Nenda kwa yaliyomo

Tope Fasua

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Tope Fasua (alizaliwa tarehe 11 Septemba 1971) ni mjasiriamali, mchumi, mwanasiasa, na mwandishi kutoka Nigeria. Kwa sasa ni mshauri maalum wa masuala ya uchumi kwa Rais Bola Tinubu.

Alikuwa mgombea urais wa Nigeria mwaka 2019 kupitia chama cha Abundant Nigeria Renewal Party (ANRP). Pia ndiye mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji (CEO) wa Global Analytics Consulting Limited, kampuni ya ushauri wa kimataifa yenye makao makuu mjini Abuja.[1]

Kama mwanamageuzi wa kisiasa, alianzisha ANRP na akachaguliwa Februari 2018 kuwa mwenyekiti wa kitaifa wa chama hicho. Aidha, ameandika makala nyingi za magazeti na vitabu 11.

  1. Chinedu, Asadu (27 Oktoba 2023). "THE LIST: 2019 presidential candidates and their political parties". TheCable. Iliwekwa mnamo 16 Machi 2024.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tope Fasua kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.