Troposfia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Troposfia

Troposfia ni sehemu ya chini ya anga ya Dunia. Inasheheni asilimia 75 ya wingi wa anga na 99% ya mvuke wake wa maji na erososi. Urefu wake ni karibu kilomita 15. Ni ndefu zaidi katika tropiki (kilomita 20) na fupi kwenye ncha (kilomita 7).

Troposfia ni mahali ambapo hali ya hewa ya Dunia kama mvua, theluji, radi, au dhoruba hutokea. Mawingu yanaweza kuunda urefu wa kilomita 10-15.

Troposfia ni mahali ambapo watu wanaishi, kwa sababu inakaribia ngazi ya chini.

Safu ya pili inaitwa stratosfia. Kati ya tabaka mbili kuna tropopozi.

Katika troposfia, joto hupungua huku urefu wa uelekeo wa juu unaongezeka. Hii ni tofauti na stratosfia. Hii pia inamaanisha kwamba troposfia haina msimamo kidogo: gesi zinaweza kuinuka au kuanguka kwa urahisi. Hivyo troposfia imechanganyika vyema. Mvuto huu wenye nguvu wa anga pia husababisha mzunguko wa anga wa jumla.

Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.