Triheptanoini
| Jina la (IUPAC) | |
|---|---|
| 2,3-di(heptanoyloxy)propyl heptanoate or glyceryl triheptanoate | |
| Data ya kikliniki | |
| Majina ya kibiashara | Dojolvi |
| AHFS/Drugs.com | Professional Drug Facts |
| Taarifa za leseni | US Daily Med:link |
| Kategoria ya ujauzito | ? |
| Hali ya kisheria | ℞-only (CA) ℞-only (US) |
| Njia mbalimbali za matumizi | Kwa mdomo |
| Vitambulisho | |
| Nambari ya ATC | ? |
| Visawe | UX007 |
| Data ya kikemikali | |
| Fomyula | C24H44O6 |
| |
Triheptanoini, inayouzwa kwa jina la chapa Dojolvi, ni dawa inayotumika kutibu matatizo ya oksidi ya asidi ya mafuta ya mnyororo mrefu (LC-FAOD).[1] Hii inajumuisha upungufu wa pyruvati kaboksilasi na upungufu wa Kanitini palmitoil-transferesi ya pili.[2][3] Dawa hii inamezwa kwa mdomo.[1]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na maumivu ya tumbo, kuhara, kutapika, na kichefuchefu.[1] Kwa wale walio na upungufu wa utendaji wa kongosho, kutofyonzwa vizuri kwa chakula tumboni kunaweza kutokea.[1] Ni aina kuu ya mafuta mwilini ya mnyororo wa kati iliyotengenezwa na ni chanzo cha kalori na asidi ya mafuta.[1][4]
Triheptanoini iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2020.[1] Kufikia mwaka wa 2022, ilikuwa haijaidhinishwa Ulaya au Uingereza.[4] Nchini Marekani, iligharimu takriban dola za Marekani 5,600 kwa mililita 500 kufikia mwaka wa 2022.[5]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- 1 2 3 4 5 6 "Dojolvi- triheptanoin liquid". DailyMed. 30 Juni 2020. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2 Agosti 2021. Iliwekwa mnamo 24 Septemba 2020.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)"Dojolvi- triheptanoin liquid". - ↑ "Pyruvate Carboxylase Deficiency". NORD (National Organization for Rare Disorders). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 23 Oktoba 2022. Iliwekwa mnamo 4 Novemba 2022.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ RESERVED, INSERM. "Orphanet: Carnitine palmitoyl transferase II deficiency, myopathic form". www.orpha.net (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 27 Novemba 2021. Iliwekwa mnamo 4 Novemba 2022.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - 1 2 "Triheptanoin". SPS - Specialist Pharmacy Service. 2 Februari 2018. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 31 Januari 2022. Iliwekwa mnamo 4 Novemba 2022.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Dojolvi Prices, Coupons, Copay & Patient Assistance". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 16 Septemba 2021. Iliwekwa mnamo 4 Novemba 2022.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)