizuri. Hata hivyo, tamthilia hiyo haikupokelewa vizuri mwanzoni na ilishindwa kifedha.[22]

Perry hakuacha, na kwa kipindi cha miaka sita iliyofuata aliendelea kuiboresha tamthilia hiyo mara kwa mara, ingawa ilikumbwa na mapokezi duni. Mwaka wa 1998, akiwa na umri wa miaka 28, alifanikiwa kuiweka upya tamthilia hiyo na kuionesha tena Atlanta, kwanza katika House of Blues, kisha katika Fox Theatre. Perry aliendelea kuunda tamthilia mpya za jukwaani, akizitembeza katika mzunguko wa maonesho ya kinachojulikana kama "Chitlin' Circuit", ambao sasa unafahamika pia kama "mzunguko wa tamthilia za mijini",[1] na kuendeleza kundi kubwa la mashabiki waaminifu, hasa miongoni mwa hadhira ya Waafrika-Waamerika. Mnamo 2005, jarida la Forbes liliripoti kuwa alikuwa ameuza "zaidi ya dola milioni 100 kwa tiketi, dola milioni 30 kwa video za maonesho yake, na takriban dola milioni 20 kwa bidhaa mbalimbali", na "maonesho yake ya moja kwa moja 300 kwa mwaka huhudhuriwa na wastani wa watu 35,000 kwa wiki".[21]

Filmografia

[hariri | hariri chanzo]
Filamu za Tyler Perry
Mwaka Jina la Filamu Uhusika
2002 Madea's Family Reunion Madea
2002 I Can Do Bad All by Myself Madea
2005 Diary of a Mad Black Woman Brian, Madea
2006 Madea's Family Reunion Madea, Brian, Joe
2007 Daddy's Little Girls
2007 Why Did I Get Married? Terry
2008 Meet the Browns Madea, Joe
2008 The Family That Preys Ben
2009 Madea Goes to Jail Madea, Joe, Brian
2009 I Can Do Bad All by Myself Madea
2010 Why Did I Get Married Too? Terry
2010 For Colored Girls
2011 Madea's Big Happy Family Madea, Joe
2012 Good Deeds Wesley Deeds
2012 Madea's Witness Protection Madea, Joe, Brian
2012 Alex Cross Dr. Alex Cross
2013 Temptation: Confessions of a Marriage Counselor
2013 A Madea Christmas Madea
2014 The Single Moms Club T.K.
2014 Gone Girl Tanner Bolt
2016 Boo! A Madea Halloween Madea, Joe, Brian
2017 Boo 2! A Madea Halloween Madea, Joe, Brian
2018 Acrimony
2018 Nobody's Fool
2019 A Madea Family Funeral Madea, Joe, Brian
2020 A Fall from Grace
2022 A Jazzman's Blues
2025 Straw

Mifulizo ya Runinga

[hariri | hariri chanzo]
Mifululizo ya Runinga Tyler Perry
Mwaka Jina la Mfulizo Uhusika Maelezo
2006 House of Payne Muigizaji (Madea - mgeni) Mtayarishaji, Mwandishi, Mwongozaji
2011 For Better or Worse - Mtayarishaji, Mwandishi, Mwongozaji
2013 Love Thy Neighbor - Mtayarishaji, Mwandishi, Mwongozaji
2013 The Haves and the Have Nots - Mtayarishaji, Mwandishi, Mwongozaji
2014 If Loving You Is Wrong - Mtayarishaji, Mwandishi, Mwongozaji
2016 Too Close to Home - Mtayarishaji, Mwandishi, Mwongozaji
2018 The Paynes - Mtayarishaji, Mwandishi, Mwongozaji
2019 Sistas - Mtayarishaji, Mwandishi, Mwongozaji
2019 The Oval - Mtayarishaji, Mwandishi, Mwongozaji
2020 Bruh - Mtayarishaji, Mwandishi, Mwongozaji
2020 Ruthless - Mtayarishaji, Mwandishi, Mwongozaji
2021 Assisted Living - Mtayarishaji, Mwandishi, Mwongozaji
2022 Zatima - Mtayarishaji, Mwandishi, Mwongozaji


