Tume ya Biblia ya Kipapa
Mandhari
Tume ya Biblia ya Kipapa (kwa Kilatini: Pontificia Commissio Biblica) ni chombo cha kitaaluma cha Kanisa Katoliki kinachohusika na kukuza utafiti wa Biblia na kutoa miongozo kuhusu tafsiri sahihi ya Maandiko Matakatifu.
Tume hiyo iliundwa na Papa Leo XIII mwaka 1902 na sasa inafanya kazi chini ya Idara ya Mafundisho ya Imani. Inaundwa na wasomi bingwa wa Biblia kutoka sehemu mbalimbali duniani ambao huteuliwa na Papa kwa kipindi cha miaka mitano.
