Tycho Brahe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Sanamu ya Tycho Brahe pamoja na Johannes Kepler mjini Praha

Tycho Brahe (aliyezaliwa kama Tyge Ottesen Brahe 14 Desemba 154624 Oktoba 1601) alikuwa mtaalamu wa astronomia nchini Denmark aliyejenga kituo cha kuangalia nyota cha Uraniborg.

Brahe alizaliwa katika familia ya makabaila wa Denmark akaendelea kuwa mtaalamu mashuhuri wa astronomia ya siku zake.

Alikuwa na uwezo mkwa wa kuangaia nyota na kuelewa miendo yao. 1572 aliona nyota mpya iliyoonekana kwa muda wa mwaka mmoja. Alichoona ilikuwa nyota iliyolipuka hivyo kuanza kun'gaa kwa ghafla. Alitambua ya kwamba hii nyota aliyoona kuwa mpya haikuwa sayari.

Kati ya wanafunzi wake alikuwa mwanaastronomia mashuhuri wa baadaye Johannes Kepler. Baada ya kifo cha Brahe Kepler alirithi kumbukumbu yake juu ya miendo ya sayari ikamsaidia kutunga nadharia mpya ya mwendo wa sayari.

Scientist.svg Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tycho Brahe kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.