  1. 1.0 1.1 1.2 "Tyler Perry Biography: Film Actor, Filmmaker, Screenwriter, Playwright (1969–)". Biography.com (FYI/A&E Networks). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Septemba 9, 2015. Iliwekwa mnamo Desemba 15, 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Saul Austerlitz (2010). Another Fine Mess: A History of American Film Comedy. Chicago Review Press. uk. 444. ISBN 9781556529511. Iliwekwa mnamo Desemba 30, 2012.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "10-movies". 10-movies. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Aprili 23, 2013. Iliwekwa mnamo Desemba 31, 2012.
  4. Sheri Parks (2010). Fierce Angels: The Strong Black Woman in American Life and Culture. Random House Publishing Group. uk. 131. ISBN 9780345503145. Iliwekwa mnamo Januari 8, 2013.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Aitken, Peter C. (Septemba 13, 2011). "Tyler Perry tops Forbes' list of the highest-paid men in entertainment with $130 million made in a year". Daily News. New York. Iliwekwa mnamo Januari 3, 2023.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. "Oprah Strikes Partnership with Tyler Perry". Oprah.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-05-11. Iliwekwa mnamo Juni 1, 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. "Tyler Perry's Net Worth Is Fully $1 Billion—Here's How He Made All His Money". Cosmopolitan. Juni 14, 2023. Iliwekwa mnamo Julai 20, 2023.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. Costa, Cassie da (Januari 18, 2020). "Tyler Perry Built a Movie Empire by Selling Out Black Women". The Daily Beast. Iliwekwa mnamo Julai 20, 2023.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. "Tyler Perry: Can Black Audiences Celebrate His Success Without Enjoying His Movies? Perry continues to be a divisive figure in black cinema". IndieWire. Machi 29, 2018. Iliwekwa mnamo Julai 20, 2023.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  10. "Tyler Perry and the weight of Misrepresentation". Eastern Michigan University. Iliwekwa mnamo Julai 20, 2023.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  11. "Tyler Perry: The 100 Most Influential People of 2020". Time. Iliwekwa mnamo Septemba 23, 2020.{{cite magazine}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  12. Nazareno, Mia (2021-12-17). "Smokey Robinson, Berry Gordy, Jr. & More to Be Inducted at 2022 Black Music and Entertainment Walk of Fame". Billboard (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2021-12-27.
  13. "Perry, Willie Maxine Campbell". The Advocate. Desemba 11, 2009. Iliwekwa mnamo Novemba 5, 2010.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  14. "Willie Maxine Campbell Perry Obituary: View Willie Perry's Obituary by The Advocate". Legacy.com. Desemba 8, 2009. Iliwekwa mnamo Desemba 31, 2012.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  15. 15.0 15.1 "Tyler Perry's Traumatic Childhood".
  16. "Tyler Perry recounts childhood abuse on Web site". CNN. October 6, 2009.
  17. Park, Michael Y. (Oktoba 6, 2009). "Tyler Perry Reveals He Was Abused as a Child". People. Iliwekwa mnamo Januari 20, 2010.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  18. Hobdy, Dominique (Machi 18, 2014). "Tyler Perry: My Mother Lied About My Biological Father". Essence.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  19. "Oprah Talks to Tyler Perry". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2025-06-07. Iliwekwa mnamo 2025-06-07.
  20. "Speaker Bio: Tyler Perry". natpe.org/. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Mei 20, 2013. Iliwekwa mnamo Mei 24, 2013.
  21. 21.0 21.1 Pulley, Brett (2005-09-15). "A Showbiz Whiz". Forbes. Iliwekwa mnamo 2010-03-25.
  22. Bowles, Scott (Septemba 10, 2008). "Tyler Perry holds on to his past". USA Today. Iliwekwa mnamo Machi 25, 2010.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)