Tom De Sutter
Mandhari
Tom De Sutter (amezaliwa 3 Julai 1985) ni mwanasoka wa zamani wa Ubelgiji aliyekuwa akicheza katika nafasi ya mshambuliaji.
Kazi yake ya awali
[hariri | hariri chanzo]De Sutter alianza shughuli zake za soka katika timu ya kwao ya KVV Balegem, ambako aligunduliwa na klabu ya daraja la tatu, Standaard Wetteren. Kutoka hapo alihamia Club Brugge, lakini hakufanikiwa kupata nafasi katika kikosi cha kwanza, hivyo akarudi kucheza katika timu ya daraja la tatu, safari hii KM Torhout 1992.
De Sutter alikaa huko kwa msimu mmoja tu, ambapo alimaliza akiwa mfungaji bora, kabla ya kugunduliwa na wapinzani wa jiji wa Club Brugge, Cercle Brugge, baada ya mchezo wa kirafiki ambao De Sutter alifunga hat-trick (mabao matatu katika mchezo mmoja).[1][2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://static.rbfa.be/project/publiek/jrinteren/speler_PH_5732.htm#itop
- ↑ https://www.fanatik.com.tr/bursaspor/tom-de-sutter-lokeren-ile-anlasti-1239919
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Tom De Sutter kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |